CCM yatenga mabilioni kuwaghilibu mawakala wa CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yatenga mabilioni kuwaghilibu mawakala wa CHADEMA!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Sep 26, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,842
  Likes Received: 420,418
  Trophy Points: 280
  Unapokuwa umemaliza kupiga kura yako unaishia kwenda nyumbani ukifikiri ya kuwa mshindi atapatikana kutokana na kura zilizomo kwenye sanduku la mahesabu ya kupigia kura. I MUST SAY, IT IS A WRONG ANSWER.

  Kwa CCM, kura zinaanza kupigwa baada ya mpiga kura wa mwisho kuainisha matakwa yake na kuishia kwani ushindi huwa unapangwa mezani. Katika chaguzi ndogo kama nne zilizohusisha Bunge lililomaliza kipindi chake hivi NA MCHAKATO WA AWALI WA UCHAGUZI wa hivi karibuni tulijifunza yafuatayo:-

  A) CCM kwa kuelewa ukapa wa vyama vya upinzani wapo tayari kuwanunua mawakala wao ili wabariki matokeo ambayo CCM wanayataka. Upo ushahidi wa kutosha wa mawakala kuingia mitini hususani baada ya uchaguzi kufanyika. Mawakala hawa hawapo hata tayari kutoa taarifa au kupeleka fomu za matokeo kwa viongozi wao kwa uhakiki wa ziada!

  B) Katika kura za maoni za CCM zilizokwisha hivi punde tu tumejionea wenyewe rafu za waziwazi wagombea wakifanyiwa. Ngazi za juu zipo tayari kumzushia mtu siyo raia ili tu wampitishe mtu wao waliye na uhakika ni mbumbumbu ambaye baadaye atakuwa BW. au Bi. "YES" Bungeni. Kama CCM wapo tayari kufanyiana wao wenyewe unyama na hiyana je VYAMA VYA UPINZANI NA HUSUSANI CHADEMA SI WASUBIRI SHUBIRI TU?

  C) Katika kura za ubunge wa chaguzi ndogondogo tumeshuhudia mawakala wa vyama vya upinzani wakikithiri kwa kulalama ya kuwa hawakuwa wamelipwa haki zao na vyama vya upinzani pengine kuchochea ukosefu wa uzalendo kwa vyama vyao pale ambapo CCM wanawadobosha na mapesa wakati wa kuhesabu kura. Kama vyama vya upinzani, havikuwa na bajeti stahili ya kuwatuliza mawakala wao katika chaguzi ndogo je mahitaji ya bajeti ya malipo ya kuwalipa mawakala wote katika uchaguzi mkuu watahimili vishindo?

  D) Katika zoezi la kusaili wagombea tumejionea wenyewe jinsi viongozi wa halmashauri ambao ndiyo watendaji serikalini wanavyopewa madaraka na NEC isivyo halali kuwa makamisaa wa uchaguzi na jinsi wanavyozitumia nafasi hizo katika kuwang'oa wapinzani kwenye kinyang'anyiro na hivyo kuwanyima wapiga kura haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. Hali hii itachachamaa zaidi kwenye uchaguzi mkuu, kwa sababu NEC kwa makusudi mazima itaendelea kuwatumia vibosile wa halmashauri kama makamisaa!!!!!!!!!

  D) CCM imekuwa ikisaidiwa na misamaha haramu ya kodi inayozidi Bilioni 700 kwa mwaka hususani kwenye eneo la madini. Shehemu kubwa ya ulaji huu kazi yake kubwa siyo kusomesha watoto bure. La hasha. Siyo kutoa tiba bure . La hasha... bali ni kuwarubuni mawakala wa upinzani ili washinde chaguzi.

  E) CCM imewalipa waalimu tu nyongeza za mishahara kwa kuelewa ndiyo watakaohusika katika kuhesabu kura. Wafanyakazi wengine wa umma wametekelezwa kwa vile mchango wao zaidi ya kupiga kura ambazo CCM wana uhakika watazichakachua watakavyo unabezwa katika kufanikisha azma ya CCM ya ushindi wa Tsunami. Waalimu hawa ndiyo CCM inawategema wawatunzie siri ya uchakachuaji wa matokeo kwa vile kura zinahesabiwa kama njugu na wala siyo kwa kompyuta. Waalimu ambao pamoja na nyongeza ya mshahara kiduchu bado watawakarimu CCM ili wapate fungu la BINGO la ghafla siku ya kuhesabu kura......

  F) Kutokana na mapungufu ya NEC, CCM imechapisha au kupewa nakala za kutosha na NEC za fomu za kujaza matokeo wayatakayo. Ungefikiria ya kuwa taifa ambalo lisilo la "wahuni" fomu za kujaza matokeo ya uhesabuji wa kura zingekuwa zimetengenezwa kwa gharama kubwa ili kuzuia uchakachuaji lakini CCM na NEC wao kwa kuelewa wanachotaka kukifanya fomu hizo mtu yoyote tu aweza kuzichapisha na hivyo kutanua mianya ya uchakachuaji wa matokeo.

  G) Ikumbukwe baadhi ya wagombea wa Chadema wa ngazi za Ubunge na udiwani hawakuchekechwa vizuri. Kama zoezi hili lingekuwa limefanyika kwa umakini pasingekuwepo mgombea amabaye anachukua fomu na kuipeleka CCM ambako anakatiwa dau la TSHS milioni mbili kwa mgombea udiwani na kati ya milioni THS 15 hadi 30 kwa mgombea ubunge ili kuwaachia mawaziri watese bila upinzani na kuashiria kukubalika feki kwa wakubwa hao kwenye majimbo yao. Hali ya dhuluma hii kwa wapiga kura itashamiri zaidi siku ya kupiga kura. Aidha kuwanunua wagombea walioangusha isivyo halali na kinyume na sheria kwa minajili ya kuwazuia kwenda mahakamani au kuwanunua hata wanasheria ambao watawategemea wagombea atjwa katika kuwasaidia mahakamani kwa kuwadai fedha ambazo wanajua hawawezi kuwa nazo. Na mbinu nyingine chafu hata zaidi ya hizo ili mradi kuzima vuguvugu au kuzipooza za kutaka mabadiliko ya mfumo wetu wa uendeshaji wa Nchi hii.

  H) Ununuzi wa shahada za wapiga kura ambao CCM inauendesha Nchi nzima waashiria ya kuwa uchaguzi huu fedha ndizo zitamua CCM iendelee madarakani au hapana. Haya yote CCM inayafanya CCM ikielewa NEC iko upande wake. Aidha shahada hizo zitawazuia wapinzani kupiga kura au vilevile CCM itawatumia makada wake kuhakikisha inapiga kura mara mbilimbili. Yote haya ni dhuluma tu kwa Taifa hili.

  Kutokana na changamoto hizi mkakati wa Chadema wa kuhakikisha inaibuka kidedea ni huu hapa:-

  i) Hakikisha uteuzi wa mawakala unafanyika kwa uangalifu mkubwa ili kukwepa kupandikiziwa makada wa CCM ambao watasababisha kilio na kusaga meno.

  ii) Hakikisha bajeti ya kutosha ipo na malipo ya mawakala yanafanywa na makao makuu ya Chadema bila ya kuwaachia wagombea ambao wengi wao ni hohehae kiuchumi.

  iii) Kuanza kuchunguza uwezekano wa kisheria wa kuhesabu kura mara ya pili baada ya makamisaa kutangaza matokeo. Uhesabuji wa kura wa mara ya pili utakizima CCM milele. Na hapo tutaanza kuzungumzia utaratibu wa kisheria wa CCM kurudisha mali zote walizopora taifa hili ili zirudishwe kwa wamiliki halali: Wananchi. Baada ya hapo CCM kama ilivyo kwa Kanu hapo Kenya, UNIP kule Zambia na vyama vingine vilivyoleta uhuru kifo chao kitakuwa kimekamilika na taifa la pili la Tanzania litazaliwa.

  i) Kuhamasisha raia wote kujitokea saa za jioni kwenye vituo vyao vya kupiga kura ili kuhamasisha mawakala, kushinikiza na kuhakikisha haki itendeke na ionekane ikitendeka.

  Taifa la pili kuzaliwa kutaanza na siyo mara baada ya kuchimbwa kwa kaburi la CCM bali baada ya kuhakikisha hata mizimu yake yote ya CCM imefukiwa kilometa nzima ndani ya kaburi lake.

  AMA KWELI '"YOTE YAWEZEKANA BILA YA CCM"
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  hapa umesema mkuu
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Intelligent Contriibution!! Thank you!!
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mchango mzuri
   
 5. e

  emalau JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Don't be complacent, CCM are creative of all evil stuff, they might come out with something new !
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Uchakachuaji wa kura inabidi iwemo kwenye ilani yao
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  CCM the angel of death
   
 8. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona rafu zimefanyika hata huko CHADEMA na haichukuliwi kama kigezo cha kuiba kura kwenye uchaguzi mkuu?

  Uchaguzi wa 2005 mgombea wenu wa Urais alibariki matokeo na hata alishiriki sherehe za kutangaza matokeo na akaenda kumpongeza na kumkumbatia jukwaani huku wapinzani wengine wakisusia matokeo hayo. Sasa kitakachotokea ni kuwa nyie mtasusia na katika harakati za kulipiza kisasi wengine watahudhuria hizo sherehe halafu mje na hoja za kusadikika, kama kawaida yenu.
   
 9. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  We kibaraka wa CCM elewa kuwa 2005 na 2010 mabadiliko makubwa sana yametokea kwa watanzania, only majinga machache kama wewe yameshindwa kujiendeleza hata kielimu miaka hiyo mitano na kutoa tongotongo za imani ya kishirikina kuwa Tanzania bila thithiemu haiwezekani.... Wenzio tumebadilika na tunachagua CHADEMA na DK SLAA. Kikwete tunajua hatahudhuria kuapishwa kwa Dr Slaa, yeye atasusa laikini sie twalaaaa. Full ushindi 2010, Full mabadiliko Tanzania.
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu wajiandae kuleta wapatanishi hata marais jirani hawataweza labda aje Kofi Anan na Ban ki-Moon. Nimesha acha wosia nyumbani inawezekana siku ya kupiga kura yakawepo matanga na inawezekana wasinione milele. Take my words.
   
 11. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmebadilika baada ya kunywang'anywa ulaji ndani ya CCM na waakina Makamba. Siku zote mlikuwa mnaishangilia hiyo CCM lakini baada ya kupigwa mieleka huko ndiyo mnajifanya waut wa mageuzi na Slaa wenu.

  Yes mtaendelea kupata ushindi kwenye online forums lakini kwenye kura na hata midahalao kama ya jana mtabaki kuwa chama cha tatu tu.
   
 12. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni hivyo basi wapunguzie mzigo ndugu zako na ukachonge jeneza lako na ukalichimbe kaburi lako maana watu kama nyinyi ni wakupigwa virungu na mkong'oto tu.
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Nirudie kusema mara ngapi.
   
 14. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani uliporudia kwenye mjadala huu, ilikuwa mara ya ngapi? :becky:
   
 15. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  :mad2:
   
 16. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Naona sababu zishaazwa kutafutwa mapemaaa
   
 17. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nitakuwa wakala wa CHADEMA kwa gharama zangu mwenyewe..Nitalinda kura yangu na za wenzangu waliokipigia CHADEMA.
  Nitalinda kura za SLAA kwa niaba ya mzee wangu anayepata huduma mbovu za afya pamoja na kukatwa kamshahara kake kila mwezi kulipia kile kinachoitwa huduma ya afya wakati akienda hospitali anapewa panado na aspirin tu..anashindwa kujenga sababu cement iko juu ne kilichonikera zaidi ni pale CCM waliposema hawahitaji kura yake..Nawahakikishia HAKUNA HELA YA KUNININUA.
   
 18. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Badala ya kupoteza pesa kwenye gharama za Internet bora ungeenda kumtibia huyo mzee wako anayetibiwa kwa aspirin na panadol. Pia anaweza kujenga kutumia udongo, si unaona baba yake Slaa kajenga kwa udongo wa kawaida wala hakungojea cement? :becky:

  Hatudanganyiki lakini tunaendelea kudanganya kila siku :glasses-nerdy:
   
 19. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya ni mawazo yako na ninayaheshimu kama ninavyoyaheshimu mawazo ya wana jamvi wengine. ukweli kwamba mfumo wa bima ya afya wa sasa una mapungufu hilo liko wazi na huhitaji kubishana hapa katika hilo. ni jambo moja tu kati ya mengi ambayo hayatabadilika chini ya serikali hii. inawezekana ile kauli ya kuwa SIHONGEKI imekukasirisha sana, ila huo ndi ukweli safari hii hatudanganyiki
   
 20. D

  Dotori JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ...Mchango mzuri....Navishauri chama pinzani kuanza utaratibu wa kujenga mtandao toka chini.....
   
Loading...