CCM yawavua Uanachama watu 29

CCM yawavua Uanachama watu 29

Chenge si anatoka shinyanga mbona sijaona jina lake na hao walio fukuzwa wamefanya dhambi gani kubwa kushinda mafisadi yaliyojaa hapo Lumumba
 
Wanachama 29 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamevuliwa uanachama na wengine sita kushushwa vyeo mkoani Shinyanga, kutokana na kile kilichoelezwa ni kukisaliti wakati wa uchaguzi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu, ambapo miongoni mwa waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.

Akizungumzia viongozi waliovuliwa uongozi na uanachama , alisema Kanuni ya Maadili Toleo la 2012 Ibara ya 8 inasema kosa kubwa kuliko yote ndani ya chama ni kusaliti na kukiweka chama katika hali ya kushindwa katika uchaguzi na mtu anayefanya kosa hilo, lazima afukuzwe.

Wakati huo huo, alisema wanachama 12 walijivua wenyewe, hivyo Kamati Kuu ilibariki kuondoka kwao.
Acha wafu wazike wafu wao
 
Waende kwenye chama cha mafisadi chadema. Sisi hatutaki wanafiki.
OMG Yamekua hayo!!!! Yaani CCM wanawaita CDM chama cha mafisadi. Kweli kabla ya kufa hujaumbwa. CCM imeacha lini kuwa mtambo wa kuzalisha mafisadi?
 
Siasa bwana, nilidhani kwenye vyama vikongwe na vikubwa hakuna kufukuzana / timua timua kama tunavyoshuhudia kwenye vyama vichanga.
 
unafiki ni kitu kibaya sana mmewafuza uanachama watu wadogo wakati akina Sophia Simba au Nchimbi na hata Mwapachu mmekaa nao meza moja huku walila posho bila jasho
 
Hawa jamaa wakali sana wanaposikia "kusalitiwa". Lakini mambo mengine yenye maslahi makubwa kwa nchi, wapooole!
 
Back
Top Bottom