THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Sasa ndio umefuata zomeazomea nyingine humu?
si bora ingekuwa kijiko msingezomewa,,, bil200 escrow,, bilioni nyingi za epa,, rada, dowans,iptl,ndege ya raisi, richmond.. wakati kashfa moja tu marekani ya watergate ilienda na raisi pamoja na watendaji wote,,,, sasa kwa nini msizomewe.. toa sababu kwa nini msizomewe???
na huo ni mwanzo tunakoeendea mtapigwa mpaka na mawe nyie na viongozi wetu,, ni suala la muda tu.... wale waliolala wameanza kuamka kidogo kidogo,,,, hongera sana wazomeaji!!!!
UPI NI UKOMAVU WA KISIASA KUZOMEWA WANA CCM AU KUIBA MALI YA UMMA....
Wanajamvi ,
Hiki kitendo sikukipenda wakati naelekea Singida kuungana na katibu wangu wa CCM ndugu Kinana, tukiwa ndani ya gari tumevaa sare zetu za chama maeneo ya Ol- Matejoo kuna vijana walipotuona wakaanza kutuzomea kama vile sisi ni wezi kitendo ambacho sio ukomavu wa demokrasia nchini.
Mosi tendo hili tuliambiwa na baadhi ya makada wenzetu wanaoishi Arusha imekuwa vigumu kwao kupita barabarani na sare ya CCM.
CHADEMA acheni hiyo tabia sio ukomavu kisiasa na sio dhambi kada CCM kuvaa sare ya chama.
mmaranguoriginal. acha uzandiki. Mimi niko Arusha miaka yote na kijana ndio mavazi yangu mara nyingi. Mbona sizomewi? Hizi propaganda za kitoto zikome.
Zomeeni na migomba na miti yote yenye rangi ya kijani.