CCM yasalimu amri Zanzibar

Kwa hiyo unanishauri nika balance story na gazeti la Uhuru?

Mahaba hupunguza uwezo wa fikiri, mahaba hufanya vipofu wakaona kwa muda, kwa maana nyingine tujifunze kusoma na kuona tusivyovitaka au kuvitarajia.
 
Nafikiri kwa mujibu wa gazeti la serikali, tunachosubiri sasa hivi ni kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi tu kwa vile kikatiba tayari uchaguzi umeshafutwa rasmi.

Nani ---- wewe atakapiga kura don't be a stupid like ur fellows ccm
 
Kwa jinsi CCM inavyopenda madaraka, si rahisi kwa unayoyasama. CCM inaamini haki ya kutawala ni yake tu. Ipo tayari hata kufanya llolote kumbuka mauaji ya 2001.

Habari,

Ninazoendelea kuvuja kutoka ndani ya kikao kilichoketi Jumatatu hii na kuhusisha marais wastaafu Mh.Mwinyi, Mh. A. Karume, rais wa Zanzibar Dr. Shein, Balozi Seif na Maalim Seif, zinasema chama cha Mapinduzi Zanzibar kimekubali kuachia madaraka.

"Kilichobaki ni kustahimili kushirikiana na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa" alisema mmoja wa wawakilishi kutoka CCM.

Habari zaidi kutoka CCM Lumumba zinasema "hatuwezi kuendelea kupigania kitu ambacho kimeshatutoka. Haya tuache tusonge mbele, kwani dunia nzima inatushangaa."
 
Habari yako inapingana na habari iliyopo kwenye gazeti la serikali,acha uongo lete habari za kueleweka JF inaheshimika zaidi ya vyombo vyote vya habari unavovijua wewe.

Huu ni uongo uliotukuka ,vyombo vyote vya habari ??? Sasa imekuaje ukaamini gazeti la serikali na usiamini kilicholetwa hapa jamvini ??
 
Mahaba hupunguza uwezo wa fikiri, mahaba hufanya vipofu wakaona kwa muda, kwa maana nyingine tujifunze kusoma na kuona tusivyovitaka au kuvitarajia.
Unachekesha sana unanishauri nisome nisivyovitaka wakati wewe unaidharau source ya Mawio.
 
Nafikiri kwa mujibu wa gazeti la serikali, tunachosubiri sasa hivi ni kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi tu kwa vile kikatiba tayari uchaguzi umeshafutwa rasmi.

Kwa kuwa Jamii Forums ni sehemu ya Facts na siyo kupindishapindisha mambo, ni vema kwa manufaa ya Umma, ukaweka hivyo vifungu vya Sheria ndani ya Katiba,kusema tu kama kasuku bila hata kuongeza nyama ya vifungu husika haina tija sana!
 
Nani ---- wewe atakapiga kura don't be a stupid like ur fellows ccm

Hapakua na sababu ya kutumia nguvu nyingi kiasi hicho, kwanza naomba utambue kwamba mimi sio mwanachama wa ccm na sitarajii kuja kujiunga na ccm. Pili kuna vitu ni sheria kikatiba siwezi kuvibadili hata kama sivitaki au sivipendi.
Mfano, mshindi wa urais akishatangazwa na tume hairuhusiwi kuhojiwa na chombo chochote, si pendi na wala siridhiki na ukweli huo lakini kwa vile ndio sheria iliyopo siwezi kubadili hilo.

Hapo nilichokielezea ni kwamba, kama gazeti la serikali limeshatangaza rasmi kufuta uchaguzi ina maana hakuna namna unaweza tena kutumia matokeo ya uchaguzi uliopita kumalizia mchakato wa kumpata mshindi wa urais. Ina maana zoezi lazima lianze upya, na hiyo ni kwa mujibu wa sheria zilizopo vinginevyo watengue huo utaratibu.Ni kweli mimi sio mjinga na wala sio mwana ccm!
 
Kama huyo Maalim Seif ameshinda uchaguzi wa Zanzibar inabidi tu atangazwe mshindi.
Hayo yaliyofanywa na Jecha ya kufuta uchaguzi ni ushereshaji tu wa shughuli kama ambavyo hufanywa na maMC.
 
Hapakua na sababu ya kutumia nguvu nyingi kiasi hicho, kwanza naomba utambue kwamba mimi sio mwanachama wa ccm na sitarajii kuja kujiunga na ccm. Pili kuna vitu ni sheria kikatiba siwezi kuvibadili hata kama sivitaki au sivipendi.
Mfano, mshindi wa urais akishatangazwa na tume hairuhusiwi kuhojiwa na chombo chochote, si pendi na wala siridhiki na ukweli huo lakini kwa vile ndio sheria iliyopo siwezi kubadili hilo.

Hapo nilichokielezea ni kwamba, kama gazeti la serikali limeshatangaza rasmi kufuta uchaguzi ina maana hakuna namna unaweza tena kutumia matokeo ya uchaguzi uliopita kumalizia mchakato wa kumpata mshindi wa urais. Ina maana zoezi lazima lianze upya, na hiyo ni kwa mujibu wa sheria zilizopo vinginevyo watengue huo utaratibu.Ni kweli mimi sio mjinga na wala sio mwana ccm!

WEWE KUMBE HUJAMSIKIA HUYU X MWANASHERIA MKUU ANASEMA KITU GANI KUHUSU HAYO ULIYOYAANDIKA

MSIKILIZE KJWA UTULIVU HAPA https://www.youtube.com/watch?v=hNoSZggJ_Ag
 
Zanzibar hawaendi kokote, watu wanaota, mtakuja kuona kitakachotokea. Uchaguzi utafanyika baada ya miezi mitatu full stop. People should grow up Tanzania haikuota kama uyoga.

Mataifa ya nje ambayo wapatishi na kutuma ujumbe wao,ikiwa uchaguzi unatakiwa urudiwe lazima wasimamie wao,Suala hilo ccm hawataki na wanajua kuwa hawatapata jimbo hata moja, katika vikao vya ccm muakilishi wa kikwajuni aliwaambia wenziwe kuwa anajua yeye alicho fanya hadi kupata jimbo, hata balozi Seif Ali Iddi anajua kwenye uchaguzi hivyo kurudi kwenye uchaguzi ni kuanguka tena chali

Ccm kulikuwa na makundi mawili, moja likitaka uchaguzi urudiwe na moja hapana, ndio ukaona huku unaona habari kwenye magazeti na huku mazungumzo yanaendelea kwa viongozi wa juu.

Kuna taarifa za ndani kuwa Seiff Ali Iddi viongozi wenzake wametaka asipewe uwongozi wowote kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa.
 
WEWE KUMBE HUJAMSIKIA HUYU X MWANASHERIA MKUU ANASEMA KITU GANI KUHUSU HAYO ULIYOYAANDIKA

MSIKILIZE KJWA UTULIVU HAPA https://www.youtube.com/watch?v=hNoSZggJ_Ag

Nimekusoma vizuri sana mkuu. Hapa hii kutapatapa kote ni kwa sababu tumetoka kwenye hoja. Suluhu inayotafutwa hapa haina nia njema mkuu. Ndio maana watu wanaokoteza sheria ili kuhalalisha matakwa yao. Msingi unabaki palepale, turudi kwenye HOJA ya msingi kwamba Mwenyekiti wa ZEC kavunja taratibu na sheria!

Hili jambo ni zito kuliko wanavyofikiria.
 
Back
Top Bottom