cardiologue
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 351
- 90
Kosa liko wapi kiongozi? Au kutaka kufaham ukawa ni ndio mdudu gani?? Acha siasa za mahaba, fikiria kwa kutumia kichwa sioWewe ni gamba, tens lililo kubuhu
K.ali.o
Kosa liko wapi kiongozi? Au kutaka kufaham ukawa ni ndio mdudu gani?? Acha siasa za mahaba, fikiria kwa kutumia kichwa sioWewe ni gamba, tens lililo kubuhu
Ndugu Malafyale,
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) imeundwa baada ya maridhiano yaliyoanzia kwenye vyama vya siasa ambavyo ni wadau wakuu katika kuunda serikali.
Maridhiano hayo hayo yanaweza vile vile kuvunjwa kwa kupitia vyama vya siasa ambavyo ni wadau wakuu, kwa maana nyingine waliokubali wanaweza wasikubaliane tena. CCM Zanzibar wameona msingi wa makubaliano umeanza kukiukwa na kwa maana hiyo, hata uwepo wa SUK unakuwa hauna maana katika ujenzi wa Zanzibar.
Hakuna kisichowezekana katika kuvunja SUK, ndiyo maana kuna utaratibu uliwekwa kikatiba wa kurekebisha au kuvunja SUK.
By the way, Kwa nini unadhani CUF wanang'ang'ania uwepo wa SUK wakati CCM hawataki?. Kwa nini na wao CUF wasiseme lugha ile ile kuuvunja inayosemwa na wanaCCM Zanzibar?.
Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu
Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.
Watakao jigawa ni wao wenyewe ccm coz ndani ya ccm kuna watu SUK hawataki iondoke karume na nassor moyo ni ccm damu.Wazanzibari kaeni mkao wa kula-CCM inawagawa tena!-Kufanikisha agenda ya 2015?
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.
Waride alisema makubaliano yanayotokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa yameanza kuvurugwa na kukiukwa kidogo kidogo katika misingi yake mikuu huku kauli za chuki na uhasama zikitawala.
Alikumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba sababu za kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni tofauti za kisiasa na kauli za chuki ambazo zilisababisha kuwepo kwa malumbano ya kisiasa katika majukwaa ya kisiasa.
Alisema kwa bahati mbaya, misingi hiyo sasa imeanza kuyumba na kuporomoka kidogo huku matusi na kejeli kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, zikichukua nafasi kubwa.
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na kauli za chuki na uhasama, zinazotolewa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ambazo zinaashiria kuyumba kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kurudisha chuki na uhasama, alisema.
Waride alifafanua kwamba CCM ambayo ni mshirika anayeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatamka bayana kwamba haipo tayari kushiriki kuunda serikali hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alifahamisha CCM haikuwa na sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu ilipata ushindi wa kutosha, uliowafanya kuunda serikali. Hata hivyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria.
CCM haioni sababu tena ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu wenzetu CUF wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uhasama zinazorudisha nyuma matarajio ya wananchi wa kuwepo maridhiano ya kisiasa, alisema.
========================
Chanzo: Habari leo
Ndugu,
Wewe unadhani serikali ya kitaifa ingepatikana bila matakwa na maridhiano ya CCM?.