Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imeeleza huzuni na masikitiko makubwa kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani, mauaji ya wananchi, na uharibifu wa mali yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Askofu Dkt. Stanley Hotay, Mwenyekiti wa CCT, amesema jumuiya hiyo imepokea taarifa mbalimbali kutoka kwa makanisa wanachama nchi nzima zikionesha athari kubwa kwa jamii kutokana na vurugu zilizojitokeza katika kipindi hicho.
“Taarifa hizo zimeonesha kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, mauaji ya wananchi, uharibifu wa mali na matukio yaliyosababisha maumivu kwa familia nyingi na jamii kwa ujumla. Hali hii imegusa moyo wa CCT na imeibua maombi na tafakari kubwa juu ya hali ya taifa letu,” amesema Askofu Hotay.