CCM yaupoteza upinzani Tunduma

Wamesomba watu na mafuso halafu mkutano ulipo isha tu kila mtu ikawa kivyake. Wamepata shida sana hasa akina mama.
 
Huwezi kuupoteza upinzani KAMA hujaongelea kufeli kwa wanafunzi na mgao wa umeme!
Tunduma na Mbeya kwa ujumla mimi nawajua...
Wako kama Wahaya
 
CCM msicho kijua ni kuwa watu wa Mbeya huwa si wanafiki, nyie njoo na ahadi kibao halafu mlete mchezo
 
Gari au Lori ni usafiri kama usafiri mwingine, kama CCM wananyenzo au uwezo wa kusafirisha mashabiki wao kwenda kwenye mkutano Tatizo liko wapi?.
Wangekuwa wanatumia FFU kuwapandisha kwenye magari hapo kweli lingekuwa tatizo. Lakini kuwasafirisha tu, hii maana yake raia wenyewe kwa utashi wao wako willing kuhudhuria, CCM inafacilitate usafiri wao tu.
 
Wandugu inawezekana wengi hawaelewi kwamba Katiba ya CCm ni kati ya moja ya maajabu saba duniani!
Ni kwamba vyeo vyote unaweza kugombea, lakini cheo cha Mwenyekiti wa Taifa hakuna anayeruhusiwa kugombea. Mgombea wa kiti hicho anateuliwa na Halmashauri Kuu. Kwa maneno mepesi Huwezi ukaenda CCM kuomba femu za kugombea uenyekiti wa Taifa ukazipata. hazipo!
Kwa mantiki hiyo, Halamshauri Kuu kwa woga hawawezi kuteua mgombea wa pili (wa Kiti hicho) ili apambane na mgombea mtarajiwa ambaye moja kwa moja anakuwa Rais
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameuangamiza kabisa upinzani Tunduma katika mkutano mkubwa uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwaka.
Nape Jembe la Chama alibebwa juu juu kama shujaa na pia Mama Migiro alishangiliwa sana.

Katika hali isiyo ya kawaida CCM Imedhihirisha kukomaa kisiasa baada ya kuongea mambo ya msingi yenye kueleweka.

upinzani unaangamizwa jwa mkutano mmoja? hupajui Tunduma,waulize polisi
 
Back
Top Bottom