CCM yasitisha kikao chake cha NEC

Facts1

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Messages
308
Points
0

Facts1

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2009
308 0
Chama cha Mapinduzi CCM kimeahirisha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, kilichotarajiwa kufanyika mwezi huu mjini Dodoma, kwa ajili ya utekelezaji wa dhana ya kuvuana magamba, inayowalenga makada wawili, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Duru za siasa kutoka ndani ya CCM zinasema kikao hicho kinaweza kumezwa pia na matokeo ya uchaguzi wa Igunga, kwa kutegemea kama CCM kinashinda au kinashindwa.

Wachambuzi wa siasa wanasema kama CCM itaibuka kidedea, utakuwa wakati mgumu kwa chama hicho kuendelea kuwatuhumu makada wanaoitwa mafisadi, maana kimelazimika kumtumia Rais Kikwete kumpigia magoti mmoja wao, Rostam Azizi, ili akisaidie kushinda.

Na kama kitashindwa, makada wanaorusha tuhuma dhidi ya mafisadi, watapata wakati mgumu kwa kuwa ndio waliosababisha Rostam kujiuzulu ubunge wa Igunga na kushindwa kwa CCM kutaonyesha nguvu ya watu walewale wanaosemekana wanakichafua chama.

Hata kauli za Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kumsifia Rostam katika mkutano wa uzinduzi wiki iliyopita, ni kitanzi kingine kwa CCM inayojidai inawatosa kina Rostam kwa ufisadi wao.

Tanzania Daima
 

Dumelambegu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
1,052
Points
0

Dumelambegu

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
1,052 0
Tangu wakati Kolimba aliposema chama kimepoteza mwelekeo yaani hakina dira mpaka leo madudu ni yaleyale. Tena basi bora hata wakati huo kuliko leo ambapo majambazi maarufu wa nchi hii wapo ndani ya chama wanapigiwa magoti kama wafalme. Shiiiiiiitt!!!!!
 

Bigirita

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
15,822
Points
2,000

Bigirita

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
15,822 2,000
Kwa hiyo amekula n'ke wa kada mwenzake?
Yeye hakwenda na n'ke wake kwenye kampeni?
Au ndo utaratibu wao wa kutafuna wake wa wenzao kwenye kampeni!!
 

Gagnija

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2006
Messages
7,629
Points
2,000

Gagnija

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2006
7,629 2,000
Either way, CCM inakwenda kuanguka. Bila shaka Nape atakuwa amepata sababu za kuachana na chama hicho kama kitashindwa kutekeleza maazimio kiliyopitisha. Tatizo ni nani atoke na nani abaki, maana kama alivyosema Sofia Simba, hakuna msafi huko.
 

Forum statistics

Threads 1,389,991
Members 528,065
Posts 34,040,508
Top