CCM yashtushwa na wingi wa wanahabari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yashtushwa na wingi wa wanahabari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 29, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  CCM yashtushwa na wingi wa wanahabari

  na Edward Ibabila, Musoma
  Tanzania daima~Sauti ya Watu

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeshtushwa na wingi wa waandishi wa habari waliofika mkoani hapa kwa lengo la kuandika habari za kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kinachoanza leo kijijini Butiama.

  Kushtushwa kwa chama hicho kulibainishwa jana na Ofisa Habari na Mawasiliano wa CCM Makao Makuu, Gabriel Athuman, alipozungumza na waandishi wa habari jinsi ya ushiriki wa vyombo hivyo katika kikao hicho.

  “Ndugu zangu chama kimeshtushwa na wingi wenu, hasa ukizingatia kuwa mmeandika sana juu ya kikao hiki hata kabla ya kikao kuanza…inawezekana mnayoandika ni ya kweli au pengine si ya kweli. Hivyo basi mtashiriki, lakini kwa utaratibu maalum,” alisema.

  Akitangaza utaratibu wa ushiriki wa vyombo vya habari katika kikao hicho, Athuman alisema waandishi wote hawataruhusiwa kuwa kwenye kikao hicho, lakini watasubiri taarifa ya maazimio katika siku ya mwisho Machi 30, mwaka huu.

  Aidha, alisema waandishi wote watakuwa na vitambulisho maalum na kuwa kila chombo cha habari kitajitegemea kwa usafiri na mahitaji mengine.

  Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Yusufu Makamba, alitoa sh 100,000 kwa ajili ya usafiri wa waandishi hao wa habari.  Maoni ya Wasomaji
  Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
  Maoni 6 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
  Kama kawaida yake makamba anawafanya watu wote wapumbavu niliwahi kutowa maoni yangu wakati fulani kuhusiana na huyu Makamba alipokwenda akawambia maneno machafu wandishiwa habari na wapiga picha nayaita maneno machafu kwasababu mtu mzima kama yeye kuwa waeleza watu wenye heshima zao na kazi zao zinazosaidia jamii na Taifa kwa ujumla kuwa haya pigeni picha halafu muondoke ni utovu wa adabu na leo anawatukana kistarabu kwa kutowa pesa eti kwa ajili ya safari za wandishi nakama wandishi watazitumia kwa safari hiyo basi watakuwa wao ndio wamejikubalisha kuwa wapumbavu wa hali ya mwisho kabisa.Tukumbuke kuwa Kuna wakati Rais KAMBARAGE alisema ikiwa mtu atakwambia mambo ya kipumbavu na wewe ukayakubali basi ni wewe uliyoyakubali ndio Mpumbavu na hiyo ndio njia anayoitumia Makamba kuwafanya watu wote wapumbavu. Makamba usijidanganye Tunaishi katika maleniam mpya

  na Andrew, Tanzania, - 29.03.08 @ 12:03 | #4036

  sasa CCM munaogopa nini? Au kuna siri huko hamutaki itoke nje?

  na Kirambo, musoma, - 29.03.08 @ 13:08 | #4046

  wanataka kujadiliana namna ya kuficha mambo yao ktk EPA namba mbili maana namba moja watu wamewashtukia.watanzania tuwe macho tuhakikishe kona zote zinalindwa wasituingize mkenge hao

  na kamwene - 29.03.08 @ 16:54 | #4064

  Wakati wa kampeni za kugombea urais 2005 CCM hamkushtushwa na wingi wa waandishi wa habari!!! Mmesahau jinsi mlivyokuwa mnawanunua na kuwagharimia kila kitu ili habari zanu ziandikwe! Leo kwa vile waandishi wanaandika uozo wenu na jinsi mnavyo ikuza na kuisujudu rushwa basi imekuwa nongwa na mnawashangaa.

  Siku isiyo na jina inakuja Mungu atawatujalia Watanganyika tuweze kuyafahamu makosa tunayoendelea kuyafanya ya kuipa kula CCM. Ndipo Mhe. Makamba tutakapo kutana pale Maheza-nguu Korogwe akiwa anakumbuka enzi za ufalme wao.

  na Jackson, London, - 29.03.08 @ 17:16 | #4065

  Paukwa, pakawa! fisadi wa EPA angejenga barabara ingekuwa ya kilomita ngapi? ohhhhh halo halo! EPA type of plundering and squandering public money is the vivid cause of our Poverty! but most important CCM is growing blind because of old age? No hypocrisy! It is high time you know it because our economy is downing, but still you fool us otherwise. No Economy should be a national interest and not political hypocrisy.

  na Majaliwa, Musoma, - 29.03.08 @ 18:10 | #4069

  Paukwa, pakawa! fisadi wa EPA angejenga barabara ingekuwa ya kilomita ngapi? ohhhhh halo halo! EPA type of plundering and squandering public money is the vivid cause of our Poverty! but most important CCM is growing blind because of old age? No, hypocrisy! It is high time you know it because our economy is downing, but still you fool us otherwise. No, Economy should be a national interest and not political hypocrisy.

  na Majaliwa, Musoma, - 29.03.08 @ 18:14 | #4072
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nadhani wamejitokeza CCM iwaone na mjue nani wa kumnunua wakati mkiwahitaji kwa ajili yenu leo wapo kwa ajili ya Watanzania mnaogopa kitu gani ?
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kamanda, mimi ningependa kujua umuhimu wa kukopi maoni ya hao wachangiaji katika hilo gazeti na kuyaleta hapa...
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Uone wengine wanasema nini ambao hawajatokea JF maana mnadhani JF ni anti CCM mnashindwa kujua kwamba CCM ina breed maadui kwa matendo yake yenyewe .Beside nilitegea ulalie hoja ya gazetini zaidi kuliko ku hoji uhalali wa wachangiaji ama umaana wao .
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Tatizo liko wapi, kwani hutaki kusikia Watanzania wengine wana maoni gani kuhusu yanayojiri ndani ya nchi yetu!? :confused:
  Lini ulichaguliwa hapa JF kuamua kipi kinastahili kutumwa hapa na kipi hakistahili!? :confused:
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Well said Lunyungu.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Yeye ajadili hoja iliyo mezani na si kuhoji mawazo ya wengine
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hakuna tatizo Kamanda... ni vema kujua na wengine wanasemaje kuhusu yachapishayo kwenye magazeti....
   
Loading...