CDM yamhenyesha Pinda uingereza

CDM yamhenyesha Pinda uingereza

Waziri mkuu Pinda amefanya ziara isiyokuwa na miguu wala kichwa nchini Uingereza. Akiwa huko alipata habari za uwepo wa mkutano wa wanachadema uliongozwa na Wenje amabye ni mkurugenzi wa mambo ya nje wa CDM na Munishi ambaye ni katibu Mkuu wa BAVICHA.

Habari zilizovuja zinasema Pinda aliamua kumshinikiza Balozi wa Tanzania Uingereza kuitisha mkutano wa wana CCM kwa mgongo wa jina "WATANZANIA" siku ya Jumanne ya terehe 16/10/2012 ubalozini baada ya kusikia CHADEMA wamekutana ijumaa iliyopita na kuazimia kuisambaratisha CCM Uingereza.

Katika mkutano huu walijitokeza watu wasiozidi 15 na taarifa za ndani zinadai Pinda ametamka ndani ya kikao hicho kuwa CHADEMA ni "KIBOKO" kwani siku za nyuma walizoea kupata mapokezi makubwa yenye mbwembwe kama viongozi wa serikali lakini baada ya CDM kujikita nje kwa siku za hivi karibuni , hali hiyo imetoweka na kuwaduaza viongozi wa serikali.

Ikumbukwe wiki tatu zilizopita, makamu wa rais Gharibu Bilal alifanya ziara kama hiyo nchini Uingereza na kuambulia patupu.

Viongozi wa CDM walifanya mkutano wao tarehe 12/10/2012 jijini London na kukusanya idadi kubwa ya watu kutoka miji ya Reeding, Birmingham na London na baadhi ya watanzania waishio huko walijiunga na CDM.

Source: Mtanzania aliyekuwapo mkutanoni kwenye ubalozi wa Tanzania London.

CDM inatwangwa kote kote.
 
Ukweli husemwa:

Wewe ndiyo umekurupuka bila kuisoma post yake vizuri. Amesema, Waziri Mkuu hayuko UK kwa shughuli za kisiasa na wala hajafanya mkutano wa kisiasa.

Na wewe inabidi ufikirie critically sometimes. The fact kuwa haukuwa mkutano wa kisiasa haina maana kuwa hakuzungumzia mambo ya kisiasa.

Katika kuhitimisha hotuba yake Mh. Pinda aliongelea hali ya kisiasa nchini. Kwa mfano, alizungumzia matukio mbalimbali ya hivi karibuni ya vurugu kama ya kuchoma makanisa mbagala, na visiwani Zanzibar, mauaji ya raia wakati wa maandamo Morogoro, Arusha na ya mwandishi wa habari David Mwangosi alieuwawa na polisi pamoja na mauaji ya kutisha ya RPC Barlow.

Hata hivyo, mleta mada kudai eti walikuwepo watu 15 tuu kwenye mkutano ni uongo mtupu. Propaganda za Chadema huko UK wabaki nazo huko huko.
 
Ukweli husemwa:

Watanzania bana.
Ndiyo maana nchi yetu imefika hapa ilipo. Wananchi Wengi ni waongo, wanasiasa ndiyo usiseme.

Tunakuwa wachakajuaji na waongo wa kupindukia. Kumbuka ukweli mara nyingi husimama pale penye uongo. Unaandika uongo ili kuwafurahisha watu humu JF. Ninaamini umeandika wakati moyo unakusuta na full of guilt conscience.

Mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye huo mkutano na watu naweza kusema walikuwa ni zaidi ya 50. Halafu naomba ujue UK siyo Tanzania. Watu wengi huku maisha ni kazi na kazi mara nyingi watu wengi wanamaliza kazi saa kumi na moja za jioni, halafu siku hiyo ilikuwa ni jumanne.

Tujaribu kuwa wakweli angalau hata kidogo.

Habari na makala yako imejaa maneno ya udaku.
 
ok.. ningesema hizi...Mh. Pinda alikutana na Watanzania waishio Uingereza na kuzungumzia mustakabali wa maendeleo ya nchi kisiasa, kiuchumi, n.k. It does not matter whether or not huo mkutano ulikuwa wa kisiasa. Kinacho-matter ni kwamba whether or not alizungumzia mambo ya kisiasa kwenye huo mkutano hata kama ulikuwa ni wa kidini.

Sikuzumgumza 'subjectively' intentionally lakini kwa kujibu yaliyoulizwa na scolari...

Tatizo ulikuwepo kwenye mkutano as an independent bystander. Otherwise, you could have break it down like this, regardless of whether or not unakubaliana na aliyosema. Next time don't just go and stand in meetings. At least do something.

Mh. Pinda aliongelea mambo ya kiuchumi, kisiasa, kiusalama, kimaendeleo, n.k. Baadhi ya mambo aliyoyaongelea:

  1. Hali halisi ya uchumi inaendelea kukua vizuri taratibu siku hadi siku tokea Rais Kikwete aingie madarakani
  2. Kukua kwa GDP kutoka asilimia 6.9% mpaka 7%.
  3. Kuongezeka kwa pato la wastani kwa mtanzania wa kawaida. Kwa sasa Mtanzania wa hali ya chini anaishi chini ya dolla moja ($1.00) kwa siku.
  4. Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 imedhamiria kuwa Tanzania iweze kunyanyuka na kuingia katika ngazi ya Kati au Middle Income Country ifikapo mnamo mwaka 2025.
  5. Mfumuko wa bei za vyakula imetokana na uuzwaji wa vyakula kwa nchi jirani.
  6. Tatizo la umeme bado ni sugu na linasababishwa na kupanda kwa gharama za mafuta ya uendeshwaji.
  7. Mapato ya ndani yanazidi nayo kuongezeka. TRA mwaka 2000 walikuwa wanakusanya bilion 64 kwa mwezi wakati sasa hivi makusanyo ni kiasi cha sh bilion 650 kwa mwezi.
  8. Tanzania imejipanga vizuri kuimarisha uchumi na maendelo kwa ujumla.
  9. Rais Kikwete amerejesha timu ya mipango inayosimamiwa Dr Mipango ambaye ndio mtendaji mkuu ili kuhakisha mipango yote inayopendekezwa ifanyike kama ilivyopangwa.
  10. Serikali imedhamiria kuongeza megawati wa umeme toka zilizopo sasa hivi ambazo ni megawati 600 mpaka megawati 2780 ndani ya miaka ijayo
  11. Bandari ya Dar inapanuliwa pia ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo umeshakamilika pesa na mkandarasi vimeshapatikani imebakia kuanza kazi.
  12. Kuwekuwa na wimbi kubwa la uwekezaji ambapo nchi nyingi za magharibi zinakimbilia kuja kuwekeza nchini hasa baada ya kugundulika kwa gesi, makaa ya mawe, dhahabu na Uranium nyingi.
  13. Kwa ujumla Tanzania bado ni kisiwa cha amani na utulivu kulinganisha na sehemu zingine.
  14. Alizungumzia matukio mbalimbali ya hivi karibuni ya vurugu kama ya kuchoma makanisa mbagala, na visiwani Zanzibar, mauaji ya raia wakati wa maandamo Morogoro, Arusha na ya mwandishi wa habari David Mwangosi alieuwawa na polisi pamoja na mauaji ya kutisha ya RPC Barlow Mwanza.
  15. Watanzania wasiogope kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo au kuwekeza zaidi nyumbani ili kuweza kujenga taifa letu.
 
Ukweli husemwa:

Watanzania bana.
Ndiyo maana nchi yetu imefika hapa ilipo. Wananchi Wengi ni waongo, wanasiasa ndiyo usiseme.

Tunakuwa wachakajuaji na waongo wa kupindukia. Kumbuka ukweli mara nyingi husimama pale penye uongo. Unaandika uongo ili kuwafurahisha watu humu JF. Ninaamini umeandika wakati moyo unakusuta na full of guilt conscience.

Mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye huo mkutano na watu naweza kusema walikuwa ni zaidi ya 50. Halafu naomba ujue UK siyo Tanzania. Watu wengi huku maisha ni kazi na kazi mara nyingi watu wengi wanamaliza kazi saa kumi na moja za jioni, halafu siku hiyo ilikuwa ni jumanne.

Tujaribu kuwa wakweli angalau hata kidogo.

Habari na makala yako imejaa maneno ya udaku.

Vi vema wewe umesema labda wataacha longolongo na chumvi chumvi....
 
Picha za michuzi inaonesha watu zaidi ya 50 walikuwepo wakimsikiliza
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ukweli husemwa:

Umekimbilia kujibu bandiko langu bila kujua mfurulizo wa kile nilichokuwa ninamjibu.

Jitahidi kwanza kujua mzizi wa maongezi mpaka yakafikia hapo na hiyo itakusaidia kunijibu ipasavyo.

Sijasema haukuwa mkutano wa kisiasa au la. in fact, kama sheria mama haijaweza kuainisha shughuli zipi niza kisiasa au la kwa viongozi serikalini, nitakacho weza kusema kiujumla kuwa Waziri mkuu ni mwanasiasa. siwezi kusema lolote zaidi kuhusiana na hilo.

Na wewe inabidi ufikirie critically sometimes. The fact kuwa haukuwa mkutano wa kisiasa haina maana kuwa hakuzungumzia mambo ya kisiasa.

Katika kuhitimisha hotuba yake Mh. Pinda aliongelea hali ya kisiasa nchini. Kwa mfano, alizungumzia matukio mbalimbali ya hivi karibuni ya vurugu kama ya kuchoma makanisa mbagala, na visiwani Zanzibar, mauaji ya raia wakati wa maandamo Morogoro, Arusha na ya mwandishi wa habari David Mwangosi alieuwawa na polisi pamoja na mauaji ya kutisha ya RPC Barlow.

Hata hivyo, mleta mada kudai eti walikuwepo watu 15 tuu kwenye mkutano ni uongo mtupu. Propaganda za Chadema huko UK wabaki nazo huko huko.
 
Ukweli husemwa:

Watanzania bana.
Ndiyo maana nchi yetu imefika hapa ilipo. Wananchi Wengi ni waongo, wanasiasa ndiyo usiseme.

Tunakuwa wachakajuaji na waongo wa kupindukia. Kumbuka ukweli mara nyingi husimama pale penye uongo. Unaandika uongo ili kuwafurahisha watu humu JF. Ninaamini umeandika wakati moyo unakusuta na full of guilt conscience.

Mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye huo mkutano na watu naweza kusema walikuwa ni zaidi ya 50. Halafu naomba ujue UK siyo Tanzania. Watu wengi huku maisha ni kazi na kazi mara nyingi watu wengi wanamaliza kazi saa kumi na moja za jioni, halafu siku hiyo ilikuwa ni jumanne.

Tujaribu kuwa wakweli angalau hata kidogo.

Habari na makala yako imejaa maneno ya udaku.

Kimsingi mleta mada ana kiwanda cha uongo. Kwa mfano anasema kuwa Mh. Pinda aliamua kumshinikiza Balozi wa Tanzania Uingereza kuitisha mkutano wa wana CCM kwa mgongo wa jina "WATANZANIA".

Ina maana hao wana CCM wasingekuja kama angeitisha mkutano wa Watanzania?

Ina maana wana CCM walingizwa mkenge kuwa utakuwa mkutano wa CCM kumbe ni Watanzania?

Hivi wana CCM UK siyo Watanzania eh?

Na Wana Chadema je?
 
Ukweli husemwa:

Hili ni tatizo la uongo kutaka kuufanya Uongo uwe ni ukweli. Kama unavyosema, maelezo yake yote hayana hata chembe ya Common sense.

Tatizo Watanzania wengi kwa sasa kila kitu ni siasa za kiitikadi. Tunakuwa na ndimi ndefu vitendo vifupi.

Kimsingi mleta mada ana kiwanda cha uongo. Kwa mfano anasema kuwa Mh. Pinda aliamua kumshinikiza Balozi wa Tanzania Uingereza kuitisha mkutano wa wana CCM kwa mgongo wa jina "WATANZANIA".

Ina maana hao wana CCM wasingekuja kama angeitisha mkutano wa Watanzania?

Ina maana wana CCM walingizwa mkenge kuwa utakuwa mkutano wa CCM kumbe ni Watanzania?

Hivi wana CCM UK siyo Watanzania eh?

Na Wana Chadema je?
 
Ukweli husema:

Inachukiza kuona watu wanaidanganya jamii ili kufurahisha mioyo yao bila sababu zozote.

Kwanza aliyeleta hili bandiko anaonekana wala hayupo hapa UK achilia mbali London. kwa nini huyu aliyempa hii habari ya kupika hakuibandika yeye mwenyewe hapa JF?

Vi vema wewe umesema labda wataacha longolongo na chumvi chumvi....
 
Hivi huyu Mzembe, kubwa jinga PM yupo kweli?

Maana mambo yanakwenda mrama kila siku halafu hatumuoni wala kumsikia.
 
haa jamani chadema wanachama matawi yake ni vijiwe vya mateja wauingereza nani ana muda na siasa za tz watu wamepinda wamepigika hawana hata pauni unawaletea siasa za nini mateja wanakuwa wamelewalewa hata hawapohawapo
 
Sidhani kama unajua unachoongea au upo kwenye majonzi baada ya Ponda kukamatwa! kwanza unafahamu UK yote acha England kuna watanzania wangapi jumla??Kama hujui nitakupatia statistics za Watanzania wote waliopo UK!

Utanipatia statistics wewe balozi wa Tanzania nchini Uingereza? Halafu kuhusu Uingereza kaa kimya kabisa Uingereza naijua kuliko wewe unavyoijua Moshi.

Vipi una viwanda vingapi vya uongo?
 
Utanipatia statistics wewe balozi wa Tanzania nchini Uingereza? Halafu kuhusu Uingereza kaa kimya kabisa Uingereza naijua kuliko wewe unavyoijua Moshi.

Vipi una viwanda vingapi vya uongo?
haha ha uingereza uijue wewe?? usiniache hoi! mm siwezi kuijua moshi sana maana huwa naenda tu kikazi au kwa matembezi! ila uingereza huwezi kunificha kitu, naifahamu maana nimesoma elimu yangu yote humo!!wewe kama waja na kuondoka sisi twaishi humu!
 
Utanipatia statistics wewe balozi wa Tanzania nchini Uingereza? Halafu kuhusu Uingereza kaa kimya kabisa Uingereza naijua kuliko wewe unavyoijua Moshi.

Vipi una viwanda vingapi vya uongo?
kwanza uingereza magaidi hawaruhusiwi!!
 
Chadema bana badala ya kujenga chama vijijini mnakimbilia London.

Wakati mwingine jaribu kufikiri kidogo, CDM wakienda vijijini mnataka kuwaua eti si wakati wa kampeni, leo wako nje ya nchi unasema waende vijijini. Lakini je umesahau kuwa kuna M4C?
 
Tunaipenda CCM sana, lakini siyo hii ya sasa hivi isiyothamini maadili ya Mwalimu.
 
Na wewe inakuhusu au kinakuuma nini ? Kama una ushauri si ungemshauri huyo Dhaifu mbona yeye hajengi chama chake vijijini ( na kuinua maisha bora kwa kila mtanzania), au sababu wamewashtukia na dili za kanga, ubwabwa na akina Mwigulu kuwaibia wake zao ?? Ofcok ameinua maisha bora kwa mafisadi including bingwa wa kuishi kimjini-jini aka mwenyekiti wa THT Riz1

Chadema bana badala ya kujenga chama vijijini mnakimbilia London.
 
Back
Top Bottom