CCM yatangaza kuachana na siasa za kibabe na kurudi kwenye siasa zake za asili za Upendo na Urafiki mwema!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,137
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amesema CCM haitajiingiza katika siasa za kibabe na visasi bali itajikita kwenye siasa zake za asili zilizosheheni Upendo na Urafiki.

Huu ni mwanzo mzuri sana kwa sekretarieti mpya ya CCM na vyama makini vya upinzani ikiwemo ACT wazalendo wamepongeza.

Kazi Iendelee!
 
Ubabe walikuwa wanamfanyia nani na kwa ulazima gani hadi wafikie huko na kwanini hawakutaka kufuata utaratibu wa kikanuni na sheria elekezi !?
Mbona hata CHADEMA walkuwa wababe, wakakutana na mbabe, wakaishiwa ubabe. Sahizi nawasikia wameanza tena kelele. Kale kadada ka Dodoma kaliongea sana siku ile. Hii ni baada ya mbabe wa siasa za kibabe kuchomoa rout.
 
Sidhani kauli hii yatosha kukisafisha chama hiki ambacho kina tuhuma lukuki nyingi zaidi ya hizo za kutesa, kuumiza, kupoteza watu na wizi wa kura uliotukuka.
 
Vipi kuhusu wahudumu waliondolewa kurudishwa makao makuu hajasema neno?
 
Dikteta magufuli wenzie wanadhidi kumkana kadri siku zinavyoenda,,

Mungu amtupe fiinali Jehanamu.
 
Kutojiingiza katika siasa za kibabe ni pamoja na kukubali kuanzisha TUME HURU YA UCHAGUZI, na kuondoa Sheria kandamizi za uchaguzi!

Wasipofanya hayo ni sawa na kumpigia Mbuzi gitaa ili akate kiuno kitu kischowezekana kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…