Ndiyo, hawawezi kuunda tena umoja huo maana huu mwaka ndo wa mwisho kwao kuongoza Tanzania. USIWE CCM.CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.
Waride alisema makubaliano yanayotokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa yameanza kuvurugwa na kukiukwa kidogo kidogo katika misingi yake mikuu huku kauli za chuki na uhasama zikitawala.
Alikumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba sababu za kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni tofauti za kisiasa na kauli za chuki ambazo zilisababisha kuwepo kwa malumbano ya kisiasa katika majukwaa ya kisiasa.
Alisema kwa bahati mbaya, misingi hiyo sasa imeanza kuyumba na kuporomoka kidogo huku matusi na kejeli kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, zikichukua nafasi kubwa.
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na kauli za chuki na uhasama, zinazotolewa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ambazo zinaashiria kuyumba kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kurudisha chuki na uhasama, alisema.
Waride alifafanua kwamba CCM ambayo ni mshirika anayeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatamka bayana kwamba haipo tayari kushiriki kuunda serikali hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alifahamisha CCM haikuwa na sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu ilipata ushindi wa kutosha, uliowafanya kuunda serikali. Hata hivyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria.
CCM haioni sababu tena ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu wenzetu CUF wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uhasama zinazorudisha nyuma matarajio ya wananchi wa kuwepo maridhiano ya kisiasa, alisema.
========================
Chanzo: Habari leo
kwa hiyo wana uahakika wa kupita si ndio
hawataunda kwani watarudi madarakani?
Ndugu Malafyale,MwanaDiwani huwa sometimes nakulaumu sana kuleta habari bila kuzichuja kwanza ww mwenyewe!
Serikali ya Muungano ya ZNZ ipo kisheria,kuivunja unapaswa ipigwe kura ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa ushindi wa 2/3!Sasa huyu Mama muimba chakacha yy hayajui haya?
Kwa kadhia hii ya KATIBA ya Chenge KUINYIMA ZNZ uhuru wake wa maamuzi ni kabuli la CCM huko visiwani na anayedhani CCM itapata hadi 2/3 ya viti BARAZANI ili wawe huru kubadili katiba na kuvunja Serikali hii ya meto AKAPIMWE AKILI
Unaweza kukuta hata hajui ni kwa nini SUK iliundwa. Halafu anavyosema CCM haiko tayari kuunda tena inaonyesha kwa akili yake ni kuwa CCM iko pale kutawala milele. Na hiyo sio yeye pekee bali watu wengi ndani ya CCM bado wana mawazo ya miaka ya 1960's pamoja na JK kuwaambia wajiandae kisaikolojia lakini wapi!
Ndugu,Kwani serikali ya kitaifa inatokana na katiba ya zanzibar au matakwa ya ccm?
Ndugu,Kumbe madaraka mazuri mnajambishwa mnaruka kishenzi sasa mnasusaga nini? Hata kama katiba inasema msipobadirika mnatoswa mazima kususasusa na kutoka ndio kunawapa jeuri watu kuwanawisha mapema. Mkizingua serikali mtaisikia tu JF.
Maridhiano yalikuwa ni utashi wa Karume. CCM haijapata kuwa muumini wa maridhianoNdugu,
Wewe unadhani serikali ya kitaifa ingepatikana bila matakwa na maridhiano ya CCM?.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitaunda tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kutokana na baadhi ya washiriki wake kuvuruga utaratibu na misingi ya kuanzishwa kwa serikali hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.
Waride alisema makubaliano yanayotokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa yameanza kuvurugwa na kukiukwa kidogo kidogo katika misingi yake mikuu huku kauli za chuki na uhasama zikitawala.
Alikumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba sababu za kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni tofauti za kisiasa na kauli za chuki ambazo zilisababisha kuwepo kwa malumbano ya kisiasa katika majukwaa ya kisiasa.
Alisema kwa bahati mbaya, misingi hiyo sasa imeanza kuyumba na kuporomoka kidogo huku matusi na kejeli kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, zikichukua nafasi kubwa.
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na kauli za chuki na uhasama, zinazotolewa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ambazo zinaashiria kuyumba kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kurudisha chuki na uhasama, alisema.
Waride alifafanua kwamba CCM ambayo ni mshirika anayeunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inatamka bayana kwamba haipo tayari kushiriki kuunda serikali hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alifahamisha CCM haikuwa na sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu ilipata ushindi wa kutosha, uliowafanya kuunda serikali. Hata hivyo ilifanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria.
CCM haioni sababu tena ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu wenzetu CUF wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uhasama zinazorudisha nyuma matarajio ya wananchi wa kuwepo maridhiano ya kisiasa, alisema.
========================
Chanzo: Habari leo
Mbona ccm wanakuwaga mabigwa wa kujifanya wana muenzi mwalimu?mwalimu ndio alipendekeza kuwepo na serekali ya mseto mwaka 1995.baada ya uchaguzi mkuu,inamaana ccm wamemjeka tena mwalimu?hv ni kweli ccm wameamua kurudi tena kwenye siasa za kumwaga damu na chuki
Kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti yeye alikaa mjengoni 25 amekula bata kutoka ndio anaelekeza wenzio alishindwa nini. Wakati ndie aliyefuta upinzani.