CCM Zanzibar: Hatutaunda tena Serikali ya Kitaifa Zanzibar

Huyo naye kachemka vibaya sana, yani kwa hiyo hali ilivyochafuka huko kwa support ya UKaWA bado anategemea watashinda uchaguzi wa October?

Wataunda Serikali ya mseto ipi ilhali watakuwa washatupwa nje?
 
2015 CCm kitakuwa ni chama cha upinzani,

Bora wameanza kulijua hilo mapema kwa sasabu chama tawala CUF na UKAWA havitokubali kuwashirikisha CCM katika serikali zao.

Huyo mwenezi safi sana kauona na kausoma upepo.

Ameabza kujiandaa kisaikolojia kuwa chama pinzani

Ulikuwa kichwani mwangu mkuu.
 
MwanaDiwani msaka tonge na wewe umelishadidia hili? Kweli njaa mbaya sana! Nina mashaka na utimamu wako wa akili ndio maana unakubali kutumika kama msukule kwa ajili ya CCM, mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya hivi

Wacha CCM wakutumie kama condom ukimalisha shida watakutupa kama walivyowatupa wengine

Serikali ya Umoja wa Kitaifa haiwezi kuvunjwa na Waride Bakari Jabu wala CCM yoyote naomba uelewe hilo
 
huyu dada yuko usingizini,ana weweseka tu ,she doesnt know what time it is,ccm haina uwezo wa kuamua kutokuunda serikali ya umoja wa kitaifa,sababu wao sio waloiweka madarakani, hajui anaongea nini yupo kwenye ndoto za miaka ilee ya zamani wakati ccm ilipokua na rungu la maamuzi yote.

ni wananchi ndio waloiweka na ni wao tu wanaweza kuiondoa,na wanachi wa ccm kwa zanzibar labda wamebakia 15% tu,kwa hio ccm kuweza kuvunja suk chance ya ni hio 15% ni ndotoni tu
 
sasa mlitaka muundeje serikali ya umoja wa kitaifa wakat hamtashinda?
 
Ni matakwa ya Katiba sasa sijui imebadilishwa lini?! Huu ulevi wa wanasiasa wajinga wa Unguja utaisha lini?

Umeiona eh!Maana nilidhani siye Mabush lawyers tu ndiyo hatujui Katiba za Nchi yetu,kumbe hata wale wanaoipitisha pia hawajui walichopitisha na hivyo anajikuta kwa mongezi yake anataka kuivunja...............Basi ukisikia ngoma inavuma sana karibia itapasuka.............Wazanzibar hilo lenu..................
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.

Waride alisema makubaliano yanayotokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa yameanza kuvurugwa na kukiukwa kidogo kidogo katika misingi yake mikuu huku kauli za chuki na uhasama zikitawala.

Alikumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba sababu za kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni tofauti za kisiasa na kauli za chuki ambazo zilisababisha kuwepo kwa malumbano ya kisiasa katika majukwaa ya kisiasa.

Alisema kwa bahati mbaya, misingi hiyo sasa imeanza kuyumba na kuporomoka kidogo huku matusi na kejeli kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, zikichukua nafasi kubwa.

"Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na kauli za chuki na uhasama, zinazotolewa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ambazo zinaashiria kuyumba kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kurudisha chuki na uhasama," alisema.

Waride alifafanua kwamba CCM ambayo ni mshirika anayeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatamka bayana kwamba haipo tayari kushiriki kuunda serikali hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alifahamisha CCM haikuwa na sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu ilipata ushindi wa kutosha, uliowafanya kuunda serikali. Hata hivyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria.

"CCM haioni sababu tena ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu wenzetu CUF wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uhasama zinazorudisha nyuma matarajio ya wananchi wa kuwepo maridhiano ya kisiasa," alisema.
========================

Chanzo: Habari leo
Nani kakwambia CCM mwaka huu itakamata dola?!! hilo sahau mkuu. Hakuna marefu yasiyo na ncha na arobaini yenu imetimia R I H CCM
 
Tatizo linaonaekana huyu mama hajui kuwa serikali ya umoja wa kitaifa ipo kwa mujibu wa katiba na wala sio kwa hisani ya CCM,kama hawaitaki ni kurudi kwa wananchi ihitishwe kura ya maoni kwa maandalizi kuanzia ndani ya baraza la wawakilishi,wananchi waamue kama bado wanaitaka au awaitaki,je CCM wana ubavu huo??
 
MwanaDiwani huwa sometimes nakulaumu sana kuleta habari bila kuzichuja kwanza ww mwenyewe!

Serikali ya Muungano ya ZNZ ipo kisheria,kuivunja unapaswa ipigwe kura ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa ushindi wa 2/3!Sasa huyu Mama muimba chakacha yy hayajui haya?

Kwa kadhia hii ya KATIBA ya Chenge KUINYIMA ZNZ uhuru wake wa maamuzi ni kabuli la CCM huko visiwani na anayedhani CCM itapata hadi 2/3 ya viti BARAZANI ili wawe huru kubadili katiba na kuvunja Serikali hii ya meto AKAPIMWE AKILI
 
Last edited by a moderator:

Sasa unataka Nape afanye kazi gani wakati ndio kibaqua chake kinachomuweka mjini?
 
Last edited by a moderator:
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.

Waride alisema makubaliano yanayotokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa yameanza kuvurugwa na kukiukwa kidogo kidogo katika misingi yake mikuu huku kauli za chuki na uhasama zikitawala.

Alikumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba sababu za kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni tofauti za kisiasa na kauli za chuki ambazo zilisababisha kuwepo kwa malumbano ya kisiasa katika majukwaa ya kisiasa.

Alisema kwa bahati mbaya, misingi hiyo sasa imeanza kuyumba na kuporomoka kidogo huku matusi na kejeli kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, zikichukua nafasi kubwa.

“Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na kauli za chuki na uhasama, zinazotolewa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ambazo zinaashiria kuyumba kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kurudisha chuki na uhasama,” alisema.

Waride alifafanua kwamba CCM ambayo ni mshirika anayeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatamka bayana kwamba haipo tayari kushiriki kuunda serikali hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alifahamisha CCM haikuwa na sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu ilipata ushindi wa kutosha, uliowafanya kuunda serikali. Hata hivyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria.

“CCM haioni sababu tena ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu wenzetu CUF wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uhasama zinazorudisha nyuma matarajio ya wananchi wa kuwepo maridhiano ya kisiasa,” alisema.
========================

Chanzo: Habari leo

Hajielewi huyu.
 
Huyo naye kachemka vibaya sana, yani kwa hiyo hali ilivyochafuka huko kwa support ya UKaWA bado anategemea watashinda uchaguzi wa October?

Wataunda Serikali ya mseto ipi ilhali watakuwa washatupwa nje?

Huyu akili hazimtoshi,kwani mlilazimishwa kujiunga na umoja wa kitaifa?au hali ilivyokuwa ndio iliwalazimu kufanya hivyo?hata hivyo ccm zanzibar msijidanganye kuwa mtashinda uchaguzi mkuu.hizo ni ndoto za Alinacha.CUF NDIO MPANGO MZIMA.SHIKAMOO MAALIM SEIF UTAPITA URAISI KIULAINI SANA.HAYA MAFISADI YAMETUCHOSHA
 
Mpaka kuvunjika SUK kuna hatua nyingi zipite ndio iweze kuvunjika

1) Baraza la Mapinduzi, huko ipatikane thuluthi mbili, na hakuna anayeweza kuifikia (Sio CUF wala CCM

2) Baraza la Wawalilishi mchakato wake ni kama BLM

3) Referendum ya wananchi, pia inahitaji ipate 66% watakaoikataa

Sasa huyu MwanaDiwani anapokuja na habari kama hizi na kuzishabikia sijui anakua na akili gani Wallahi? Ndio nikasema huyu anatumika kama condom, kuishabikia CCM ni lazima uwe mwendawazimu

Na hao waandishi wa habari makanjanja wanaoandika habari hizi sijui upeo wao unakuaje juu ya kufuatilia mambo mpaka wanakubali kuziandika habari kama hizi
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.

Waride alisema makubaliano yanayotokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa yameanza kuvurugwa na kukiukwa kidogo kidogo katika misingi yake mikuu huku kauli za chuki na uhasama zikitawala.

Alikumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba sababu za kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni tofauti za kisiasa na kauli za chuki ambazo zilisababisha kuwepo kwa malumbano ya kisiasa katika majukwaa ya kisiasa.

Alisema kwa bahati mbaya, misingi hiyo sasa imeanza kuyumba na kuporomoka kidogo huku matusi na kejeli kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, zikichukua nafasi kubwa.

“Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na kauli za chuki na uhasama, zinazotolewa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ambazo zinaashiria kuyumba kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kurudisha chuki na uhasama,” alisema.

Waride alifafanua kwamba CCM ambayo ni mshirika anayeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatamka bayana kwamba haipo tayari kushiriki kuunda serikali hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alifahamisha CCM haikuwa na sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu ilipata ushindi wa kutosha, uliowafanya kuunda serikali. Hata hivyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria.

“CCM haioni sababu tena ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu wenzetu CUF wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uhasama zinazorudisha nyuma matarajio ya wananchi wa kuwepo maridhiano ya kisiasa,” alisema.
========================

Chanzo: Habari leo
nyie wanawake hivi mnajua kwa nini SUK iliundwa? Maccm Ovyo kabisa!
 
Back
Top Bottom