Facts1
JF-Expert Member
- Dec 23, 2009
- 307
- 28
Chama cha Mapinduzi CCM kimeahirisha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, kilichotarajiwa kufanyika mwezi huu mjini Dodoma, kwa ajili ya utekelezaji wa dhana ya kuvuana magamba, inayowalenga makada wawili, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Duru za siasa kutoka ndani ya CCM zinasema kikao hicho kinaweza kumezwa pia na matokeo ya uchaguzi wa Igunga, kwa kutegemea kama CCM kinashinda au kinashindwa.
Wachambuzi wa siasa wanasema kama CCM itaibuka kidedea, utakuwa wakati mgumu kwa chama hicho kuendelea kuwatuhumu makada wanaoitwa mafisadi, maana kimelazimika kumtumia Rais Kikwete kumpigia magoti mmoja wao, Rostam Azizi, ili akisaidie kushinda.
Na kama kitashindwa, makada wanaorusha tuhuma dhidi ya mafisadi, watapata wakati mgumu kwa kuwa ndio waliosababisha Rostam kujiuzulu ubunge wa Igunga na kushindwa kwa CCM kutaonyesha nguvu ya watu walewale wanaosemekana wanakichafua chama.
Hata kauli za Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kumsifia Rostam katika mkutano wa uzinduzi wiki iliyopita, ni kitanzi kingine kwa CCM inayojidai inawatosa kina Rostam kwa ufisadi wao.
Tanzania Daima