CCM yawakaanga Bashe, Kigwangalla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yawakaanga Bashe, Kigwangalla

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Sep 1, 2012.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,146
  Likes Received: 988
  Trophy Points: 280
  Mustapha Kapalata, Nzega na Frederick Katulanda, Mwanza | Mwananchi - Sept 01, 2012

  SAKATA la makada wa CCM, Hussein Bashe na Dk Hamis Kigwangalla kutoleana bastola, limechukua sura mpya baada ya uongozi wa chama hicho Wilaya ya Nzega, kutaka suala hilo liondolewe polisi ili walishughulikie kimyakimya ndani ya chama kwa madai kuwa linakifedhehesha chama.

  Tayari taarifa zimeeleza kuwa chama hicho jana kiliwaandikia barua ya kuwaita kwenye kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya makada hao kuwataka wajieleze kwa tukio la kugombana hadharani.

  Katibu wa CCM Mkoa Tabora, Idd Ame alithibitisha kutoa agizo kwa uongozi wa chama hicho Nzega kushughulikia suala hilo nje ya dola na kueleza kuwa kinachofanyika sasa ni utekelezaji wake.

  "Tulikwisha kutoa maelekezo kwa Katibu wa CCM wa Wilaya wa namna ya kushughulikia suala hili. Atakuwa anajua zaidi mkimuuliza," alisema Ame.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Nzega, Kajoro Vyohoroka alisema kuwa makada hao wataitwa kwenye kikao cha dharura kilichoitishwa kwa agizo la CCM mkoa.

  Baada ya kikao hicho, mapendekezo yake yatapelekwa kwa Katibu wa mkoa ambaye ndiye aliyeagiza kifanyike," alisema Vyohoroka.

  Hata hivyo, Vyohoroka alisema kuwa kwa itifaki ya CCM, yeye hataueleza umma mapendekezo ya kikao hicho, badala yake atakayefanya hivyo ni Katibu wa CCM wa Mkoa. Hatua hiyo ya CCM kutaka kushughulikia suala hilo nje ya mkono wa dola limekuja huku polisi ikiwa bado inaendelea na uchunguzi wake.

  Dk Kigwangalla akataa suluhu
  Dk Kigwangalla alithibitisha kupokea barua ya kuitwa katika kikao hicho na kusema kwamba anatambua kuwa ni cha dharura mahsusi kwa ajili ya kuwasuluhisha. Hata hivyo, alisema hayupo tayari kukubaliana na jambo hilo.

  "Nimepokea, barua ya wito wa kikao najua wanataka kutusuluhisha, lakini nasema sipo tayari kwa sababu chama wanataka kusuluhisha suala hili wakati mimi nimeshachafuka, sitakubali," alisema.

  Awali, Dk Kigwangalla alisema alifikiria kuachana na suala hilo kwa kuwasamehe wote waliomkosea isipokuwa Bashe lakini sasa amebadili mawazo.

  "Nilianza kufikiria kuwasamehe walau wale walionishambulia kwa matusi na kunisukuma kwa dharau. Nilitaka abaki yule aliyetishia kunipiga risasi na kuniwinda, lakini sasa siko tayari kufanya hivyo, nitaendelea na kesi hii hadi mahakamani na ukweli utadhihirika kule na haki itatolewa," alisema.

  Alisema uamuzi wake umekuja kutokana na kuona ameanza kugeuziwa kibao huku akisema imani yake ni kuwa atapiganiwa na Mungu.

  Bashe ataka mkondo wa sheria
  Bashe alisema hajapata barua ya kuitwa kwenye kikao hicho ila anayo taarifa kwamba kikao hicho kinafanya tathmini ya uchaguzi uliofanyika wilayani humo.

  "Sina barua na sasa niko safarini kuelekea Dar es Salaam. Ninachojua kikao hicho ni cha tathmini ya uchaguzi na Kigwangalla ameitwa kwa kuwa ni mjumbe. Mimi siyo mjumbe, lakini kama watajadili suala hilo wanaweza kuniita," alisema.

  Hata hivyo, alieleza kuwa msimamo wake ni kutaka suala hilo liende mahakamani ili kulinda heshima ya chama hicho.

  "Niseme tu kwa kifupi kwamba, utaratibu wa sheria unapaswa kuheshimika."

  Alisema ili chama kiheshimike kinapaswa kusimama kwenye sheria hivyo haoni sababu za uamuzi wa suala hilo kuondolewa polisi kwa vile ndicho chombo husika kwa masuala hayo.

  RPC asisitiza uchunguzi
  Kamanda wa Polisi Mkoani wa Tabora, Antony Lutta alisema kwa simu jana kwamba upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea.

  Atakayebainika kutumia silaha kinyume cha taratibu, hatua itakayochukuliwa ni kunyang'anywa silaha na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria kama vile kupelekwa mahakamani.

  Alisema sheria ya umiliki wa silaha hairuhusiwi kutishia maisha watu pasipo sababu za msingi na kuongeza kuwa vibali vya kumiliki silaha hutolewa kwa mtu mwenye akili timamu.

  "Bado tunaendelea na upelelezi juu ya hilo na endapo ukweli utabainika basi mtu huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma," alisema Kamanda Lutta.
   
 2. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  na mbado mpaka kieleweke....rpc anasema anakabidhiwa silaa mtu mwenye akili timamu haya bwana
   
 3. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hata rage ........timamu haya bwana
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du ugomvi wa kitoto Bwana kila mtu anataka aonekane kidume, mara Ww sio chaguo la wanaNzega na huyu mara ww sio Raia wa Tanzania
   
 5. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nawasihi ndugu zangu hawa waache fujo.
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  CCM kwishney!
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana kabisa na swala hili. Lazima liishie Mahakamani maana huko ndiko ukweli utaanikwa.

  Vikao vya CCM ni vya FUNIKA KOMBE na wanakuweka Kiporwa. Siku ikifika wanakufunua na huna pa kwenda.

  IT'S NOW OR NEVER.
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  Wote wanafiki tu!!!!!!
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Yote haya yamesababishwa na vitumbua na maandazi!
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Wanyang'anywe tu bastola aka mguu wa kuku aka chuma aka ngoma
   
 11. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama kawaida hawa ni ndugu wa BABA mmoja CCM, ngoja tushike jembe tukalime ......................!.
  Wakija kusituka tayari mavuno ni mengi, hatutawaua njaa tutawapikia ugali.
   
 12. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo CCM wameamua kuidharau Mahakama Live! Jambo la kutishia kuua tena kwa Silaha ni jambo la kimahakama, leo hii CCM wanataka litoke mahakamani liende kwao ndo wanaoweza kuliamu vizuri, Duh! Labda ni kwa sababu wanawajua hata aina ya Majaji waliowateua uwezo wao ni mdogo kuliko wa Nape ndio maana wanataka walishughulikie wao wenyewe.
   
 13. M

  MR.KUMEKUCHA Senior Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtindo huu CCM inajizika yenyewe.Hata wasio na akili timamu wamejua kuwa cha hiki kimefika ukingoni walio baki watakufa kisabuni tu kama 'ninawie'.MUNGU IBARIKI Tz.Amani na upendo kwa vitendo.
   
 14. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna kosa la jinai viachiwe vyombo vya dola washugulikie jinai.ccm waache kuviingilia vyombo vya dola maswala ya jinai hayawahusu.ccm hawazuiliwi kuwachukulia hatua za kinidham wanachama wake na huku vyombo vya dola vikiendelea na kazi zao kuliko hivi ambavyo ccm wanataka kufanya.labda kama wanataka kulindana.
   
 15. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  CCM wanachojali ni heshima ya chama, wanaficha/kukanusha kila kitu kulinda CHAMA.
   
 16. C

  Cognitivist JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 973
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda hii comment yako, majaji hata hukumu hawajui kuandika na mwingine nasikia anajiandaa kupiga kitu cha sapu. Mmh kweli ccm imejipanga.
   
 17. Fyengeresya

  Fyengeresya JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 702
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Wanaogopa kuumbuana maana hata mafisadi wao kila wizi unasemekana ulipitishwa na baraza la mawaziri isijekuwa hata mauaji ya vikongwe na maalubino yamepitishwa na baraza la mawaziri ndiyo maana hayaishi.
   
 18. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa nani katishiwa maisha..BASHA au KINGWANGWALA...Maana naona kila mmoja anasema yeye ndo katishiwa...kwahiyo ilikuweka wazi lazima muhimili wa serekali utumike na sio jopo la wauza maneno wa sisim...kukaa na kupindisha sheria...
  Kutishiwa maisha na kutisha maisha ni kosa la kisheria sio kichama...ndo mnaanza hivi hivi kidogo kidogo matokeo yake hata kesi kubwa mnaweza kusema mtazitatua kichama..Acheni mambo yasio leta tija nchini...WAPELEKWE MAHAKAMANI
   
 19. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Washaidharau Mkuu wangu,kwa kuongelea suala lilipo mahakamani kwenye vikao. Hivi katika hao Bashe na Kigwa wameshinda nafasi gani?au uchaguzi bado haujafanyika?
   
 20. H

  HByabatto jr Senior Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waacheni wanawali wale wali wao...!
   
Loading...