CEO na Bodi ya Simba

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,910
5,081
Manara kama mwajiriwa anawajibika kufuata sheria za kazi kwa mapana yake.

Lakini hili la kuanza kutukana mkuu wake wa kazi hadharani kwenye mambo ya kazi na tena kwa ushahidi kabisa! Hilo ni kosa kubwa. Pamoja na yeye kufanya kazi anayosema ni kubwa ya jasho na damu lakini kila mtu anafanya hivyo kazini kwake na hulipwa malipo kama compasation.

Yaani yeye anatakaga awe mkubwa kuliko CEO wake hiyo ni structure ya wapi tena jamani! Mwenyekiti wa bodi hapo hamna usuluhishi Bali ni sheria zifuatwe inavyotakiwa hata kama kutakua na gharama kidogo. Hatuko desperate sana na confederation cup hadi kufikia kuua discipline ya team. Kama mkimuachia Manara basi na akina Mkude muwaache tu Bila kuwa na nidhamu.

Mara atukane waandishi mara atukane wachambuzi, mara atukane kila mtu! Sasa joka limefugwa linataka kumla mfugaji.

Kwa level ya Simba kinatakiwa kichwa kitulivu pale.

Halafu anapenda sana kutukana wanawake hadharani!!
 
Barba ni jipu.
Na sisi wanasimba hatutakubali kuona hili jipu likitaka kuiharibu brand yetu.Wanasimba tuko nyuma ya Manara.Ameitumikia club hii kwa jasho na damu na sisi ni mashahidi
Na ujinga wenu ulobebwa na uzezeta, mnaona wenyewe mmepata msemaji wa team!

Kwa Watanzania ni basi tu, ila Ulaya Huyu angecost team mara nyingi sanaa. Msemaji wa team, muda wote unasemea vibaya team zingine KWA kashfa na kejeli, unahamia KWA watu binafsi kuwadhalilisha na kejeli KWA waandishi wa habari?

Huyu ni vile kakuta Watanzania wastaarabu na mashabiki mazezeta ya Simba, Ila ile cream ya Simba walishajuaga hapa kuna mtu zimenyofoka mbili tatu
 
Wahuni bhana Manara na elimu yake ya ngumbaru anasikitika kulipwa laki saba anataka kuishi maisha ya kina Diamond kwa maisha ya kulipwa mshahara, wale wahuni wanatafuta wenyewe mambo ya hovyo hovyo kila kukicha hiyo nafasi inataka mtu muelewa sio Manara na Simba ipo na itaendelea kuwepo hata bila Manara.. Angetoka damu angekuwa hai maneno ya kina Kaduguda hayo watu hawawezi kuishi bila Simba...
 
Barba ni jipu.
Na sisi wanasimba hatutakubali kuona hili jipu likitaka kuiharibu brand yetu.Wanasimba tuko nyuma ya Manara.Ameitumikia club hii kwa jasho na damu na sisi ni mashahidi
Manara hana busara, binafsi namwona kama anatumia ulemavu wake Wa ngozi kama ngao ya kugombana hovyo na watu.

Jerry Muro, Maulid Kitenge, Prisca Kishamba na wengine wengi ni baadhi ya watu ambao ameingia nao kwenye mgogoro bila sababu za msingi.

Kiufupi Manara ana mambo ya kike sana, kupenda kusutana.
 
Manara kama mwajiriwa anawajibika kufuata sheria za kazi kwa mapana yake.
Lakini hili la kuanza kutukana mkuu wake wa kazi hadharani kwenye mambo ya kazi na tena kwa ushahidi kabisa! Hilo ni kosa kubwa. Pamoja na yeye kufanya kazi anayosema ni kubwa ya jasho na damu lakini kila mtu anafanya hivo kazini kwake na hulipwa malipo kama compasation...
Hebu wekeni hapa na sisi tumhukumu ana hatia au hana? Si kila mtu humu amemsikia Manara akitukana japokuwa Mimi nasisitiza mara kwa mara Manara hana hadhi ya kuwa msemaji wa Simba. Hana tofauti na Jerry Muro kwa Yanga kipindi kile.
 
Barba ni jipu.
Na sisi wanasimba hatutakubali kuona hili jipu likitaka kuiharibu brand yetu.Wanasimba tuko nyuma ya Manara.Ameitumikia club hii kwa jasho na damu na sisi ni mashahidi
Hapana sio kweli! ndio Manara katoa mchango wake mkubwa kwa SSC lakini sidhan kama SSC bado inahitaji kuendeshwa kwa hamasa tena.

Ni muhimu mambo kama nidhamu, mshikamano, uwazi, uwajibikaji vizingatiwe vitu ambavyo Babra ana offer kwa timu japo si kwa kiwango kizuri ila atleast she does her part well.

Manara yupo kwa peak lakini naona ni kama kashindwa kumudu status anayoenjoy kwa sasa and probably tunaweza witness his demise,who knows.

Mi shabiki wa SSC but I wasn't happy with how he responded to Prisca(Clouds Media Employee).The man sounded unprofessional and that was not to be tolerated by the management of SSC .To make it shorter, the man needs to step aside and this is my opinion coz we can not move foward with people of his category. Thank You!
 
Wahuni bhana manara na elimu yake ya ngumbaru anasikitika kulipwa laki saba anataka kuishi maisha ya kina diamond kwa maisha ya kulipwa mshahara wale wahuni wanatafuta wenyewe mambo ya hovyo hovyo kila kukicha hiyo nafasi inataka mtu muelewa sio manara na Simba ipo na itaendelea kuwepo hata bila manara..angetoka damu angekua hai maneno ya kina kaduguda hayo watu hawawezi kuishi bila Simba...
Mnakumbuka huyo mabara alikuwa mwenezi wa ccm mkoa wa dar,hivi mnajua alikimbia na hela ccm?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana ikawa Haji ana makosa, likewise inawezekana ikawa Barba ana makosa.

Lakini swali langu kubwa ni MOJA TU.Kwanini kila mfanyakazi wa simba akifukuzwa Simba katika interview zao lazima wanatupia lawama zao Kwa CEO,barba iwe direct or indirect.

Sijawahi sikia mfanyakazi yoyote wa simba akimlaumu manara tokea nimeishabikia simba, sijawahi kumsikia mfanyakazi yoyote wa simba akimlaumu CEO aliyepita MAGORI wala sijawahi kumsikia mfanyakazi yoyote wa simba akimlaumu CEO aliyepita SENZO

Lakini kwa siku za hapa karibuni,kila mfanyakazi aliyefukuzwa simba alikuwa akitupia lawama zake kwa barba,kwa mfano CEO SENZO mwenyewe aliwahi kusema kuna wali walikuwa wanampinga ambao hawakuwa kwenye management yake,habari za kiinteligence zikasema kuwa alikuwa ni barba akichochea Moto ili achukue nafasi.

Hali kadhalika kwa swebi na kashembe kila mmoja amekuwa na manung'uniko na management ya Barba.

Ni dhahiri kuwa barba ana aminiwa sana na Mo kwani alianza kufanya kazi kwenye kampuni zake kabla ya kumleta pale Simba,so ni ngumu sana kwa mtumishi yoyote yule mwenye mawazo tofauti na Barba kuendelea ku-survive pale Simba.

Haji anaumaarufu mkubwa sana kuliko mtu yoyote pale Simba,hiki kitu nadhani ndio kinamfanya barba awe na wivu.Angalia hata project nyingi za Simba, Barba huwa anajipa credit yeye mwenyewe badala ya kuipa credit management yote ya simba,hii ni selfish behaviour na ni mbaya sana kwa mustakabali wa timu.Anapenda sana kujipa utukufu mwenyewe pasipo ku recognise efforts za watendaji wengine.

Kama umeisikiliza ile clip ya manara utagundua kuwa haji anaongea kwa hisia sana,ni dhahiri kuwa kulikuwa na sintofahamu ya muda mrefu na ameivumilia sana sasa kaamua kutema nyongo.

Huu ugomvi utawagawa mashabiki wa Simba na viongozi wao.Barba anaungwa mkono na Mwenyekiti wa Bodi huku manara akiungwa mkono sana na mashabiki wa Simba,so maamuzi yanapaswa kuwa ya uangalifu sana.Ni vyema wakae chini watatue kwa amani.

Sioni kosa lolote kwa manara kukutana na watu wa GSM.Yule ni celebrity lazima atumie uamarufu wake kutafuta kipato.

Kuwa ambassador wa kampuni ambayo ni mshindani wa boss wako kibiashara sio kosa,hilo ni swala la ujajusi wa KIUCHUMI hapo Barkhera kawin hiyo game,alichopaswa Mo ni kumshawishi Manara awe ambassador wake na sio kuleta chuki.
 
Mkuu kitu cha kujiuliza sio idadi ya watu wanaomlalamikia CEO Barbra, cha kujiuliza ni je, waliondolewa kwa haki na kwa mujibu wa taratibu stahiki ?
Sio wakati wote malalamiko yanamaanisha innocence ya mtu.
Kama anakwaruzana nao katika kusimamia misingi ya kazi, acha awaondoe hata wakiwa LAKI TISA.
Cha msingi ni kwamba isitokee hata mtu mmoja akaondolewa kwa kuonewa.

Pili, approach aliyoitumia Haji kuleta mambo ya kazi kwenye mitandao ya kijamii ni mbaya sana. Hata kama anaonewa, zipo taratibu za kiofisi za kushughulikia haya mambo, anaweza kuonewa na Barbra lakini hawezi kuonewa na watu wote walipo pale Simba.
Kama si wakati huu, basi wakati mwingine wowote, Manara atakuja kupoteza haki na stahiki zake nyingi sana (ikiwemo heshima) kwa kuleta mambo ya ndani huku nje kwa sisi waswahili wenzako (instagram, twitter, facebook, redioni na kwenye TV)
 
Mwaka ambao Simba hawatachukua vpl ndo itajulikana kama Mo ni Mfadhili wa club au Mwekezaji.

Kwasasa watu hawataki kuungalia mfumo mbovu uliopo Simba sababu timu inashinda lakini Pana shida kubwa ni suala la muda tu. Haya yanayoibuka ni viashiria vya tatizo lenyewe.
 
Back
Top Bottom