CECAFA ikiwa na watu kama Musonye haiwezi kupata wadhamini wa maana. Lazima aondoke ili iendeshwe kisasa zaidi. Yeye anawaza hela za mlangoni mpaka leo.
nani anasema kwamba afrika inajitawala ? Watu kama musoye bado wanatutawala akili zetu , kwani vijana hawana haki kuonyesha vipaji vyao ?both sides are wrong yanga and cecafa ,lakini kuwanyima haki vijana wa yanga ni mbaya zaidi .cecafa ikiwa na watu kama musonye haiwezi kupata wadhamini wa maana. Lazima aondoke ili iendeshwe kisasa zaidi. Yeye anawaza hela za mlangoni mpaka leo.
Hawa wawakilishi wa TFF katika BONANZA LA MUSONYE wanafnya kazi ya kubutuabutua tu dk ya 45 bado bilabila. Mashabiki kiduchu,nadhani Musonye mwakani ataileta Tanzania.
Labda kwa wazanzibar manake wanaweza kuwanunua....azamfc kwa mpira wa jana si wakuwalaumu naamini mechi zinafuatia watacheza vizuri hilo nauhakika
Teh, usiniambie ni mambo ya Zanzibar si Nchi?View attachment 176622Hawa UKWELI na UHAKIKA ni kweli mashindano haya ni ya nchi TANO tu? Mbona bendera ya Zanzibar haipo hapo?
AZAM FC imeanza kwa sare ya bila kufungana na wenyeji Rayon katika mchezo wa ufunguzi Klabu Bingwa AfrikaMashariki na Kati, CECAFA Kagame Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
Azam ilicheza vizuri na bahati haikuwa yao tu hawakuweza kupata mabao na nafasi ambayo wataikumbuka zaidi niya mapema tu sekunde ya 24, shuti la Himid Mao ‘Ninja' lilipogonga mwamba na kwenda nje.
Pamoja na kwamba walicheza nyumbani, lakini Rayon walifurahia sare na mabingwa hao wa Bara, kwani walikuwakwenye hatari ya kupoteza mchezo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, KipreBalou, Himid Mao/Mudathir Yahya dk89, Salum Abubakar ‘Sure Boy', John Bocco ‘Adebayor', Kipre Tchetche naKhamis Mcha ‘Vialli'/Didier Kavumbangu dk70.
Rayon Sport; Bikorimana Gerard, Ndayisenga Fuad, Nizigiyimana Karim, Sibomana Bakari, Serugendo Arafat,Tubane James, Leon Uwumbazimana/Hategekimana Aparodis dk67, Sibomana Hussein, Ndatimana Roberts, YossaBetrand/Sekle Zico dk88 na Motombo Govin/Kambala Salita dk78.
Kuna mwaka mashindano yaliwahi kuchezwa miaka kadhaa mfululizo hapa Darisalama, kwetu kuna hamasa kuliko popote katika kanda huu.pale kigali mwaka huu yamepoa sana. nimeamini tz mpira unapendwa watu huwa wanajaa, lakini huko kwingine naona viti vitupu vingi sana. labda jana tu wakati APR na ATLETICO wanacheza.
Kuna mwaka mashindano yaliwahi kuchezwa miaka kadhaa mfululizo hapa Darisalama, kwetu kuna hamasa kuliko popote katika kanda huu.