Kwahiyo sheria ya kuzuia mikutano wakati wa sensa inaihusu chadema peke yake? Kuwa ccm siyo kibali cha kuacha kufikiri!
Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.
Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*
Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*
Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *
Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.
Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.
Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*
Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.
Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.
Kama hili tamko limetolewa na Nape basi naomba afanye juhudi hata kama ni kwa unafiki alikane aende akatubu.Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa askari watatu wa kuzuia fujo. Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.
CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.
Vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu.
Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Mnauye jijini Mwanza leo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kulaani mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi wa Chanel Ten Mkoani Iringa wakati wa vurugu za polisi na wafuasi wa Chama cha CHADEMA mwezi September 2 mwaka huu 2012
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.
Kumbe waliambiwa wasitishe mikutano yao mpaka sensa iishe?
Wanaleta fujo na machafuko halafu wanakuja humu JF kujidai wameonewa? hawa wana matatizo makubwa sana na wakiendelea kuachwa wataitumbukiza shimoni hii nchi, wadhibitiwe mapema sana, hatua nzuri ni kukifuta tu hiki chama.
Hapa nasema yeyote aliyeamrisha watu waende kwenye mkutano wakati Serikali imezuia.
Nape nilikuwa nakuheshimu sana lakini umekuwa mwendawazimu.Siamini kwamba ni kauli ya Nape hii
Hakuna sheria yeyote inayohalalisha kumpiga mwananchi risasi ama bomu wakati wakiwa hawana silaha.Ni watanzania tu ndo watakubali ujinga huu.
polis wamkamate nape maana anajua ukweli wote,yeye ndiyr mratibu wa haya mauaji ndiyo maana aliwatahadhalisha wananchi,ana alivyo mpumbavu,anasema wananchi hawakusikia ushauri wake.wako kwenye utekelezaji.liwalo naliwe.by pinda"chadema wana kila sababu ya kuawajibika kwa matukio ya kinyama yanayotokea kwenye mikutano yao ta kisiasa,,
na ni aibu kwa matukio ya namna hii kutokea kwenye mikutano ya kisiasa,, viongozi wa kisiasa ni lazima wawajibike kwa umma,, lakini matukio kama haya yamekuwa yakitokea bila viongozi kuwajibika" nukuu ya kauli ya nape nauye.. Source habari leo,,,
....that is true hapa anayepashwa kushitakiwa ni babu slaa wala sio polisi kwani walikuwa wanatimiza kazi waliyosomea, kama walikatazwa kuandamana kwa nini waliandamana? hii ni hatari kwa nini tusiangalie kenya ilivyokuwa kipindi kile waliokuwa wanapigana na kuuana walikuwa ni vyama pinzani tu,tendwa futa hiki chama cha wauaji
Hivi jamani nchi hii mnavyoona bado kuna amani au ni utulivu tu unatawala?Ila siku wananchi wakichachamaa ndo watajua kama kuna amani au hakuna,watu wanalala njaa,madawa hosp hakuna,wamama wanajifungulia njiani,ufisadi wa kutisha kwenye pesa ya uma,haki za watu zinaminywa n.k, halafu tudanganyane kuna amani,au kwa vile wenzetu wapo kinvulini wanauhakika na maisha yao,ila mwisho wao ukaribuItakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa askari watatu wa kuzuia fujo. Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.
CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.
Vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu.
Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Mnauye jijini Mwanza leo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kulaani mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi wa Chanel Ten Mkoani Iringa wakati wa vurugu za polisi na wafuasi wa Chama cha CHADEMA mwezi September 2 mwaka huu 2012
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.
Huwezi kumfananisha zito na Nnauye hata siku moja, kuhusu mauaji Nauye kaelezea hisia zake na isitoshe ametoa tamko ambalo linaeleweka kwa mwenye akili, lkn wanaomshutumu nadhani wako kiitikadi zaidi, Issue hapa huwezi kuwalaumu polisi peke yao kwa ssababu hata wao askari wao wameumizwa na bomu hilo, swali la kujiuliza hapa hivi polisi wanaweza kujidhuru wenyewe kwa bomu, na je polisi wangewweza kutumia silaha bila mkutano wa silaa ambaye tayari alishatanguliza msg za vitishop vya mauaji kwa IGP hata kabla ya mkutano huo? ulitegemea polisi ambao wao kazi yao ni kuzuia madhara yasitokee, wasingeenda kwenye tukio wananchi walio wengi wakapata majeraha, angelaumiwa nani wakati silaa alishatoa tahadhari ya kujitoa mhanga? Mimi nadhani polisi wamefanya kazi yao lkn yaliyotokea ni ajali kazini na inawezekana kabisa lile bomu hakulitupa polisi, kama ni polisi basi wangemshuti kwa mbali na sio karibu vile hadi na wao wajeruhiwe, kuna mambo mengi ya bkujiuliza hapa, kuna uwezekano kabisa kama kulikuwa na malumbano au uhasama aliyekufa akajitoa mhanga. au polisi wamerusha kwa bahati mbaya katika kunyang'anyana silaha na marehemu, au watu wa nje kurusha kwenye mkusanyiko, na mambo hayo yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina, na hiyo tume ili kubaini kilichosababisha mauaji, na kuendelea kushutumiana na kuruhusu hisia za kisiasa zaidi ni kuonyesha kutokukomaa kwa demokrasia. kuhusu issue ya tume iko sawa kwa sababu pamoja na kuwa polisi ni watuhumiwa bado nao wameumizwa, kwa hiyo kupewa nafasi kwenye tume ni haki yao kwani nao ni binadamu na siyo vyuma kama kina lissu na silaa wanavyofikiria. kwa hiyo tuache mahaba ya vyama.Huyu ni mnafiki kama Zito!!