CCM yasitisha kikao chake cha NEC

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Chama cha Mapinduzi CCM kimeahirisha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, kilichotarajiwa kufanyika mwezi huu mjini Dodoma, kwa ajili ya utekelezaji wa dhana ya kuvuana magamba, inayowalenga makada wawili, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Duru za siasa kutoka ndani ya CCM zinasema kikao hicho kinaweza kumezwa pia na matokeo ya uchaguzi wa Igunga, kwa kutegemea kama CCM kinashinda au kinashindwa.

Wachambuzi wa siasa wanasema kama CCM itaibuka kidedea, utakuwa wakati mgumu kwa chama hicho kuendelea kuwatuhumu makada wanaoitwa mafisadi, maana kimelazimika kumtumia Rais Kikwete kumpigia magoti mmoja wao, Rostam Azizi, ili akisaidie kushinda.

Na kama kitashindwa, makada wanaorusha tuhuma dhidi ya mafisadi, watapata wakati mgumu kwa kuwa ndio waliosababisha Rostam kujiuzulu ubunge wa Igunga na kushindwa kwa CCM kutaonyesha nguvu ya watu walewale wanaosemekana wanakichafua chama.

Hata kauli za Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kumsifia Rostam katika mkutano wa uzinduzi wiki iliyopita, ni kitanzi kingine kwa CCM inayojidai inawatosa kina Rostam kwa ufisadi wao.

Tanzania Daima
 
CCM hawana kitanzi, watatafuta mlango wakutokea ktk hili suala ila NAPE imekula kwake hakuna atakaye jivua gamba hapa zaidi ya RA
 
watabadilika sana lakini tumeshajua uhuni wao ndio hapo watakapo jua tz ni ya 1970 au ni yakizazi kipya?
 
Tangu wakati Kolimba aliposema chama kimepoteza mwelekeo yaani hakina dira mpaka leo madudu ni yaleyale. Tena basi bora hata wakati huo kuliko leo ambapo majambazi maarufu wa nchi hii wapo ndani ya chama wanapigiwa magoti kama wafalme. Shiiiiiiitt!!!!!
 
Mwigulu asemekana KUTIMUA VUMBI na NGUO YA NDANI ya mke wa Kada mwenzie, Raajabu, pale alipofumaniwa kwenye EVENT kwenye mojawapo Mi-Guesi kibado Igunga ambako CHADEMA walinyimwa haki ya malazi kama wateja wengine.

Kwani Mwigulu amekwisha chukua mke mwingine wa watu?
 
KUMBE! NI MWIGULU NCHEMBA. MWIGULU NCHEMBA, KATIBU WA FEDHA NA UCHUMI CCM(nec), NDIO KAMCHUKUA MKE WA MTU NA KUSABABISHA MTAFARUKU NA HATIMAYE KUIMBA NGUO YA NDANI A.K.A chupi. Jamani!
 
Kwa hiyo amekula n'ke wa kada mwenzake?
Yeye hakwenda na n'ke wake kwenye kampeni?
Au ndo utaratibu wao wa kutafuna wake wa wenzao kwenye kampeni!!
 
Wazee wazamani kina Kolimba walikuwa na mtazamo wa mbaliiiiiiii sana
unajua ukweli unauma lakini ni bora ukiambiwa uufanyie kazis
 
Either way, CCM inakwenda kuanguka. Bila shaka Nape atakuwa amepata sababu za kuachana na chama hicho kama kitashindwa kutekeleza maazimio kiliyopitisha. Tatizo ni nani atoke na nani abaki, maana kama alivyosema Sofia Simba, hakuna msafi huko.
 
Back
Top Bottom