CCM: ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC mwaka 2014!!

CCM: ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC mwaka 2014!!

Quote: CCM: ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC mwaka 2014!!

=====

Nasema hivi..Mambo haya si ya kuamuliwa na Chama fulani tu kwa jinsi kinavyojisikia. No!

Lazima itambulike kuwa suala la Zanzibar kujiunga na OIC au jumuiya yeyote ya kidini au kimataifa haliko chini ya mamlaka ya CCM. Si Zanzibar kwa mamlaka yake wenyewe wala kuidhinishwa na CCM. Ni lazima Zanzibar ipate kibali cha serikali ya Jamhuri ya Muungano. Pia ni lazima kuwe na nguvu za msukumo wa kisheria kapitia katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano pamoja na baraka zote la Bunge la Muungano na si vinginevyo.

Huwa wakati mwingine hujiuliza kama huko Zanzibar kuna watu waliosoma na wenye weledi wa kutosha katika ufahamu wa mambo wa kuweza kuishauri serikali yao ki ufasaha wa kisheria. Au kuwa wanapenda kusikia tu ahadi za uwongo na matumaini hewa hata pale ambapo kisheria haiwezekani.
Ninaposikia kauli kama hizi inanifanya nikumbuke ule mjadala ulioletwa na mbunge mmoja wa Visiwani kule Bungeni pale alipodai ufafanuzi kuwa Zanzibar ni nchi au si nchi?🙂 na kujibiwa na Waziri Mkuu Mh Pinda kuwa 'SI Nchi'. Kwani katika uelewa wa kikawaida tu kwa mtu kama Mbunge hajuelewi kama Zanzibar ni nchi au si nchi basi unashangaa na kujiuliza kuwa alifikaje bungeni huyu? Na hata pale alipojibiwa katika tafsiri ya kisheria kuwa SI NCHI bado ikawa ni mambo ya munkari🙂 Lakini ni jibu sahihi mpaka leo hii kuwa "SI NCHI" na siku Muungano utakaponjika itarudi kuwa nchi. Na hali ni hiyo hiyo kwa Tanganyika. Sasa unashangaa gumu ni lipi hapo?

Na masuala kama haya yananifanya pia nikumbe ile kesi ya uhaini kule Zanzibar ambapo hukumu ile ya Supreme Court ilibainisha juu ya jambo hili kuwa Zanzibar si nchi (Kwa mantiki ya kuwa Sio Sovereignty) na wala Rais wa Zanzibar haiwezi kupinduliwa kwani yeye sio Amiri Jeshi Mkuu (Commander in Chief).

Hivyo kauli kama hii iwapo imetolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Chama cha CCM Ni kauli yenye nia ya 'kupika mgogoro' kwa kuwajaza watu Zanzibar hamasa na matuini hewa ili hali ni ahadi isiyoweza kutekelezeka kisheria.
 
Je, inawezekanaje Zanzibar ikatambulika kimataifa halafu wakati huo huo zanzibar ikawa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika? Sijaelewa!!!
 
Kila heli wazanzibar hata mkiitaka na nchi yenu chukueni.
Mdhulumiwa mno na mwl jk muasisi wa muungano huu haramu hata karume alivyoshtukia uharamu wa muungano kabla hajanyanyua mdomo nyerere akamuua.
Haki ya na heshima ya mtu haipotei hata siku moja mungu atakusimamieni na mtaipata haki yenu na wale waliouliwa kidhuluma tunaamini watapata haki yao mbele ya muumba wa mbingu na nchi mwenye sifa ya kutodhulumu.
 
Hakuna danganya toto tena, Hizo kasoro zitakuja automatically kujirekebisha wenyewe Zanzibar ikishapata mamlaka yake., Vuai Zanzibar siyo yako peke yako, Zanzibar ina watu wake (wananchi wote wa zanzibar) vikao vya dodoma haviwezi kuwaamulia waznzibari mambo yao, Muhimu Warioba aheshimu maoni ya wazanzibari asilimia 66.2% wanataka Muungano wa Mkataba, Zanzibar kuwa na mamlaka yake ni lazima otherwise kura ya maoni jibu litakuwa NOOO., Hizo kasoro muda woote CUF wamekuwa wakisema na katika maoni pia nyinyi mulikuwa munapinga bado munasema zanzibar inafaidika sasa munatia vidole puani., Zanzibar bila ya Mamlaka yake hakitaeleweka
 
Je, inawezekanaje Zanzibar ikatambulika kimataifa halafu wakati huo huo zanzibar ikawa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika? Sijaelewa!!!

Kaka Zanzibar siyo sehemu tena ya Jamuhuri ya Muungano, Zanzibar ni nchi, Zanzibar lazima itakuwa na mamlaka yake kama nchi zote duniani, Kama ni Muungano utakuwa ni wa Mkataba otherwise Katiba yenu mpya kwa Zanzibar jibu litakuwa NOO kwenye kura ya Maoni.,
 
Mbona dodoma na Tabora haina rais wala bunge lake?

Kaka Zanzibar Imepata uhuru wake 1964 kutoka kwa mkoloni baadae Nyerere akamtumilia hadaa Karume kutaka nchi hizi mbili ziungane na ndivyo ilivyokuwa baada ya hapo Karume akagundua uhuni wa Nyerere kwa kutaka kuimeza Zanzibar na Karume kutaka kujitoa kwenye Muungano wakampiga risasi wakamuua,

Sasa Dodoma na Tabora ilipata uhuru wake LINI? mbona nyi Watanganyika akili zenu zimechanganyika na mafuta ya Taa?
 
Nyerere ndie mtu pekee alomtia fitna na kumrubuni kwa ulaghai muuaji wa karume, ndie aliyepanga mikakati hiyo na akiitaka pia aifanye nchi ya uganda kwa kutilia fitna iddy amini, hasidi huyu nyerere mungu amlipe huko aliko na moto unaomuwakia. Amin
 
Vikao vya ccm wakikuabaliana ndiyo inakuwa sera ya taifa?

Mafuta na gas halitakuw suala la muungano. Ila kama hawatakuwa na mafuta eti watakosa faida. Hawa watu wamezoea kupata faida bure kwa mgongo wa wa Tanzania. Faida tugawane, ila tatizo likitokea, hawataki muungano. Uone jinsi hata hawana hata hisia.

Ina maana kwamba katiba mpya itadeclare kwamba Zanzibar ni nchi? Kwa hiyo itakuwa ni nchi ya kiislam? Muungano utakuwa na muundo wa serikali ngapi?

CCM MNAJIKOROGA KWELI KWELI.
 
Asilimia 95% ya wazanzibari ni waislam kwa hiyo hii article uliyoiweka hapa haleti mabadilko yoyote kwa nchi kazi zanzibar
Kwahiyo Mkuu unadhani hao 5% wa dini zingine Zanzibar hawana haki ya kushika nyadhifa zozote za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwasababu ya dini zao tu? Ingekuwa hiyo 5% ni waislamu wangejisikiaje kwangetengwa kwa kila nyanja? Kama lengo kuu la OIC/IAO ni kuwafanya waafrika wote waislam je unafurahia njia wanazotumia kufikia adhma yao?Kwa dhati kabisa, napinga mpango wa watu au dini yoyote kuwalazimisha wengine waingie katika imani wasiyoitaka kwa kutumia hata mauaji. Kama Mungu amewaachia hata mashoga waishi hadi siku ya hukumu, mtu ni nani hata ashike upanga ili watu waamini?Leo hii wakristo wanatendwa vibaya unguja na tumeambiwa na kiongozi wa serikali kuwa ni kazi ya Mungu. Wangeuawa wao wangedai hivyo? Huu ni mpango wa shetani na majeshi yake kuudhoofisha ukristo na kamwe hautafanikiwa kwani KristoYesu ndiye Mfalme mkuu na Bwana wa mabwana.
 
kaka ukweli wenyewe mimi binafsi si mereketwa wa dini yoyoote,dini ni imani binafsi ya mtu,mnaweza kuwa mnatoka famila moja lakini kila mtu na dini yake,kwa upande wangu dini ni moja katika njia za kuwa-control binadamu,Mimi sijaiweka hii mada kidini kwasababu sipendi udini,Kama mtanzani nafikiri zaidi maendeleo ya nchi,muona wangu Kama nchi itajiunga na organization yoyote ile inayosaidia jamii iwe ya kikiristo,Agha kan,ya kiisalmu ,ya kihindi nk,acha nchi ijiunge kwani kwani hiyo misaada itawasaidia watu wote haito chagua dini ya mtu

Nimeandika hayo niliyo andika kwasababu hii article inaeleza kuwa OIC inataka kuigeuza Africa iwe na dini ya kiislam,kitu ambacho hakiwezekani,kuwambia wazanzibari kuwa wasijiunge na OIC kwasababu OIC ina sera ya siri ya kuifanya Afrika iwe na dini ya kiislamu ni kichekesho kwasababu asilimia 95% ya wazanzibari ni waislamu kwao wao haitakuwa tishio bali

Hamna mkristo hata mmoja alietendwa vibaya zanzibar ukweli wenyewe wakristo wameongezeka zanziabr,makanisa yameongezeka zanzibar kama wakristo wanatendwa vibaya zanzibar ingelikuwa kunyume chake,Binafsi naona hayo mambo yanayotokea zanzibar ni ya kisiasa zaidi sio ya kidini
 
Nimefurahi kuwa wewe si mkereketwa wa dini yoyote. Watu wa dini yoyote kupata msaada kutoka kwa yoyote si hoja kama tu msaada huo HAUTAKUWA kwa sharti la kumuathiri mwingine ambaye si muhusika mkuu au hajaridhia. Kweli si tisho kwa wazanzibari 95% lakini yaweza kuwa tishio kwa wale 5% kama masharti ya uanachama nikuwanyima haki na uhuru hao5% Hata kama wahafidhina wa dini ni wachache lakini wanapoachiwa kufanya wapendavyo basi hata wale wasio na dini au ukereketwa wanaweza kuathirika kwa uhafidhina huo. Si kweli kuwa ni matukio ya kisiasa kwani katika zama hizi, ni siasa gani zimefanyika kwa kuchoma makanisa, kudhuru wakristo, kuwalazimisha kufuata kanuni na maadili ya kiislamu kama vile kutokula /kutouza chakula mchana wakati wa ramadhani? Unadhani mwislam mmoja akitembelea Vatican itakuwa ni sawa kulazimishwa kuinama akimwona papa au kula nguruwe kwa kuwa 99.99% ni waroma katoliki?Lengo langu si kujenga hoja ya kubaguana kidini au vyovyote vile isipokuwa kulinda haki na uhuru wa wote kuishi kwa mujibu wa sheria za nchi. Tatizo haliondoki kwa kusema halipo au kwa kuliita dogo bali kwa kulikabili kwa dhati kama walivyofanya wazee wetu Nyerere na Mwinyi zama zao. Ni nchi yetu sote, tupendane na kulindana si kuwindana na kutendana.
 
Hivi nifamilia gan hii baba hana dini halaf mama anadini? cbora waachane2! wagawane watoto kila mmoja alee kwa itikad zake!!!
 
Kiini cha haya ni kuwa mkoloni mweusi anatapa hana pa kushika,jamhuri ya watu wa zanzibar kwanza.
 
Makamu ccm bara Vuai ALi Vuai ,amesema ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC na kwamba suala la mafuta na gas halitakua la muungano!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema Zanzibar itakuwa na nafasi ya kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), mara baada ya kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania mwaka 2014, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Msimamo huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, katika kongamano la siku moja la kumuenzi Rais wa Kwanza wa Zanzibar na muasisi wa Mapinduzi na Muungano, marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, lililofanyika katika chuo cha Afya Mbweni, mjini hapa.

Vuai alisema suala la kujiunga na OIC na mafuta na gesi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, isiwe sababu ya kuzorotesha au kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Vuai ambaye alikuwa akiwahutubia zaidi ya wajumbe 600 kutoka mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba, ambao ni wanachama wa umoja wa vijana UVCCM, alieleza kuwa mabadiliko ya Katiba yanayokuja yana neema kubwa kwa Zanzibar ikiwemo kufanyiwa marekebisho kwa sera ya mambo ya nje.

“Kuna mambo tumekubaliana ndani ya vikao vya juu vya chama yaondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano, kama suala la mafuta na gesi asilia, bandari, takwimu na uhusiano wa kimataifa ili Zanzibar iweze kuwa na nafasi ya kujiunga na OIC au umoja wa nchi za visiwa duniani,” alisema Vuai.

Hata hivyo, Vuai alisema kama mafuta yatakuwa hayapo Zanzibar, wakati Tanzania Bara ikiwa tayari imeanza kufaidika na rasilimali hizo ikiwemo gesi, Zanzibar itakuwa imepoteza mchango mkubwa wa kiuchumi kupitia sekta hiyo kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kama yapo mafuta Zanzibar sawa, lakini kama hakuna tutakuwa tumeliwa wenzetu wameshaanza kuvuna” alisema Vuai huku akishangiliwa na vijana.

Kuhusu mchango wa Marehemu Karume, Vuai alisema kuwa umesaidia kuinua kiwango cha elimu kwa kupatikana bila ya malipo, kujenga umoja wa Wazanzibari, kudumisha misingi ya Muungano, kuwapatia makazi bora wananchi wake.

Alisema miongoni mwa faida za Muungano ni fursa zinazopatikana Tanzania Bara ambapo Wazanzibari wameweza kumiliki ardhi wakiwa raia wa Jamhuri ya Muungano, kupata matibabu sawa, pamoja na kunufaika na elimu ya juu, mbali na suala la ulinzi na usalama.

Hata hivyo aliwataka Wazanzibari kuwa makini na watu wanaotetea Muungano wa mkataba, kwa vile huwezi kuujadili Muungano wa mkataba bila ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Endapo mfumo wa Muungano ukibadilika, tutakuwa matatizo makubwa, ya kiuchumi, kijamii na kibiashara, sote tuna fursa sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano bila ya ubaguzi wowote,” alisema Vuai.

Alisema bado kuna watu Zanzibar wana kiu ya kuongozwa na Sultan, kinyume na malengo ya Mapinduzi ya kutaka wananchi wajitawale wenyewe na kuwataka wananchi kuwa makini na wanaotumia siasa na dini kutaka kuvuruga amani na umoja wa kitaifa miongoni mwa watanzania.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UVCCM Martin Shigela alisema, watu wanaopandikiza chuki za kidini wana ajenda zao za siri ikiwemo kutaka kujipatia umaarufu kwa maslahi yao binafsi.

Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa makini na kujiepusha na siasa za jazba, na kutumiwa na watu wenye malengo binafsi ya kisiasa ya kutaka kuvuruga amani na umoja wa kitaifa, ikiwemo kuwagawa wananchi katika misingi ya kikanda, kama vile kudai rasilimali zinazopatikana katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
Sawa umesikika mkubwa.
 
Hili koloni letu la zanzibar limeshaanza chokochoko!!!!!!!!!!
 
Hapa kama ukoloni basi ni wa Zanzibar kuitawala Tanganyika kwa vigezo hivi; (1) wanashiriki kutunga sharia za kuitawala kwenye bunge linaloitwa la muungano lakini sharia hizo hazina nguvu huko hadi baraza la wawakirishi na rais wa serikali ya mapinduzi wapitishe(ndivyo ilivyo tangu azimio la Arusha ambalo halikufika huko.) (2) wana sehemu ya ardhi wanayoimiliki upande wa Tanganyika ilhali baadhi ya wakazi wa Bagamoyo hawana ardhi ya kutumia, Tanganyioka haihodhi hata mchanga wa popote pale.Wao wanashika hata wizara zisizo za Muungano(kama waziri wa afya) wakati watanganyika hawawezi kufanya hivyo kwao. (3) Wakati Tanganyika imepoteza alama na hadhi zake zote za utaifa (Hata jina lake limefutwa kisheria Zanzibar inazo zote na raois wake tunamfanamu na anapigiwa mizinga 21 kama maraisi wengine(anayemjua rais wa Tanganyika au msemaji wao popote pale na yeyote yule anijulishe). Wao wano huhuru wa kuishi popote Tanganyika na kujihushisha na shughuli halali na maisha, Mtanganyika yoyote hawezi kutambuliwa Zanzibar hadi aishi miaka kadhaa(kuna raia wa Zanzibar na wana vitambulisho lakini hakuna raia wa Tanganyika) (4) wanamipango yao ya uchumi na maendeleo lakini fedha za uchumi na maendeleo zitokanazo na Tanganyika zinatumika kwa mabo ya muungano , badala ya kuchangiwa, mfano ni ununuzi wa rada ambao hapa chengi yake ya ufsadi iliporudishwa wakataka wapewe mgao. Tusubiri katiba mpya labda itakuwa na mambo mapya. Kwa sasa kuna kero nyingi za muungano ambazo watanganyika wanawakilishwa na viogozi wa muungano ilhali wenzetu wanawakilishwa na viongozi wao. Muungano ni mzuri isipokuwa watu waache chokochoko na pamoja tutafuta suluhisho la ama serikali moja( Naunga mkono) au serikali tatu ( mawaunga mkono wanaopendelea lakini siungi mkono mfumo wa sasa wsa serikali mbili wenye utata nilioeleza hapo juu.
 
Nimefurahi kuwa wewe si mkereketwa wa dini yoyote. Watu wa dini yoyote kupata msaada kutoka kwa yoyote si hoja kama tu msaada huo HAUTAKUWA kwa sharti la kumuathiri mwingine ambaye si muhusika mkuu au hajaridhia. Kweli si tisho kwa wazanzibari 95% lakini yaweza kuwa tishio kwa wale 5% kama masharti ya uanachama nikuwanyima haki na uhuru hao5% Hata kama wahafidhina wa dini ni wachache lakini wanapoachiwa kufanya wapendavyo basi hata wale wasio na dini au ukereketwa wanaweza kuathirika kwa uhafidhina huo. Si kweli kuwa ni matukio ya kisiasa kwani katika zama hizi, ni siasa gani zimefanyika kwa kuchoma makanisa, kudhuru wakristo, kuwalazimisha kufuata kanuni na maadili ya kiislamu kama vile kutokula /kutouza chakula mchana wakati wa ramadhani? Unadhani mwislam mmoja akitembelea Vatican itakuwa ni sawa kulazimishwa kuinama akimwona papa au kula nguruwe kwa kuwa 99.99% ni waroma katoliki?Lengo langu si kujenga hoja ya kubaguana kidini au vyovyote vile isipokuwa kulinda haki na uhuru wa wote kuishi kwa mujibu wa sheria za nchi. Tatizo haliondoki kwa kusema halipo au kwa kuliita dogo bali kwa kulikabili kwa dhati kama walivyofanya wazee wetu Nyerere na Mwinyi zama zao. Ni nchi yetu sote, tupendane na kulindana si kuwindana na kutendana.

OIC haina masharti kwenye kutoa misada ya jamii kuna nchi ambazo watu wake ni asilimia mia moja 100% wakristo mfano Rusia,Msumbiji nk na ni wanachama wa OIC.ni mawazo wa ya watanzania wachache wenye ubaguzi wa kidini ndio wnafikiria kuwa OIC ni taasisi ya dini,

Waulize wanasiasa wa Zanzibar kuhusu siasa zao mpaka wemefanya wananchi kuchoma makanisa, mambo ambayo hayajawahi kutokea Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Kuhusu mwezi Ramadhani ikifika mwezi wa Ramadhani mtu mwenye dini isiyokuwa ya kiislam au mwislam ambae hajafunga hakatazwi kula ila anakatazwa kula hadharani hiyo sheria ipo Zanzibar kabla hata hatujaungana zanzibar na Tanganyika, ni kuweka heshima kwa wale waliofunga "Religion tolerance",
 
Quote: CCM: ZNZ ipo tayari kujiunga na OIC mwaka 2014!!

=====

Nasema hivi..Mambo haya si ya kuamuliwa na Chama fulani tu kwa jinsi kinavyojisikia. No!

Lazima itambulike kuwa suala la Zanzibar kujiunga na OIC au jumuiya yeyote ya kidini au kimataifa haliko chini ya mamlaka ya CCM. Si Zanzibar kwa mamlaka yake wenyewe wala kuidhinishwa na CCM. Ni lazima Zanzibar ipate kibali cha serikali ya Jamhuri ya Muungano. Pia ni lazima kuwe na nguvu za msukumo wa kisheria kapitia katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano pamoja na baraka zote la Bunge la Muungano na si vinginevyo.

Huwa wakati mwingine hujiuliza kama huko Zanzibar kuna watu waliosoma na wenye weledi wa kutosha katika ufahamu wa mambo wa kuweza kuishauri serikali yao ki ufasaha wa kisheria. Au kuwa wanapenda kusikia tu ahadi za uwongo na matumaini hewa hata pale ambapo kisheria haiwezekani.
Ninaposikia kauli kama hizi inanifanya nikumbuke ule mjadala ulioletwa na mbunge mmoja wa Visiwani kule Bungeni pale alipodai ufafanuzi kuwa Zanzibar ni nchi au si nchi?🙂 na kujibiwa na Waziri Mkuu Mh Pinda kuwa 'SI Nchi'. Kwani katika uelewa wa kikawaida tu kwa mtu kama Mbunge hajuelewi kama Zanzibar ni nchi au si nchi basi unashangaa na kujiuliza kuwa alifikaje bungeni huyu? Na hata pale alipojibiwa katika tafsiri ya kisheria kuwa SI NCHI bado ikawa ni mambo ya munkari🙂 Lakini ni jibu sahihi mpaka leo hii kuwa "SI NCHI" na siku Muungano utakaponjika itarudi kuwa nchi. Na hali ni hiyo hiyo kwa Tanganyika. Sasa unashangaa gumu ni lipi hapo?

Na masuala kama haya yananifanya pia nikumbe ile kesi ya uhaini kule Zanzibar ambapo hukumu ile ya Supreme Court ilibainisha juu ya jambo hili kuwa Zanzibar si nchi (Kwa mantiki ya kuwa Sio Sovereignty) na wala Rais wa Zanzibar haiwezi kupinduliwa kwani yeye sio Amiri Jeshi Mkuu (Commander in Chief).

Hivyo kauli kama hii iwapo imetolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Chama cha CCM Ni kauli yenye nia ya 'kupika mgogoro' kwa kuwajaza watu Zanzibar hamasa na matuini hewa ili hali ni ahadi isiyoweza kutekelezeka kisheria.

Mi mwenyew napatwa a wasiwasi, znz sijui km wanaelim kweli, lkn huyo alieesema hivy nikada wa CCM so kwaana hiyo CCM hawana elimu nasio wazanzibar napia makamo wa raisi hana elim yakutosha au siyake.
 
Back
Top Bottom