Ccm yawatelekeza bunda wanachuo wa saut tabora bunda

Ccm yawatelekeza bunda wanachuo wa saut tabora bunda

KELVIN GASPER

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,066
Reaction score
454
Kile kilichokuwa kinaonekana kama ccm kujipenyeza katika taasisi za elimu ya juu, kimeingia doa baada ya ccm mkoa wa tabora kuwaandalia safari ya kitalii wanachuo wa saut kwenda mbuga ya serengeti. hata hivyo baada ya kufika huko, basi lililotumika kuwasafirisha limeharibika. walichofanya ccm mkoa ni kuwatafutia usafiri wa kuwafikisha bunda na kuwatelekeza hapo. wanahaha kujitafutia usafiri wa kuwarudisha tabora.
 
Ngoja hao vijana wakome. Huwezi ukajiita msomi wa kweli na bado ukashabikia magamba. Labda wasomi njaa kama akina mwigulu na nape.
 
Ngoja hao vijana wakome. Huwezi ukajiita msomi wa kweli na bado ukashabikia magamba. Labda wasomi njaa kama akina mwigulu na nape.

Nape sio msomi, labda yule mwenzake aliyenunua jina la mtu akaenda sekondari yeye.
 
Wamekomeshwa tena wamshukuru Mungu hawajaachwa mbugani,wasomi wanaandaliwa safari kama watoto wa chekechekea? Vijana wengi wa ccm wanapenda vya bure haswa usafiri,pilau na t-shirt hicho ndo kinawaponza.Wazazi wao wanategemea wapo chuo ili kuondoa ujinga kumbe ndo kwanza wanaamini ujinga.Hawa siyo aina ya vijana aliyowategemea Mwl.Nyerere kumbe ndiyo maana hawakemei ufisadi wa kutorosha wanyamapori kwa kuwa wanapandishwa magari bure kwenda kutalii serengeti.Lakini pia natoa rai kwa ccm,tafuteni njia nyingine ya kuwateka kiakili wafuasi wenu,siyo mara ya kwanza kuwatelekeza wafuasi wenu kwani mlifanya hivyo kwenye sherehe za miaka 35 jijini mwanza kwa kuwatelekeza wafuasi wenu kirumba wakaanza kuomba omba mtaani..."Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa Chama"...(Za wengine zidumae)
 
Wanachuo wengi ni watu wa tamaa na wapenda bure, hasa wanachama wa ÇCM VIJANA.

ACHA WASOTE WAJIFUNZE.
 
Chezea chichiem weye uliza wale wa ARUSHA waliofungua kesi ya LEMA Wanatakiwa kulipa mamilioni wenyewe
 
Wanaodidimiza maendeleo ya TZ ni hawa tunaowaita wasomi wa kitanzania!
 
Poleni sana,next time mjifunze,acheni akili za kushikiwa!
 
Kelvin Hii Avatar Yako Mbona inanitisha Mimi jamani,kwa hao wasomi walakini ......watajijua chezea Ccm kwa urongo na udanganyifu.
 
Kelvin Hii Avatar Yako Mbona inanitisha Mimi jamani,kwa hao wasomi walakini ......watajijua chezea Ccm kwa urongo na udanganyifu.

We jitahidi kuizoea bana. hadi leo hii boxing day bado wanachuo wapo bunda. wachache ndio wamefanikiwa kuondoka kwa gharama zao baada ya kuwezeshwa na jamaa zao wa karibu.
 
Safi sana maana wamewatumia kama kondumu,wanafunzi gani wa elimu ya juu ambao mbaka leo hawajitambui?
 
Back
Top Bottom