CDF mstaafu Mabeyo kukutana na Papa Francis

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,445
8,300
Sijui Magufuli watu kama hawa aliwapataje. Ambapo kwa sasa kama vile hawapo.

===

Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini wapo Vatican kukutana na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo kama sehemu ya ratiba za kawaida za Maaskofu kukutana na Papa kila baada ya miaka michache.

Baadhi ya picha kutoka Vatican zinamuonesha Jen. Mabeyo akiwa na Maaskofu na nyingine ikimuonesha akisoma somo Katika mojawapo ya misa iliyofanyika huko. Hii inatoa tasiwra kuwa huenda akakutana na papa Francis siku za hivi karibuni.

Desemba 4, 2021 Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis alituma barua ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jen. Mabeyo kumshukuru kwa mchango wake mkubwa kwenye kanisa hilo.

Si ajabu Waislamu Huwa wanasema Kuna mfumo Katoliki.

Vipi na cdf wa Sasa ni WA kutokea huko huko?
Sasa waislamu wameingiaje hapa??

Kuna kipindi huwa ni busara kufyata mdomo wako ili kubakiza shaka ya kuwa aidha umuerevu ama mpumbavu kuliko kufungua mdomo na kuondosha shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Mabeyo aende kwa wakatoliki uje kutaja waislamu.
 
Mabeyo amelitumikia kanisa licha ya vyeo vyake serikalini

Amekuwa akijitoa kwa hali na mali

Pope francis alimpongeza mara kwa mara kwa majitoleo yake kwa kanisa kabla ya kustaafu utumishi wa umma na ameenda kufahamiana

Inasemekana Pope Francis alimuahidi Rais Magufuli kutembelea Tanzania,so sad magufuli hayupo
 
Mimi siamini Mungu na sina dini.

Lakini napenda uhuru wa watu kuamini wanavyotaka.

Huyo mtu hata angekuwa CDF wa sasa, ana uhuru wa kutimiza imani yake anavyotaka, hii ni haki ya kikatiba na ni sehemu ya "Universal Declaration of Human Rights" tangu December 10 1948.

Kwani kavunja sheria gani?

Mnaolalama mnajua kuwa hii ni haki ya kikatiba na hapo Vatican wanaenda hata marais waliopo madarakani? Kama wanavyokwenda kuhiji Maka na sehemu nyingine za kiimani kama Bagamoyo Mlingotini?
 
Misabato na milokole huwa inaiwaza kanisa katoliki muda wote
 
Back
Top Bottom