CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi

CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi

Nasema toka rohoni mwangu nape uwezo wake wa kufikiri nimdogo sanaa! Sijui nivigezo gani vilitumiwa ili achaguliwe,au ni elimu yake ndogo ? Tuwaachie wananchi watoe hukumu 2015. Ndipo mtajua zipi chuya na mchele.
 
furaha ya wazanzibar kuona tanganyika munapigana mbona kidogoo tuuuu
 
ccm siasa zimewashinda sasa wanaua watu kupitia nguvu ya dola.
 
Huwezi kumfananisha zito na Nnauye hata siku moja, kuhusu mauaji Nauye kaelezea hisia zake na isitoshe ametoa tamko ambalo linaeleweka kwa mwenye akili, lkn wanaomshutumu nadhani wako kiitikadi zaidi, Issue hapa huwezi kuwalaumu polisi peke yao kwa ssababu hata wao askari wao wameumizwa na bomu hilo, swali la kujiuliza hapa hivi polisi wanaweza kujidhuru wenyewe kwa bomu, na je polisi wangewweza kutumia silaha bila mkutano wa silaa ambaye tayari alishatanguliza msg za vitishop vya mauaji kwa IGP hata kabla ya mkutano huo? ulitegemea polisi ambao wao kazi yao ni kuzuia madhara yasitokee, wasingeenda kwenye tukio wananchi walio wengi wakapata majeraha, angelaumiwa nani wakati silaa alishatoa tahadhari ya kujitoa mhanga? Mimi nadhani polisi wamefanya kazi yao lkn yaliyotokea ni ajali kazini na inawezekana kabisa lile bomu hakulitupa polisi, kama ni polisi basi wangemshuti kwa mbali na sio karibu vile hadi na wao wajeruhiwe, kuna mambo mengi ya bkujiuliza hapa, kuna uwezekano kabisa kama kulikuwa na malumbano au uhasama aliyekufa akajitoa mhanga. au polisi wamerusha kwa bahati mbaya katika kunyang'anyana silaha na marehemu, au watu wa nje kurusha kwenye mkusanyiko, na mambo hayo yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina, na hiyo tume ili kubaini kilichosababisha mauaji, na kuendelea kushutumiana na kuruhusu hisia za kisiasa zaidi ni kuonyesha kutokukomaa kwa demokrasia. kuhusu issue ya tume iko sawa kwa sababu pamoja na kuwa polisi ni watuhumiwa bado nao wameumizwa, kwa hiyo kupewa nafasi kwenye tume ni haki yao kwani nao ni binadamu na siyo vyuma kama kina lissu na silaa wanavyofikiria. kwa hiyo tuache mahaba ya vyama.

Waropokaji wasio tumia akili ni wingi hapa, hivi wewe hata ukileta mtoto wa chekechea huwezi kuona kwenye hii picha nani alikuwa anamuuwa nani????
attachment.php
 
Waropokaji wasio tumia akili ni wingi hapa, hivi wewe hata ukileta mtoto wa chekechea huwezi kuona kwenye hii picha nani alikuwa anamuuwa nani????
attachment.php
Unajua unachekesha sana ndg ha ha haaa, hivi mumeo akinya kitandani na wewe utakunya? na je kitanda hicho kitalalika kweli? je mwenzie akivunja sheria bila kusababisha madhara, akafanikiwa na wewe ukavunja sheria kwa kufuata mkumbo ukasababisha madhara na ukanaswa. je utasema uko halali,? kumbuka Ignornce of the law is not a difence. mumelikoroga na mutalinywa tu, no way.
 
We Nape na CCM yenu naona mmeishiwa sera. Sheria gani inaruhusu kuua? Mtu kama ana hatia askari wanashindwaje kumkamata na kumpeleka sehemu husika. Nadhani mauaji haya yanapangwa na baadhi yenu wana ccm ili kuwatishia wananchi wasihudhurie mikutano ya cdm. Hiyo ni kufirisika kifikra, naomba muigi siasa kama za marekani. kama watu wamewachoka mtawalazimishaje kuendelea kuwatawala?
 
Slaa anatakiwa apandishwe mahakamani kwa kuchochea vurugu na kumtisha IGP
 
Ni kweli mkuu. CMM na Polisi nadhani kuua raia wasio na hatia kwao ni haki. Kuvamia mikutano ya ndani ya CDM kwao ni haki. Lakini mikutano ya CCM haigusi hata kidogo. Mimi najiuliza kwamba hivi kwa wakati huu CCM na serikali yake wamezipeleka akili zao likizo? Jamani DCI Manumba, Nchimbi, Mwema na Polisi wengine walioshiriki mauaji ya raia wasio na hatia wanasubiri nini? Kwa nini wasijiuzulu?
Hilo tamko la nape linatia hasira sana, mauaji yote yanafanywa na polisi, jiulize mkutano wa CHADEMA uliofanyika jangwani na ukajaza watu na wote wakaondoka salama. Je waliohudhuria Morogoro na Iringa tofauti yao ni nini? Magamba kubalini kwamba sasa mna pumulia mashine!
 
Nape uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana. Ataenda mahakama ya kimataifa na yeye
 
"Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha", "Hakuna mwanzo usiokuwa na Mwisho" na Hakuna nafasi ya kuficha ukweli ipo siku uongo na ukweli utajitenga kama ukichanganyanywa pamoja.
Naomba watu wazidi kutoa elimu ya uraia kwa wingi kwani wananchi waliowengi hawajui haki zao na hili likiwezekana ndo ukombozi utakuja
Achananeni na vyama vyenye kujuana iwe CCM au Chadema hapa kila mmoja wetu atoe elimu juu ya wale waliokaribu naye na kotekote utakapokuwa muda huu ni mzuri
Elimu si kazi ya Chadema au CUF pekee ila tuwaelimishe ndugu zetu, dada zetu, watoto wetu, mama zetu, babu zetu, bibi zetu, nyanya zetu, wake zetu, waume zetu, wanafunzi wetu, walimu wetu, majirani zetu na wote wanaohusika na nchi hii. Kazi hii ikifanyika muda huu mpaka 2015 mabadiliko yatakuwepo na wananchi wataacha unafiki maana unafiki wao ni kutojua haki zao na hawana elimu ya uraia. Na chama tawala ndo mtaji wake wa kila uchaguzi kwa kutumia ghiliba na hila za kila namna ili kurudi uongozini na pia kuwapeleka watoto wa vigogo kugombea katika sehemu walikozaliwa wazazi wao hata kama hawajawahi kukaa huko maisha yao yote au mwaka mmoja.
 
nape jifunze kuwa mkweli sio wana siasa walioleta fujo za vifo vya mwanahabari huyo ni ninyi baada ya kuona mumezidiwa kila siku munapoteza mvuto. mtaondoka tu mtake mstike kwani muna ua raia

Nape ni mpuuzi msimsikilize
 
Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa askari watatu wa kuzuia fujo. Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.

CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.

Vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu.

Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Mnauye jijini Mwanza leo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kulaani mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi wa Chanel Ten Mkoani Iringa wakati wa vurugu za polisi na wafuasi wa Chama cha CHADEMA mwezi September 2 mwaka huu 2012


Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.
Siku zote hizo alikuwa anajishauri kutoka na mistari hiyo tuu.
 
huko watawala ni CUF bhana CCM wanajikomba kwa CUF sababu ya uroho wa madaraka. Miaka yote CUF wanashinda CCM ni wizi wa kura tu

Huu ni ukweli mtupu. CUF huwa inashinda Zanzibar kila uchaguzi! Sasa CUF wajipange wachukue Zanzibar na CHADEMA tunachukua Bara, halafu tunaunda Muungano wenye maslahi kwa wananchi wa pande mbili, tuiizike CCM na isahaulike kote Bara na Visiwani!
 
Unajua unachekesha sana ndg ha ha haaa, hivi mumeo akinya kitandani na wewe utakunya? na je kitanda hicho kitalalika kweli? je mwenzie akivunja sheria bila kusababisha madhara, akafanikiwa na wewe ukavunja sheria kwa kufuata mkumbo ukasababisha madhara na ukanaswa. je utasema uko halali,? kumbuka Ignornce of the law is not a difence. mumelikoroga na mutalinywa tu, no way.

Haya matukio yalifanyika siku moja, yote yalihusu kuvunja sheria ya sensa kama mnavyodai, sasa kwanini katika kuyashughulikia iwe tofauti? Sheria haipaswi kubagua au kupendelea! Tunataka majibu kwa wahusika waliyachukuliaje haya matukio yote! hata hivyo chadema hatukufanya mkutano wa hadhara!
 
Nape hana jibu maana anaagizwa tu huyo kusema, hakuna consistency ktk decision making, hili liko wazi, serikali imepinda kama babu anayetembea kwa fimbo fupi!
 
huna hoja ndugu yangu, rudi masomoni, huwezi kuona kuwa hapa ni ccm kujilinda na kuhafifisha wenzao maana wao wana (matumizi mabaya ya) nguvu ya dola?
 
Back
Top Bottom