CCM yawavua Uanachama watu 29

CCM yawavua Uanachama watu 29

Mliambiwa msifukue makaburi, ninyi mmeanza kuchimbua,....shauri yenu zimwi litakalotoka humo halitawaacha wamoja!
Haha..wachawi wana addiction na makaburi na sehemu za matambiko. Sio rahisi hivyo kwao kuacha hiyo biashara.Ni urithi na sehemu ya maisha yao. Niliwahi jiuliza kwanini wakuu wa wilaya wanapenda matukio, nikaja gundua hawana kazi sana,hivyo lazima watafute kitu cha kuonyesha watu kuwa nao ni muhimu.
 
Wanachama 29 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamevuliwa uanachama na wengine sita kushushwa vyeo mkoani Shinyanga, kutokana na kile kilichoelezwa ni kukisaliti wakati wa uchaguzi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu, ambapo miongoni mwa waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.

Akizungumzia viongozi waliovuliwa uongozi na uanachama , alisema Kanuni ya Maadili Toleo la 2012 Ibara ya 8 inasema kosa kubwa kuliko yote ndani ya chama ni kusaliti na kukiweka chama katika hali ya kushindwa katika uchaguzi na mtu anayefanya kosa hilo, lazima afukuzwe.

Wakati huo huo, alisema wanachama 12 walijivua wenyewe, hivyo Kamati Kuu ilibariki kuondoka kwao.
makapi yote karibuni CHADOMO tukijenge chama!
 
Waende CHADEMA ambako kuna nafasi ya kujificha
mbona CHADEMA ilipomvua uanachama msaliti Zitto na genge lake chama cha walevi mlimtetea? waende kwenye chama kilichoundwa katika misingi ya usaliti ACT-_Wasaliti.
 
Chama kikubwa kama hicho hakitakiwa kufanya mambo madogo madogo hivyo; onyo lingewatosha.
 
Hawana jipya! Siasa ni itikadi tu na utashi sio lazima! Pia ni ngumu sana kufukuza maana mtaanza hisia na kuoneana tu! Hakuna lolote! Chama kilikosa mvuto sababu kukumbatia ufisadi.....kuwafukuza hakusaidii chochote! Wajipange upya serikali ifanyie kazi kero zote za wananchi na kuwafikisha mahakamani mafisadi wa escrow na wengineo IPTL Lugumi etc
 
Waende CHADEMA ambako kuna nafasi ya kujificha
Mkuu samahani, unaweza kubadili hiyo Avatar yako. Make jamaa siku hizi ni best friend wetu na Rais wetu JMP. Ni ombi tu lakini.
 
Wanachama 29 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamevuliwa uanachama na wengine sita kushushwa vyeo mkoani Shinyanga, kutokana na kile kilichoelezwa ni kukisaliti wakati wa uchaguzi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu, ambapo miongoni mwa waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.

Akizungumzia viongozi waliovuliwa uongozi na uanachama , alisema Kanuni ya Maadili Toleo la 2012 Ibara ya 8 inasema kosa kubwa kuliko yote ndani ya chama ni kusaliti na kukiweka chama katika hali ya kushindwa katika uchaguzi na mtu anayefanya kosa hilo, lazima afukuzwe.

Wakati huo huo, alisema wanachama 12 walijivua wenyewe, hivyo Kamati Kuu ilibariki kuondoka kwao.
Bundi anavinjari ...............
 
Back
Top Bottom