CHADEMA: A mob psychology na ole wenu

Pole sana Tundu Lissu, hizo tunaziona kama kauli ya mfa maji.... Ulitaka usikamatwe kwa tuhuma unazotuhumiwa? Acha uwoga wa mahabusu, huko panaitwa MTAKUJA. Kama ilivyo hospital.. Uende kustaki wewe kama nani hapo tarime na kwa hoja gani za msingi.. We kaa mahabusu, wenzio wanakusifia eti umaarufu wako unaongezea, haya endelea kijana, siasa si lele mama, nilikushausi tangu mwanzo pale uliponitaka ushauri kuhusu kuingia kwenye siasa... Nikakushauri kuwa mtu wa HAKI na uisimamie hata kama haki hiyo ni ya ADUI yako ili upate msaada wa MWENYEZI MUNGU lakin hautaki kunisikiliza. HAYA KILICHOKUPELEKA TARIME KUCHOCHEA WATU WAUANE NI HAKI? Pole.

Hapo kwenye red Tundu Lissu ameenda kama waziri kivuli wa sheria na katiba so lilikuwa ni jukumu lake kujua kuna defect gani kaitka suala la sheria na kusaidia ktk taarifa za uchunguzi since ndugu wa marehemu walikuwa hawaiamini serikali.
Hoja za msingi ni ukiukwajii wa haki za binadamu unaofanywa na serikali kwa ushirikiano wa karibu na polisi, ikiwamo wananchi kuhamishwa ktk maeneo yao bila kulipwa fidia, bugudha na kero nyingine kama maji ya sumu pamoja na polisi kutumia nguvu ya ziada kuua wananchi kuna taarifa kuwa marehemu wamepigwa risasi na kuuwawa wakiwa wanakimbia na sio kuaatack ka polisi wanavyosema.
Unasema kaenda Tarime kuchohchea vurugu hivi una akili kweli? ni Mh. Lissu aliyewatuma polisi kuua wananchi? Ni Lissu aliyewaambia wananchi wakatae ubani wa Milioni 3 toka serikalini na kukataa serikali isijihusishe kwa lolote. Hebu acha wehu shirikisha akili aah! nimekumbuka mgao hamna umeme so mawasiliano kati ya ubongo wako na mikono yako iliyotype hiyo thread hayana mawasilaino sababu hamna umeme hujui ulichoandika pole sana

Pukudu @Ilkidin'ga, Arusha
 
Kule si mahakama ya Kisutu ndugu yangu.

I know, lakini huyu mwanamama sina shaka atatoa tafsiri nyingine kabisa kumlainisha Ban. After all kumekuwa na mbio kadhaa za kumtaka aje home for 2015 kwa hiyo atawatetea wenziwe just in case she decides to come home!
 
Kwa wale wataalam wa sheria tunafaham Tundu hawezi toka mahabusu hadi hapo mtakapoamua nyie wanachama wake kuifanya tarime iwe shwari kiusalama. Na moja ya shart la dhamana ni akitoka mahabusu hatakiwi kuwepo eneo hilo la tukio kwa sababu za kiupelelezi hadi hapo atakapotakiwa kupanda kizimbani.. TUNAHITAJI UTULIVU WAKATI sheria inapochukuwa mkondo wake. Kama tundulisu alitaka kuwatetea marehemu angekwenda huko kisheria na jopo lake la wachunguzi bila kuhamasisha watu na bila kukisemea chama, achunguze kwa kina na kukusanya ushahidi wa kutosha kufungua kesi na kuipandisha mahakaman... Kwa jinsi ninavyomfaham huyo mdogo wangu na hekima za taaluma yake nilitarajia angefanya hivyo... Kwanin amekwendakufanya mambo anayoyajua fika yatamuharibia taaluma yake?

hivi wewe ni eng wa nini?
maana unachanganya mambo kiasi kwamba sikuelewi?
 
Mimi ni blogger sasa kuna simu nimepokea hivi punde kutoka kwa jamaa aliyejitambulisha kuwa anaitwa Richard amesema yeye ni mtu wa karibu na uongozi wa CHADEMA amenipa taarifa ya kusisimua sana kuwa mwanaharakati Tundu Lissu anajiandaa kuishtaki serikali Umoja wa mataifa kwa kile inachodaiwa kukamatwa kwake huko Tarime lakini sambamba na hilo anataka kuwasilisha malalamiko kwenye AMNEST INTERNATIONAL kuhusu kile kinachoendelea kwenye migodi nchini Tanzania.........Tungoje tuone
Waandae presentation ya nguvu,maybe a PPT,kama wana links za video za huo unyama pia wazi incorporate,wasambaze kunakohusika na pia online iwe available,hapo mtaanza kuchochea fikra za mapinduzi tuwang'oe hawa mafisadi by any means neccessary,its time to come together and act,once and for all to hasten their demise,so when we die,we will die hapilly knowing that our grand children will have a prosporous future,a better life than this bullshit,better to die for them,thats how great nations where built..through SACRIFICE for the well being of next generation!
 
T. Lissu angekwenda kule kama waziri kivuri hakutakiwa kutengeneza man power kupitia chama, angekwenda kama mtendaji mkuu.. Tatizo lililopo ni kushawish na kuchochea mgogoro hatarishi eidha kupelekea JINAI AU MADA kutokea.. Yeye anajua wapi amekosea?
 
Pole sana Tundu Lissu, hizo tunaziona kama kauli ya mfa maji.... Ulitaka usikamatwe kwa tuhuma unazotuhumiwa? Acha uwoga wa mahabusu, huko panaitwa MTAKUJA. Kama ilivyo hospital.. Uende kustaki wewe kama nani hapo tarime na kwa hoja gani za msingi.. We kaa mahabusu, wenzio wanakusifia eti umaarufu wako unaongezea, haya endelea kijana, siasa si lele mama, nilikushausi tangu mwanzo pale uliponitaka ushauri kuhusu kuingia kwenye siasa... Nikakushauri kuwa mtu wa HAKI na uisimamie hata kama haki hiyo ni ya ADUI yako ili upate msaada wa MWENYEZI MUNGU lakin hautaki kunisikiliza. HAYA KILICHOKUPELEKA TARIME KUCHOCHEA WATU WAUANE NI HAKI? Pole.

Hizi ni pumba kwelikweli
 
kiujumla chadema imekosa sababu za kuikosoa serikali ndo maana wanataka makubwa yatokee ili wapate sababu za kwenda ikulu. Na watu kama hawa wakiingia ikulu kutoka kwake ni kwa tindo. Na wamekuwa wakifanya vituko visivyo na maana.inawezekanaje watu wanasikitika watu wao wameuawa halafu wao waende wakawafariji wakiwa kama wakinanani? Kama sio laana nini?
 
Mimi ni blogger sasa kuna simu nimepokea hivi punde kutoka kwa jamaa aliyejitambulisha kuwa anaitwa Richard amesema yeye ni mtu wa karibu na uongozi wa CHADEMA amenipa taarifa ya kusisimua sana kuwa mwanaharakati Tundu Lissu anajiandaa kuishtaki serikali Umoja wa mataifa kwa kile inachodaiwa kukamatwa kwake huko Tarime lakini sambamba na hilo anataka kuwasilisha malalamiko kwenye AMNEST INTERNATIONAL kuhusu kile kinachoendelea kwenye migodi nchini Tanzania.........Tungoje tuone

Kwa bahati mbaya wewe pamoja na Tindu hamjui serikali,UN,Amnesty International na owners wa migodi ni akina nani.Hao ni watoto wa baba mmoja,kwa hiyo anachofanya ni kama kupeleka kesi ya ngedere kwa nyani.Nothing will come out of it.Niseme hivi,we are surrounded.Sisi ni kondoo wanaoelekezwa machinjoni.Huo ndio ukweli, whether you like it or not.
 
Nawashauri wana JF wasijibishana na mtu anayejiita Zhu au Bollo Yang. Ni mtu mmoja aliyepandikizwa JF na Mafisadi wa hoja zisizona tija kwa taifa ili kuvuruga motions mbalimbali. Ana ID nyingi ... nafatilia nyendo zake na baada ya muda tutamweka kiti moto.
 
hilo jina ni Tindu Lissu au Tundu Lissu? mnatuchanganya

Dogo vipi, upo?
Hivi zile pesa zilizorudishwa na wezi wa EPA na dingi wako kuamuru zipelekwe na kufunguliwa 'window' pale TIB zimepotelea wapi?
 
Siamini kama nchi hii inahitaji kuwalinda Barrick kiasi hicho. Barrick ni kampuni yenye matatizo Duniani kote!
Kweli Polisi wanalinda Barrick au ni mazoea ya kuuwa raia wake?

Angalia mauaji ya Pemba enzi ya Mkapa. Angalia mauaji ya Arusha, angalia vifo vya watuhumiwa ktk vituo vya Polisi,
Na sasa angalia vitendo vya Polisi huko Tarime.

Mauaji ya Tarime ni jambo baya lakini baya kuliko yote ni hii hali ya Polisi kutoona kwamba walifanya kosa, na kuendelea kujihusisha na hao maiti.

Polisi wanaagizwa na nani?
Kama hawana anayewaagiza kwa nini hawaogopi utawala wa juu wa serikali?

Kukosekana kwa woga ktk matendo kama haya ni wazi kwamba Mwema, Pinda, Kiwete wote wanaunga mkono mauaji ya Raia wake.

Na kama inatokea Libya, matendo ya Gadafi kuchunguzwa na ICC kwa nini Kikwete asichunguzwe?

Ni hatua zipi zinazofuatwa ili kumuita Ocampo?
 
Pole sana Tundu Lissu, hizo tunaziona kama kauli ya mfa maji.... Ulitaka usikamatwe kwa tuhuma unazotuhumiwa? Acha uwoga wa mahabusu, huko panaitwa MTAKUJA. Kama ilivyo hospital.. Uende kustaki wewe kama nani hapo tarime na kwa hoja gani za msingi.. We kaa mahabusu, wenzio wanakusifia eti umaarufu wako unaongezea, haya endelea kijana, siasa si lele mama, nilikushausi tangu mwanzo pale uliponitaka ushauri kuhusu kuingia kwenye siasa... Nikakushauri kuwa mtu wa HAKI na uisimamie hata kama haki hiyo ni ya ADUI yako ili upate msaada wa MWENYEZI MUNGU lakin hautaki kunisikiliza. HAYA KILICHOKUPELEKA TARIME KUCHOCHEA WATU WAUANE NI HAKI? Pole.

Mpumbavu sana wee mayeye...umshauri wewe kama mkewe?
 
Well, hali ya Tanzania ni tete kiusalama. Polisi hawaaminiki tena kwa raia au wageni wa nje. Barrick wenyewe wametoa tamko la kushangazwa na mauaji hayo lakini viongozi wetu bado wanayaendeleza na mbaya zaidi wanayafanyia siasa za maji taka.

Serikali ya Tanzania imekosa kabisa utu. Tatizo ni kuwa akina Kagasheki wanaendesha serikali wakiwa Dar wakati wenzao akina Tindu wako Tarime kwenye tukio.

Kuna matumaini kuwa unapopiga kelele watu wakasikia wapo watakaosema na wapo watakao nyamaza. Tupige kelele kwenye jumuia za kimataifa na hapo ndo tutaona walio upande wetu. Naamini kuna mashirika na taasisi za kimataifa zitapiga kelele nasi.
 
Kwa bahati mbaya wewe pamoja na Tindu hamjui serikali,UN,Amnesty International na owners wa migodi ni akina nani.Hao ni watoto wa baba mmoja,kwa hiyo anachofanya ni kama kupeleka kesi ya ngedere kwa nyani.Nothing will come out of it.Niseme hivi,we are surrounded.Sisi ni kondoo wanaoelekezwa machinjoni.Huo ndio ukweli, whether you like it or not.

.
Ni afadhali tuzingirwe na hao weupe kuliko kuzingirwa na huyu kowadi, mweusi mwenzetu. Nyoka wa ndani ya nyumba ndie hatari kuliko wale waliopo vichakani, mbali na nyumba.
.
 
Ni vigumu kuamini lakini ni vema nieleze hisia za Watanzania.Kamanda wa Mkoa wa Mara elewa kuwa Tanzania imefikishwa mahali pagumu sana na Sera mbovu za chama cha mapinduzi Ccm na order unazopewa wewe na kutekeleza zinaweza kukugeukia na kuwa Hukumu ya milele kwako.NAOMBA UWAACHIE HAO VIONGOZI WA CHADEMA KABLA YA KESHO SAA SITA MCHANA KWANI BAADA YA HAPO YATAKAYOTOKEA TANZANIA NI HASIRA ZA WATANZANIA WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI YAO.Kumbuka kesho saa sita eleweni sisi wote tuna roho za nyama na unyama unaofanywa na uonevu unakatisha tamaa kabisa ya kuishi.MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU WABARIKI WAPENDA HAKI
 
Wote tumeona ITV walivyoonesha Majeneza ya ndugu zetu Wakristu yakiwa yametupwa porini. Najiuliza hivi wamefanya vile kwa sababu Marehemu wale walikuwa ni Wakristu au kwa sababu walikuwa wafuasi wa CHADEMA?

Naendelea kujiuliza je majeneza yale yangekuwa ya ndugu zetu Waislam je utawala huu wa Mrisho na CCM yake ungeliyatendea vile majeneza yale?

Au ni muendelezo wa Serikali dhalimu ya Kikwete dhidi ya Wakristu?
 
Back
Top Bottom