Natamani Prf.Lipumba angepata taarifa hizi.
Lakini jamani madaraka yanalevya.
Si mmemsikia rais wa Nigeria!
Mpango ilikuwa akae madarakani kwa muda tu lakini sasa ameamua kutangaza nia kuwa atagombea nafasi hiyo ili aendelee kula kuku.
Rutaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa awali ya yote pole kwa majukumu. Usihadaike na ahadi za wanasiasa kijana especial yule asiejua tamu ya uongozi akiona atasutwa atakuja na eeeh wazee wameniomba niendeleee watu makofi pwapwapwapwa! hao ndio wana si hasa
ahadi zake nyingi haziwezi tekelezeka katika miaka mitano
mfano barabara na reli huhitaji mambo mengi mpaka imalizike. kuna upembuzi yakinifu, kutafuta contractors na consultants kwa tendering na hata ujenzi wenyewe.
"Tangu mwanzo waliponiomba nilikubali...... ", Kwa kawaida huu usemi huwa si mzuri sana kwani uongozi ni wito na si kuombwa. Nadhani kauli nzuri ingekuwa ni "Tangu mwanzo nilipoamua....." huo ni ushauri kwa Dr. au aliyeandika kijarida hicho.