CCM: ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC mwaka 2014!!

CCM: ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC mwaka 2014!!

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Posts
2,782
Reaction score
877
Makamu ccm bara Vuai ALi Vuai ,amesema ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC na kwamba suala la mafuta na gas halitakua la muungano!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema Zanzibar itakuwa na nafasi ya kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), mara baada ya kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania mwaka 2014, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Msimamo huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, katika kongamano la siku moja la kumuenzi Rais wa Kwanza wa Zanzibar na muasisi wa Mapinduzi na Muungano, marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, lililofanyika katika chuo cha Afya Mbweni, mjini hapa.

Vuai alisema suala la kujiunga na OIC na mafuta na gesi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, isiwe sababu ya kuzorotesha au kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Vuai ambaye alikuwa akiwahutubia zaidi ya wajumbe 600 kutoka mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba, ambao ni wanachama wa umoja wa vijana UVCCM, alieleza kuwa mabadiliko ya Katiba yanayokuja yana neema kubwa kwa Zanzibar ikiwemo kufanyiwa marekebisho kwa sera ya mambo ya nje.

"Kuna mambo tumekubaliana ndani ya vikao vya juu vya chama yaondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano, kama suala la mafuta na gesi asilia, bandari, takwimu na uhusiano wa kimataifa ili Zanzibar iweze kuwa na nafasi ya kujiunga na OIC au umoja wa nchi za visiwa duniani," alisema Vuai.

Hata hivyo, Vuai alisema kama mafuta yatakuwa hayapo Zanzibar, wakati Tanzania Bara ikiwa tayari imeanza kufaidika na rasilimali hizo ikiwemo gesi, Zanzibar itakuwa imepoteza mchango mkubwa wa kiuchumi kupitia sekta hiyo kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kama yapo mafuta Zanzibar sawa, lakini kama hakuna tutakuwa tumeliwa wenzetu wameshaanza kuvuna" alisema Vuai huku akishangiliwa na vijana.

Kuhusu mchango wa Marehemu Karume, Vuai alisema kuwa umesaidia kuinua kiwango cha elimu kwa kupatikana bila ya malipo, kujenga umoja wa Wazanzibari, kudumisha misingi ya Muungano, kuwapatia makazi bora wananchi wake.

Alisema miongoni mwa faida za Muungano ni fursa zinazopatikana Tanzania Bara ambapo Wazanzibari wameweza kumiliki ardhi wakiwa raia wa Jamhuri ya Muungano, kupata matibabu sawa, pamoja na kunufaika na elimu ya juu, mbali na suala la ulinzi na usalama.

Hata hivyo aliwataka Wazanzibari kuwa makini na watu wanaotetea Muungano wa mkataba, kwa vile huwezi kuujadili Muungano wa mkataba bila ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
"Endapo mfumo wa Muungano ukibadilika, tutakuwa matatizo makubwa, ya kiuchumi, kijamii na kibiashara, sote tuna fursa sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano bila ya ubaguzi wowote," alisema Vuai.

Alisema bado kuna watu Zanzibar wana kiu ya kuongozwa na Sultan, kinyume na malengo ya Mapinduzi ya kutaka wananchi wajitawale wenyewe na kuwataka wananchi kuwa makini na wanaotumia siasa na dini kutaka kuvuruga amani na umoja wa kitaifa miongoni mwa watanzania.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UVCCM Martin Shigela alisema, watu wanaopandikiza chuki za kidini wana ajenda zao za siri ikiwemo kutaka kujipatia umaarufu kwa maslahi yao binafsi.

Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa makini na kujiepusha na siasa za jazba, na kutumiwa na watu wenye malengo binafsi ya kisiasa ya kutaka kuvuruga amani na umoja wa kitaifa, ikiwemo kuwagawa wananchi katika misingi ya kikanda, kama vile kudai rasilimali zinazopatikana katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
 
Makamu ccm bara Vuai ALi Vuai ,amesema ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC na kwamba suala la mafuta na gas halitakua la muungano!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwa hali ilivyo sasa haiwezekani kwani zanzibar siyo nchi bali ni mkoa kama dodoma au tabora.
 
Makamu ccm bara Vuai ALi Vuai ,amesema ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC na kwamba suala la mafuta na gas halitakua la muungano!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Makamu CCM bara,huyo ni makamu wa nini? icho cheo kipo CCM ipi?

Hata hivyo wajiunge tu kwani ni lazima watangaze tangaze au ndio wanaomba ruhusa?
 
Makamu ccm bara Vuai ALi Vuai ,amesema ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC na kwamba suala la mafuta na gas halitakua la muungano!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Haya Zenz na iwe nchi na si mkoa ili ijiamlie masuala yao. Muungano vunjia kule mbali.
 
Zanzibar ni Nchi?
Hii nayo sasa kama danganya toto
kila siku wanasema hayo hayo
Ngoja mgogoro wa Malawi uishe
maana ndiyo wenye tija sio
huko kwenye marashi ya karafuu.
 
Kama inchi ina haki ya kujiunga na OIC maana kule 99% ni waislam waacheni wajiunge kama Zenji
Apo utakapoona wazi kasoro za muungano
Muungano wa serikali mbili nilitaraji Tanganyika iwe nayo inchi ndani ya muungano ila ndo ivyo imefutiliwa mbali
Muungano wetu umekaa KIFUMBO FUMBO SANA
 
Sioni tatizo swala la gesi na mafuta kuondolewa kwenye muungano ila tuongeze na ardhi maana raia wa bara hawezi kupata ardhi zanzibar lakini wao wamekuwa wakinunua kwa wingi kwa hiyo tuweke sheria ardhi,mafuta na gesi yasiwe mambo ya muungano
 
[Umoja wa Nchi za Kiislamu

ZANZIBAR NI NCHI YA KIISLAM?

NA BARA JE?
 
Wazanzibari inafaa waache hisia zinazopindukia za kitaifa. Wajifikirie kwanza kama Watanzania. Suala la OIC ni sentimental kuliko la kiuchumi. Tanzania tayari inanufaika sana na misaada kutoka Uarabuni. Kuna benki ya kiarabu inatupa tu misaada tena mingi, kuna kuwait fund, saudia na kadhalika. Badala ya kutaka kutoa suala la mafuta na gesi kwenye muungano ingekua hekima kwa wazanzibari kudai madini mafuta na gesi viwe mambo ya muungano. Madini na gesi vipo tanzania bara wadai mgao.
 
Hoja zote za kujiunga na OIC huwa underlying motive ni kujitenga. Kujitenga ambako nako kunawezekana kuchochewa na sababu za kiuchumi na kijammii. Naamini Kuna mtu ameishawishi Zanzibar kuamini kuwa wanaweza kuwa Singapore ya Afrika, na kwamba Bara ndiyo kizuizi. Yaani kwamba Bara inawazuia kuishi maisha mazuri kutokana na kumiliki uchumi imara kama Singapore. Nimeweka Link ya Singapore uone kwamba hichi kipande kidogo sana cha ardhi watu wake wana kipato kikubwa sana, na Zanzibar inadhani haina Sababu ya kutokuwa hivyo.Singapore - Wikipedia, the free encyclopedia

Ni kweli kwamba Singapore pana uchumi imara. Lakini kwa Zanzibar kuwa kama Singapore, Wazanzibar watahitaji mila na desturi zao zibadilike na kuwa kama mila za Wachina. Wataweza? Kama wataendekeza Umwinyi watakuja kujuta walipokea dhana potofu. Bara wanapinga sana kujiunga na OIC. Naamini sababu nyingine ya Zanzibar kukaidi misimano ya Muungano ambayo inapinga kujiunga OIC ni ushauri wa nchi za Kiislam ambazo zinayo matamanio ya kupanua influence yao katika bara la Afrika.

Tuwaruhusu wajiunge na OIC, lakini pia tuwaruhusu wafanya hivyo nje ya Muungano. Hatuihitaji Zanzibar kwa lolote kwa kweli.

[ Singapore is the world's fourth leading financial centre, and its port is one of the five busiest ports in the world. The economy depends heavily on exports and refining imported goods, especially in manufacturing, which constituted 26% of Singapore's GDP in 2005. In terms of purchasing power parity, Singapore has the third highest per capita income in the world.]

Soko la Zanzibar kwa maana yoyote ile ya kibiashara lipo bara--yaani Tanganyika na zile nchi ambazo hazina bahari. Nje ya Muungano tunayo nafasi ya kuisumbua Zanzibar sana; hasa kama mafuta yaliyopo kwenye mkondo wa Rift Valley yakithibitika kuwapo ndani ya ardhi ya Tanganyika kama inavyohisiwa yapo. Wao watakuwa na mafuta yao, na sisi tutakuwa na mafuta yetu. Napata shida sana kuelewa kigezo cha kibri katika mioyo ya hawa watu. Tuwaruhusu.
 
Kama nawaona wajumbe walivyopiga makofi hapo kwenye point. Danganya toyo at its best. Mie nangojea flyovers hapa 2015 sijui tutaambiwa ndo wamemaliza kukusanya mawe?
Zanzibar ni Nchi?
Hii nayo sasa kama danganya toto
kila siku wanasema hayo hayo
Ngoja mgogoro wa Malawi uishe
maana ndiyo wenye tija sio
huko kwenye marashi ya karafuu.
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema Zanzibar itakuwa na nafasi ya kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), mara baada ya kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania mwaka 2014, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Msimamo huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, katika kongamano la siku moja la kumuenzi Rais wa Kwanza wa Zanzibar na muasisi wa Mapinduzi na Muungano, marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, lililofanyika katika chuo cha Afya Mbweni, mjini hapa.
Vuai alisema suala la kujiunga na OIC na mafuta na gesi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, isiwe sababu ya kuzorotesha au kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Vuai ambaye alikuwa akiwahutubia zaidi ya wajumbe 600 kutoka mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba, ambao ni wanachama wa umoja wa vijana UVCCM, alieleza kuwa mabadiliko ya Katiba yanayokuja yana neema kubwa kwa Zanzibar ikiwemo kufanyiwa marekebisho kwa sera ya mambo ya nje.
“Kuna mambo tumekubaliana ndani ya vikao vya juu vya chama yaondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano, kama suala la mafuta na gesi asilia, bandari, takwimu na uhusiano wa kimataifa ili Zanzibar iweze kuwa na nafasi ya kujiunga na OIC au umoja wa nchi za visiwa duniani,” alisema Vuai.
Hata hivyo, Vuai alisema kama mafuta yatakuwa hayapo Zanzibar, wakati Tanzania Bara ikiwa tayari imeanza kufaidika na rasilimali hizo ikiwemo gesi, Zanzibar itakuwa imepoteza mchango mkubwa wa kiuchumi kupitia sekta hiyo kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kama yapo mafuta Zanzibar sawa, lakini kama hakuna tutakuwa tumeliwa wenzetu wameshaanza kuvuna” alisema Vuai huku akishangiliwa na vijana.
Kuhusu mchango wa Marehemu Karume, Vuai alisema kuwa umesaidia kuinua kiwango cha elimu kwa kupatikana bila ya malipo, kujenga umoja wa Wazanzibari, kudumisha misingi ya Muungano, kuwapatia makazi bora wananchi wake.
Alisema miongoni mwa faida za Muungano ni fursa zinazopatikana Tanzania Bara ambapo Wazanzibari wameweza kumiliki ardhi wakiwa raia wa Jamhuri ya Muungano, kupata matibabu sawa, pamoja na kunufaika na elimu ya juu, mbali na suala la ulinzi na usalama.
Hata hivyo aliwataka Wazanzibari kuwa makini na watu wanaotetea Muungano wa mkataba, kwa vile huwezi kuujadili Muungano wa mkataba bila ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Endapo mfumo wa Muungano ukibadilika, tutakuwa matatizo makubwa, ya kiuchumi, kijamii na kibiashara, sote tuna fursa sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano bila ya ubaguzi wowote,” alisema Vuai.
Alisema bado kuna watu Zanzibar wana kiu ya kuongozwa na Sultan, kinyume na malengo ya Mapinduzi ya kutaka wananchi wajitawale wenyewe na kuwataka wananchi kuwa makini na wanaotumia siasa na dini kutaka kuvuruga amani na umoja wa kitaifa miongoni mwa watanzania.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UVCCM Martin Shigela alisema, watu wanaopandikiza chuki za kidini wana ajenda zao za siri ikiwemo kutaka kujipatia umaarufu kwa maslahi yao binafsi.
Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa makini na kujiepusha na siasa za jazba, na kutumiwa na watu wenye malengo binafsi ya kisiasa ya kutaka kuvuruga amani na umoja wa kitaifa, ikiwemo kuwagawa wananchi katika misingi ya kikanda, kama vile kudai rasilimali zinazopatikana katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

CHANZO: NIPASHE
 
Wanafikiri matatizo yao yatatatuliwa na jumuiya ya kiislam? Mjinga ndiye aliwae!
 
Who care about ZNZ?

Hata wakijiita Serikali ya WAislamu ZNz.It is fine.
Watanganyika tuulizwe kama tunataka Muungano ?

Enough is enough
 
Dah bora, maana kule kwao asilimia 99% ni waislam acha wajiunge watuache na Tanganyika yetu ambayo serikali yake haina dini ila wananchi wake wana dini. Wabara mnaotaka OIC & Mahakama ya Kadhi amieni Zanzibar mapema mkachukie vitambulisho vya Zanzibar mkazi!!!!
 
Back
Top Bottom