CDM yamhenyesha Pinda uingereza

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
Waziri mkuu Pinda amefanya ziara isiyokuwa na miguu wala kichwa nchini Uingereza. Akiwa huko alipata habari za uwepo wa mkutano wa wanachadema uliongozwa na Wenje amabye ni mkurugenzi wa mambo ya nje wa CDM na Munishi ambaye ni katibu Mkuu wa BAVICHA.

Habari zilizovuja zinasema Pinda aliamua kumshinikiza Balozi wa Tanzania Uingereza kuitisha mkutano wa wana CCM kwa mgongo wa jina "WATANZANIA" siku ya Jumanne ya terehe 16/10/2012 ubalozini baada ya kusikia CHADEMA wamekutana ijumaa iliyopita na kuazimia kuisambaratisha CCM Uingereza.

Katika mkutano huu walijitokeza watu wasiozidi 15 na taarifa za ndani zinadai Pinda ametamka ndani ya kikao hicho kuwa CHADEMA ni "KIBOKO" kwani siku za nyuma walizoea kupata mapokezi makubwa yenye mbwembwe kama viongozi wa serikali lakini baada ya CDM kujikita nje kwa siku za hivi karibuni , hali hiyo imetoweka na kuwaduaza viongozi wa serikali.

Ikumbukwe wiki tatu zilizopita, makamu wa rais Gharibu Bilal alifanya ziara kama hiyo nchini Uingereza na kuambulia patupu.

Viongozi wa CDM walifanya mkutano wao tarehe 12/10/2012 jijini London na kukusanya idadi kubwa ya watu kutoka miji ya Reeding, Birmingham na London na baadhi ya watanzania waishio huko walijiunga na CDM.

Source: Mtanzania aliyekuwapo mkutanoni kwenye ubalozi wa Tanzania London.
 
mh.pinda anajenga demokrasia nchini au ni mbomoaji .hebu fuatilia ziara zake anzia mikoani mfano mwanza ,nenda uingereza .historia itatuambia amefanyia nini tanzania
 
Pinda anamuiga bosi wake ku-Vasco da Gama. Huyu Oman yule UK, wakati nchi inateketea kwa vurugu.
 
Hizo zinaitwa Tantararira wafuasi wa Chadema Uingereza hawazidi 20 kina Chilisosi, Uingereza Watanzania wengi ni Wapemba nao wamejiripuwa.
 
Last edited by a moderator:
...je na hao Watanzani wanaoishi UK waliogoma kuudhulia huo mkutano wa Pinda walipewa viroba?...
 
ni kweli watu walikuwa wachache pale ubalozini. Watu wengine mnaishi tz lakini nashangaa kusikia asilimia kubwa wanaoishi uk ni wapemba. Chunga ulimi ndugu yangu hujawahi kufika hapa UK watu wana kazi zao za maana sijui nani anawadanganya kwamba watu wamejilipua!!! CCM ni chama mfu hakuna wa kukifufua. Nilikuwepo kwenye mkutano wa Wenje hivyo sioni sababu ya watu kudanganya.
 
Hebu tuwekee picha ya jinsi mkutano wa Pinda ulivyokuwa basi. Na huo mkutano wa Wenje na Munishi kama anavyodai SCOLARI ulikuaje? Nini kilijiri. Hebu shuhudia
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Chadema bana badala ya kujenga chama vijijini mnakimbilia London.
 
Waziri mkuu Pinda amefanya ziara isiyokuwa na miguu wala kichwa nchini Uingereza. Akiwa huko alipata habari za uwepo wa mkutano wa wanachadema uliongozwa na Wenje amabye ni mkurugenzi wa mambo ya nje wa CDM na Munishi ambaye ni katibu Mkuu wa BAVICHA.

Habari zilizovuja zinasema Pinda aliamua kumshinikiza Balozi wa Tanzania Uingereza kuitisha mkutano wa wana CCM kwa mgongo wa jina "WATANZANIA" siku ya Jumanne ya terehe 16/10/2012 ubalozini baada ya kusikia CHADEMA wamekutana ijumaa iliyopita na kuazimia kuisambaratisha CCM Uingereza.

Katika mkutano huu walijitokeza watu wasiozidi 15 na taarifa za ndani zinadai Pinda ametamka ndani ya kikao hicho kuwa CHADEMA ni "KIBOKO" kwani siku za nyuma walizoea kupata mapokezi makubwa yenye mbwembwe kama viongozi wa serikali lakini baada ya CDM kujikita nje kwa siku za hivi karibuni , hali hiyo imetoweka na kuwaduaza viongozi wa serikali.

Ikumbukwe wiki tatu zilizopita, makamu wa rais Gharibu Bilal alifanya ziara kama hiyo nchini Uingereza na kuambulia patupu.

Viongozi wa CDM walifanya mkutano wao tarehe 12/10/2012 jijini London na kukusanya idadi kubwa ya watu kutoka miji ya Reeding, Birmingham na London na baadhi ya watanzania waishio huko walijiunga na CDM.

Source: Mtanzania aliyekuwapo mkutanoni kwenye ubalozi wa Tanzania London.

Jamani tunapojaribu kuandika kitu humu tuwe tunaandika jambo ambalo unakuwa nalo uhakikika! Waziri mkuu hayuko UK kwa shughuli za kisiasa na wala hajafanya mkutano wa kisiasa! Hata kama tunaipinga CCM tusuzushe jambo ambalo halipo! Kama huna cha kupost humu kapost mada zindine sio lazima siasa! Siasa inahitaji ukweli sio kuandika tu bora umeandika.
 
Back
Top Bottom