CCM yawavua Uanachama watu 29

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Wanachama 29 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamevuliwa uanachama na wengine sita kushushwa vyeo mkoani Shinyanga, kutokana na kile kilichoelezwa ni kukisaliti wakati wa uchaguzi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu, ambapo miongoni mwa waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.

Akizungumzia viongozi waliovuliwa uongozi na uanachama , alisema Kanuni ya Maadili Toleo la 2012 Ibara ya 8 inasema kosa kubwa kuliko yote ndani ya chama ni kusaliti na kukiweka chama katika hali ya kushindwa katika uchaguzi na mtu anayefanya kosa hilo, lazima afukuzwe.

Wakati huo huo, alisema wanachama 12 walijivua wenyewe, hivyo Kamati Kuu ilibariki kuondoka kwao.
 
Waende kwenye chama cha mafisadi chadema. Sisi hatutaki wanafiki.
 
Mh..nilidhani sasa hivi ingekuwa hapa kazi tuu.Kumbe bado nyumba inaungua?
 
Mh..nilidhani sasa hivi ingekuwa hapa kazi tuu.Kumbe bado nyumba inaungua?
 
Usafi mzuri huanzia chumbani. habari nyepesi kabisa, Ingekuwa nzito kama usafi ungeanzia rumumba au CC.

Hata Mungu hakuanza kumfukuza maraika mdogo. Alihakikisha kamshinda shetani akaanza nae na wakaungwa malaika wafuasi wake.

Ila haishangazi maana walipojaribu approach hii enzi za MAGAMBA, ilibaki kidogo chama kisambazwe na kupotezwa.
Maamuzi magumu na mazito yana gharama sio mchezo
 
Back
Top Bottom