CECAFA Senior Challenge: Kutoka Uganda

So far Kaseja amecheza karibu mechi zote tangu Maximo aondoke (Maximo alikuwa anadai ni mfupi na hana nidhamu). Tuseme nidhamu yake imegeuka ghafla na kuwa nzuri? Ameferuka?
 

Mkuu, football ni mchezo wa makosa, tuhuma kama hizi siyo nzuri bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwamba alikula mlungula kutoka Kenya.
 
kama kazimoto kashinda huwa aliongezeki ref gemu ya msumbiji goli lakusawazisha..
 
Kipindi cha pili kinaanza...
Frank Domayo anaingia badala ya Idd Athuman Chuji
Kilimanjaro Star 1 - 0 Zanzibar Heroes
 
Dk 47 Zanzibar wanafanya shambulizi moja kali, Kaseja anaokoa kwa ustadi mkubwa
 
Zanzibar wanaonekana kuanza kwa kasi kipindi hiki cha pili, wanacheza na kumiliki sana mpira.
Kili Stars bado hawajatulia...
 
Dak. 52 Zanzibar wanaonekana kutaka goli, Kaseja anapata wakati mgumu. Bado 1-0.
 
hawa wazenji wanasawazisha soon too maana watanganyika ni pumba balaaa....
 
Dk 51 Abdallah Seif wa Zanzibar anashindwa kutumia nafasi ya wazi akiwa amashampita beki wa mwisho...
 
Dk 55 Zanzibar wanafanya shambulio zuri...Kili wanaokoa
 
Muda wote kocha wa Zanzibar Heroes anaonekana kasimama, akijiongelesha mwenyewe...nadhani anashindwa kuamini kile kinachofanywa na wachezaji wake uwanjani maana wanakosa nafasi za wazi sana...
 
Zanzibar wanapata freekick...Kaseja anapangua shuti moja kali sana na mpira unaondoka katika eneo la hatari
 
Mashabiki wa Kenya wanaonekana kuishangilia sana Zanzibar Heroes...
 
Dk 67 John Booco anakuwa offside baada ya kugongea moja mbili na Mwinyi Kazimoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…