[FONT=courier
new]CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimejipanga kuhakikisha
wanarejesha majimbo yote kiliyoyapoteza katika uchaguzi mkuu ujao wa
mwaka 2015 kwa kuwa kimeshabaini sababu za kupoteza majimbo na kata
katika uchaguzi uliopita.[/FONT]
Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Katibu Mkuu
wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza kwenye kikao
maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilemela, jijini
hapa.
Tumeshagundua sababu za kupoteza baadhi ya
maeneo ni ugomvi tu baina yetu. Sasa tumekuja na kaulimbiu mpya ya
Umoja ni Ushindi, anayesubiri CCM ishindwe atazeeka sana bila kuona
hivyo, alisema.
Kwa kuwa kikao hicho kiliwashirikisha
watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela, Mwigulu alisema wapo watu
wanaoacha kuitumikia Serikali iliyopo madarakani wakidhani kuwa kuna
Serikali nyingine itaingia madarakani hivi karibuni.
Aliwataka viongozi wa CCM wasisite kuchukua
hatua na kukemea kwa kile wanachotaka kitekelezwe na watendaji kwa
mujibu wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.[FONT=courier
new]
[/FONT]
Waliopo Serikalini wanatekeleza mkataba wa
Serikali inayoongoza nchi, tukifuata hilo Tanzania tutapiga hatua na
tunapoisimamia Serikali hatupaswi kulaumiwa na mtu, kwani tunaisimamia
ilani ya CCM itekelezwe, alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa
CCM.
Nchemba alisema kinachoigharimu Tanzania ni
baada ya uchaguzi kumalizika, halafu watu kuanza uchaguzi mwingine
badala ya kuchapa kazi ya kuwatumikia
wananchi.
Uchaguzi ukiisha tujenge kasumba ya kuacha
kampeni na maandamano ya kila siku na kuingia kazini kuwatumikia
wananchi, si mmeona wenyewe baada ya uchaguzi wa Marekani kumalizika
watu wanafanya kazi na sio kuzungumzia uchaguzi tena,
alisema.
Haiwezekani siku zote ziwe za kampeni.
Tutafanya lini kazi, siku zote kuwa za kampeni zinawafanya watumishi wa
serikali kushindwa kugawa muda wa kuwatumikia wananchi?
Alihoji.
Katika kikao hicho maalumu, Nchemba aliwagawia
wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya makabrasha ya maazimio ya
Mkutano Mkuu wa Nane wa Taifa na Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,
Jakaya Kikwete, kama vitendea kazi vyao.
Chanzo: HabariLeo | Imeandikwa na Grace Chilongola,
Mwanza | Jumapili, 23 Desemba 2012