CEO Barbara: Tumepokea simu nyingi baada ya Tuzo ya goli bora la CAF, klabu kadhaa zikimuhitaji Sakho

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Klabu ya Simba kupitia kwa Mtendaji Mkuu wao (CEO) Barbara Gonzalez, amethibitisha kuwa hadi kufikia sasa wamepokea simu nyingi sana kutoka klabu kadhaa zikiwemo vigogo wa Afrika Wydad na Raja, zikimuhitaji nyota Pape Ousmane Sakho ambaye jana usiku alitwaa Tuzo ya goli bora la CAF 2022.

"Ukweli ni kwamba Simba SC tumepokea simu nyingi sana, klabu kadhaa tangu jana usiku wamekuwa wakihitaji tumalize biashara, wengine wanamfuata mchezaji wakitaka tumalizane, presha ni kubwa sana kiukweli ila mwisho wa siku zinazipima"

"Viongozi wake wa Senegal wanashangaa na wanauliza kwanini anacheza Tanzania.! walikuwa wanamwambia anapaswa kuondoka sasa na ni lazima aondoke akacheze mbele zaidi ya hapo"

"Utamaduni wetu kama Simba ni kuwapa fursa wachezaji wetu, ikitokea wamepata ofa nzuri hakuna shida, nikikuambia nina ofa zaidi ya mbili kwa ajili ya mchezaji Sadio Kanoute utakubali? Wachezaji wetu wengi wana ofa kutoka nje, ila ni lazima tukae chini tutafakari"

"Simba bado hatujamaliza usajili, hata hapa Morocco kuna baadhi ya wachezaji nafuatilia, nisingependa kutaja idadi ila tuna maingizo mapya tunakamilisha". CEO Barbara Gonzalez.
20220722_001754.jpg
20220722_001742.jpg
20220722_080337.jpg
 
Simba SC imejitengenezea Kijiji cha kipekee sana nchini Tanzania

Kipindi hiki Simba SC ni maarufu sana Afrika na Tanzania

Performance ya Pape Sakho (Pop Machine) ikiendelea kuimarika anaenda kuwa biashara nzuri sana.
 
1658480402449.png

Barbara: Ukweli ni kwamba Simba tumepokea simu nyingi sana, klabu kadhaa tangu jana usiku wamekuwa wakihitaji tumalize biashara, wengine wanamfuata Mchezaji wakitaka tumalizane, presha ni kubwa sana kiukweli ila mwisho wa siku tutazipima”

Barbara: Simu zimekuwa nyingi sana kwa Pape, Viongozi wake wa Senegal waliuliza kwanini anacheza Tanzania, walikuwa wanamwambia anapaswa kuondoka sasa na ni lazima aondoke akacheze nje ya hapa” CEO

Barbara: Utamaduni wetu kama Simba ni kuwapa fursa wachezaji wetu, ikitokea wamepata ofa nzuri hakuna shida, nikikwambia nina ofa zaidi ya mbili kwa ajili ya Kanoute utakubali? Wachezaji wengi wana ofa kutoka nje, ila lazima tutakaa chini kutafakari”
 
Binafsi Mimi sio shabiki mkubwa wa Pape Sakho lakini to be honest jamaa katisha na kalifanyia soka la bongo Jambo kubwa Sana tena sana.

Ukweli ni kua ligi ya bongo itaanza kufatiliwa Sana na itaangaliwa kwa sura tofauti.. hapo pia niwapongeze watani Simba Sc kwa kuupiga mwingi huko duniani CAF.

Kama kweli Kuna ofa ni Bora P.O.P auzwe tu kwa masilahi mapana ya club na ya mchezaji. Ujue mchezaji Kama Sakho anatoka nchi ambayo ndio namba moja kwenye viwango vya mpira Africa so anaaminika Sana huko duniani. Ni rahisi kwa Sakho kusajiliwa huko ufaransa kuliko fei Toto kutoka Tanzania hata Kama ndo angekuwa ameshinda goli maana angeonekana ameotea tu. Trust me sahivi Sakho ni bidhaa adimu sokoni. Wakifika bei muuzeni na najua hamtasahau kile kipengele muhimu kua Simba italipwa kadiri atakavokua akiuuzwa kwende klabu kubwa zaidi.
 
Asante Wakipekee kwa uchangiaji uliokuwa bora kabisa bila ushabiki..!
 
Moja ya kazi nzuri za Gomes nawashauri Simba wasimuuze Kanoute au Banda ila Sakho wanaweza kumuuza kwani ameshafika 25 lakini waachane na kina Kagere, Boko na Mugalu ambayo ni majeruhi mara Kwa mara.
Hao viongozi wa Senegal waache unafiki wamuite timu ya taifa
Kocha wao mbna jana kamuambia kuwa ajiandae na safari ya World Cup. Na Mane nae akakazia tena.

Weuweeeeeeeeeeeeeh.
 
Moja ya kazi nzuri za Gomes nawashauri Simba wasimuuze Kanoute au Banda ila Sakho wanaweza kumuuza kwani ameshafika 25 lakini waachane na kina Kagere, Boko na Mugalu ambayo ni majeruhi mara Kwa mara.
Hao viongozi wa Senegal waache unafiki wamuite timu ya taifa
Kanute nae yumbioni kuuzwa 😥
 
Back
Top Bottom