CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Sep 5, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa askari watatu wa kuzuia fujo. Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.

  CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.

  Vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu.

  Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Mnauye jijini Mwanza leo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kulaani mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi wa Chanel Ten Mkoani Iringa wakati wa vurugu za polisi na wafuasi wa Chama cha CHADEMA mwezi September 2 mwaka huu 2012


  Imetolewa na;
  Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.
   
 2. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iringa
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

  Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

  Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

  Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

  Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

  Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

  Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

  Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

  Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

  Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

  Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

  Imetolewa na;
  Nape Moses Nnauye
  Chama Cha Mapinduzi
  Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Siamini kwamba ni kauli ya Nape hii
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  Hakuna sheria yeyote inayohalalisha kumpiga mwananchi risasi ama bomu wakati wakiwa hawana silaha.Ni watanzania tu ndo watakubali ujinga huu.
   
 5. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Amri iliyotolewa ya kusitishwa shuhuli za chama cha siasa wakati wa sensa ni kwa ajili vyama vingine isipokuwa CCM? Nape naomba jibu ili niendelee kukusikiliza ktk siku za usoni.
   
 6. Dangire

  Dangire JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  gamba hilooo! utawala wa sherie upi? wa-kikoloni? kumbuka hata wakoloni walitumia sheria kuwanyamazisha waafrika.laiti wangetii kila sheria ovu, kandamizi na za kidhalimu basi nchi za afrika zisingelipata uhuru. nadhani ccm mnafurahia kuwa na hiyo policcm. mnaitumia mtakavyo. siku yenu yaja.
   
 7. Man 4 M4C

  Man 4 M4C JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 737
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nape ndiyo muuaji wewe na ccm yako na serikali yako,acha unafiki ungali kijana
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Nape ni mweupe kichwani. Na sitegemei press release ya maana toka kwake!!! Siku zote alikuwa wapi hajatoa press? Alikuwa anajipanga au ni baada ya kuona kila mtanzania amekemea jambo hilo? Viongozi wa dini nao wamesimama kidete!!! Subirini!!!
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Untitled-1.jpg

  CC:
  Nnauye Jr Ritz chama

  Hivi Nape Hakuiona Hii Picha wakati anaandika hiyo Taarifa yake
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa toka ampate Mwarabu wake nayeye akili zimemhama kabisa! Kule nyuma hakuwa hivyo!
   
 11. mozes

  mozes Senior Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  We uko kwnye tume ilioundwa na Mwema ee! Huwez kua na majibu kama hayo yaliojaa unafki 2pu! Kajipange tena
   
 12. s

  sad JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nape jifunze kuwa mkweli sio wana siasa walioleta fujo za vifo vya mwanahabari huyo ni ninyi baada ya kuona mumezidiwa kila siku munapoteza mvuto. mtaondoka tu mtake mstike kwani muna ua raia
   
 13. m

  mzalendoasilia Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningependa kumshauri ndugu NAPE kwamaba silazima kila siku azungumze kwenye vyombo vya habari , hata kama matukio anayojaribu kuyatolea maelezo yako wazi kwamba muhusika ni serikali na ccm chini ya kivuli cha polisi! Haihitajiki kuwa na Phd kujua utoto ulioko ndani ya siasa za ccm hivi sasa na propaganda za kitoto wanazojaribu kuzitumia kujibu hoja za msingi. Haiingi akilini walioua ni polisi na ISSUE hapa ni mauaji ya kutumia bomu, hivi in this kind of situation mtu anazungumzia kuhusu chadema. Is that the main issue? swali ni kwamaba kwanini polisi waue watanzania for very cheap reasons?Haihitaji akili nyingi kujua ni nani anawatuma polisi, jaribu kuangalia watanzania wote wanalaani polisi EXCEPT ccm , wao wanalaani chadema! Tatizo ninaloliona ccm ni coordination ya mambo yao! Hata kama MPANGO ni kuifuta chadema , basi mjaribu ku organize kama watu ambao mnatumia common sense! Every propaganda ya ccm nowadays hata mtoto wa standard 1 anajua whats going on! Hii ni moja ya hasara za kupeana madaraka kindugu bila kuangalia qualifications, ndani ya ccm there is alot of capable people ambao wangeweza kufanya vyema than what we see and hear nowadays frm the so called ccm speakers! Hivi ndugu yangu Nape unapozungumzia utawala wa sheria, do u exactly know what you are saying? Kuua raia kwa bomu ni utawala wa sheria? au kwako utawala wa sheria is only for chadema to obey what ccm want them to do? Hivi kweli ccm ndio inatuhubiria habari za utawala wa sheria wakati wao ni wavunja sheria namba moja? Mkitaka watu waheshimu sheria inabidi na nyinyi muonyeshe mfano wa kuziheshimu hizo sheria! Sio sheria kwa chadema but ikija kwa ccm it is not applicable! Kujaribu kuzuia haki za watu kwa matendo yasiyohaki hakuwezi kufanikisha lengo lenu la kutotaka kukosolewa! DARKNESS has never won any war against LIGHT, believe me it is just a matter of time when you ccm will realize that!
   
 14. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Hahahhahaa Bwana Pampasi again
   
 15. s

  sad JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nape mnafiki tu. tunasubiri mpelekwe za mahakama za kimataifa
   
 16. s

  sad JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama kuna katibu mwenezi asiyejua kazi yake ni nape. yeye anajua kueneza chama nikuongea na waandishi wa habari na kbali mauaji ya pilisi ndio uenezi
   
 17. a

  adolay JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Sion kama akili imetumika kuandika na kutoa tamko la ccm

  Wanataka uchunguzi gan ilhal wamesha toa hukum kwa cdm. Hekima, busara na heshima katika tamko hili la ccm hakuna na limepoteza weledi na maana kabisa kwa kuingiza ushabiki huku likihitimisha upuuzi kwa cdm, nan kathibitisha kama ni cdm na siyo ccm au polisi. Nape kachanganyikiwa.
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Huyu ni mnafiki kama Zito!!
   
 20. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,688
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hilo tamko la nape linatia hasira sana, mauaji yote yanafanywa na polisi, jiulize mkutano wa CHADEMA uliofanyika jangwani na ukajaza watu na wote wakaondoka salama. Je waliohudhuria Morogoro na Iringa tofauti yao ni nini? Magamba kubalini kwamba sasa mna pumulia mashine!
   
Loading...