CCTV Camera yanasa tukio la kutisha la Ujambazi Salasala

Amalinze

JF-Expert Member
May 6, 2012
6,780
5,300
Hii sio movie. Ni tukio la kweli lililonaswa kwenye camera za CCTV maeneo ya Sala sala jijini Dar. Jamaa katoka bank kudraw Mil.15, kumbe kuna watu wanamfuatilia.

Akapanda pikipiki yake hadi nyumbani. Kumbe majambazi walishamtangulia kwa bodaboda. Ile anafika getini, Jamaa wakamtwanga risasi na kumuua na kuchukua begi lenye pesa. Wakamjeruhi na aliyekua anafungua geti kwa ndani.

Sikutegemea kama Tanzania tunaweza kufika kwny uhalifu wa kiwango hiki. Kutoa uhai wa mtu kisa Mil.15?? Hata kama angekua na "mabilioni" bado hakustahili kuuawa.

=====
Update
=====
Kwa waliokuwa wanadhani hili tukio ni Bongo Movie,Aliyeuawa ni Huyo Tarehe 7 January angalia na kwenye CCTV Camera utaona.

Lundo Post 7 Janu.jpg

=====
Update2
=====
Wadau Mnaweza Mkaangalia jengo liliotokea tukio Lenyewe kwa Mbele linavyoonekana,Hilo Jengo lipo Salasala,njia ya kwenda njia panda ya Kunduchi,Buyuni,Kwa pale Bahari inaonekana vizuri maana kule ni kilimani.Ukiangalia video vizuri kuna mtu alisema ni fremu kwa mbele kumbe ni trailer limepaki,Wadau naendelea kusisitiza hili tukio ni la kweli na Marehemu alishazikwa makaburi ya Kisiwani-Kigamboni.
SalaSala.jpg
 
Mbona haifunguki, ila point ni kwamba kwa nini alitembea na kiasi kikubwa hivyo cha pesa, yaliyompata mimi siwezi kumsikitikia sana
 
What a bad luck kwa marehemu ... Pole nyingi kwa ndugu, jamaa na marafiki, hope hazikutoka katika ile Bank inayotuhumiwa kuwa na utaratibu unaowapa majambazi kamwanya kakujua nani anachukua nini.

Nimejaribu kutafuta kosa la marehemu sijaliona, alijitahidi kuwa mwangalifu kwa kiasi kikubwa sana; alibeba begi na kuamua kutumia usafiri wa pikipiki ... shida ni hicho tu kiasi cha pesa, ni kikubwa sana na very tempt kwa watu wasio waaminifu.

NILICHOJIFUNZA: Kwa usalama wako, hakikisha hubebi fedha taslimu zaidi ya TZS 3 Milioni vinginevyo fanya TT, EFT ni rahisi na salama.
 
Watu husema kuwa tellers wanahusika...ila hebu tujiulize
1. Recordings zinaonyesha kuwa majambazi walitangulia nyumbani kwa "victim" dakika chache....swali....walijuaje anapoishi..
Je..hao tellers wanafahamu victim anapoishi??....kama jibu ni ndiyo.....walijuaje kuwa akichukua hizo pesa ataelekea nyumbani?
 
Tupia hiyo video vizuri haifunguki kiongozi # lakini je alishindwa kumpa askari sh. 20000/=amsindikize???
 
Watu husema kuwa tellers wanahusika...ila hebu tujiulize
1. Recordings zinaonyesha kuwa majambazi walitangulia nyumbani kwa "victim" dakika chache....swali....walijuaje anapoishi..
Je..hao tellers wanafahamu victim anapoishi??....kama jibu ni ndiyo.....walijuaje kuwa akichukua hizo pesa ataelekea nyumbani?
Kutoa kiasi hicho cha hela benki lazima utoe taarifa kwanza nahisi siku 1 au 2 kabla, so hapo ndo majambazi upata mchongo
 
Hii video mbona kama ya kufundishia????, yule jamaa aliyekuwa ndani ya geti kapigwa chuma halafu ananyanyuka tena kushangaa.

Yule mpita njia naye risasi zinapigwa hata hashtuki anaendelea na safari as if nothing.

Jambazi anaenda kwa mwenye pesa kupora na bunduki kama kabeba mfagio anaomba rifti.
 
Aisee kweli Mkuu inashangaza sana mpita njia hana wasiwasi yeye kabeba mzigo risasi zinalia yeye ndio kwanza anatembea,Majambazi wala hawana wasiwasi kabisa,cha kujifunza ni kwamba wananchi tuwe tunatoa taarifa tukiona watu si wakawaida wenye boda boda wakipark sehemu kihasara hasara.
 
wekeni hela benki zenye link na M-PESA, unadraw kuingia M-PESA na kama unajenga unanunua na kuwalipa mafundi kwa kudraw kiasi wanachotaka kwenye outlet zilizo karibu
Sisi wenye hela nyingi M-PESA haitoshi
 
Back
Top Bottom