CECAFA Senior Challenge: Kutoka Uganda

Naona mashabiki wa kibongo wanawakilisha vema......

Wengi itakuwa ni wanafunzi waliopo Uganda
 
hahaha, mkuu acha hasira bado hajakosea sana bado anakaba vizuri ingawa kushambulia yupo taratibu...

dogo boya sana toka kitambo sana ila magazeti ndio yanampaisha tu..
 
Haya mkuu ngoja twende mapumziko tukirudi tutupie tena tuwili tukalale unono leo.
 
kuna jamaa wengine kama 80 wanatoka Bukoba, walienda huko jana...

Ukiangalia vizuri walipo mashabiki wa Tanzania utaona kuna bango kubwa sana limeandikwa Bukoba Veteran hao jamaa wanaonekana ni hatari kwelikweli,halafu si unajua Bukoba mjini na Kampala ni karibu sana??!!!
 
dogo boya sana toka kitambo sana ila magazeti ndio yanampaisha tu..
Hapana mkuu, dogo anacheza vizuri na anujua mpira hasa.....

Timu zako za Azam na Simba zilichemka kwa huyu dogo, mechi zote 2 za Yanga na Azam mwaka huu(Kagame cup finl na ile ya VPL) dogo kakamua ile mbaya....Mechi ya Simba aliisumbua ngome ya Simba mpaka Nyosso akamtafutia kadi....

Mengine nadhani ni chuki binafsi....

Vijana wa U20 aina ya Jonas Mkude, Sure boy, Chris Edward, Rama Singano, Shomari Kapombe, Simon Msuva na Frank Domayo wanacheza mpira mzuri sana na ndio Taifa Stars aijayo ambayo nina uhakika wataliletea sifa kubwa sana Taifa letu....Sidhani kama ni busara kuwabeza, tunapaswa kuwaunga mkono kwa kila hali....
 
Sisi Wa Nje KUNA link ya KUONA GAME???

Samahani Mkuu sijakuelewa unamaanisha nini unaposema kwamba ninyi wa nje!lakini kama umejiunga na Super Sport Phone unaangalia unono sana kwenye Chanel 9 East.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…