CHACHANDU YA PILIPILI) yaani pilipili ya kusaga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHACHANDU YA PILIPILI) yaani pilipili ya kusaga

Discussion in 'JF Chef' started by ndetichia, Jun 5, 2012.

 1. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,637
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Jinsi ya kutayarisha (CHACHANDU YA PILIPILI) yaani pilipili ya kusaga..

  Mahitaji:
  1.Pilipili
  2.Tangawizi
  3.Kitunguu saumu
  4.Ndimu natural au mchina
  5.Chumvi
  6.Nyanya
  7.Kitunguu maji na
  8.Mafuta ya kupikia
  9.Maji kwa ajili ya kusaidia kusagia kwenye blenda

  Jinsi ya kupika
  Changanya kuanzia 1 hadi 6 kwa kuvisaga kwenye blenda ukishamaliza, weka mafuta yako jikoni kisha tia kitunguu maji kikiiva weka ule mchanganyiko wako kwenye hayo mafuta pika mpaka maji yapungue uone mafuta. Hii husaidia chachandu yako ikae muda mrefu bila ya kuharibuka..

  Cheers!
   
 2. S

  SHERRIE Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alternatively, unaweza kutumia carrots badala ya nyanya halafu unablend mahitaji yote pamoja na vitunguu maji pia. Unabandika jikoni, unaweka mafuta ya kupikia kiasi vinachemka pamoja. hii inakuwa na utamu kwa mbaaaali kutokana na carrots ulizotumia.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,637
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  oooh thanx kwa hiyo mupya..
   
 4. Siri Sirini

  Siri Sirini JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na nyingine wasaga kwa pamoja
  nyanya 1
  kitunguu maji 1
  swaumu kisi
  tangawizi kiasi
  karoti 1
  tango 1
  na pilipili jinsi upendavyo, ukimaliza waweka ndimu na chumvi, ni tam sana.
   
 5. m

  mama dunia JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kuna mchanganyiko mmoja tulikuwa tunaenda nao shule-boarding wakati huo miaka ya 98 hivi ila nimesahau ilikuwa inachanganywa vipi, tulikuwa tunaweka na vipande vya nyama nao ulikuwa mchachandu mzuriii sana
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 20,603
  Likes Received: 3,086
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
Loading...