CCM yasalimu amri Zanzibar

CCM yasalimu amri Zanzibar

Habari,

Ninazoendelea kuvuja kutoka ndani ya kikao kilichoketi Jumatatu hii na kuhusisha marais wastaafu Mh.Mwinyi, Mh. A. Karume, rais wa Zanzibar Dr. Shein, Balozi Seif na Maalim Seif, zinasema chama cha Mapinduzi Zanzibar kimekubali kuachia madaraka.

"Kilichobaki ni kustahimili kushirikiana na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa" alisema mmoja wa wawakilishi kutoka CCM.

Habari zaidi kutoka CCM Lumumba zinasema "hatuwezi kuendelea kupigania kitu ambacho kimeshatutoka. Haya tuache tusonge mbele, kwani dunia nzima inatushangaa."
Kujifariji kama hivi ni vizuri kwa kuwa unaimarisha afya yako
 
Nafikiri kwa mujibu wa gazeti la serikali, tunachosubiri sasa hivi ni kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi tu kwa vile kikatiba tayari uchaguzi umeshafutwa rasmi.
 
Umefutwa kwa kutumia sheria ipi ya uchaguzi au kwa sheria ya magazeti.
 
Habari yako inapingana na habari iliyopo kwenye gazeti la serikali,acha uongo lete habari za kueleweka JF inaheshimika zaidi ya vyombo vyote vya habari unavovijua wewe.

Serikali ipi na muda wake uliisha tarehe2 nov
 
Wacha utani we. Umeshasahau ya Bi Asha Bakari kwenay BMK? "Hatuitoi, hatuitoi, hatuitoiiii. Ilipatikana kwa bunduki na hatuwezi kuitoa kwa karatasi" Hiyo ndo sera ya CCM!!

Niliwahi isikia hiyo clip nikiwa pale airport ya zanzibar, kwa kweli nilishangaa sana na.nikauliza nani aliwahi sema hivyo, wakasema ni huyo mama mvuta sigara ka gari moshi, ile kauli ni ya uchochezi kabisa kwa mama kama yule kuisema
 
Naombeni kuuliza kwanini muungano wa TANU na Afro-Shiraz Party (ASP) uliitwa Chama cha Mapinduzi????? mbona sioni correlation yoyote?
 
Tangazo kwenye gazeti la serikali lilitoka kabla ya Kikao cha j3 na j4. Na hilo tangazo ndo lilifanya wakutane.
 
Habari,

Ninazoendelea kuvuja kutoka ndani ya kikao kilichoketi Jumatatu hii na kuhusisha marais wastaafu Mh.Mwinyi, Mh. A. Karume, rais wa Zanzibar Dr. Shein, Balozi Seif na Maalim Seif, zinasema chama cha Mapinduzi Zanzibar kimekubali kuachia madaraka.

"Kilichobaki ni kustahimili kushirikiana na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa" alisema mmoja wa wawakilishi kutoka CCM.

Habari zaidi kutoka CCM Lumumba zinasema "hatuwezi kuendelea kupigania kitu ambacho kimeshatutoka. Haya tuache tusonge mbele, kwani dunia nzima inatushangaa."
Walisema wenyewe wajuvi, nchi iliyopatikana kwa mapinduzi haiachiwi kwa karatasi!!!!
 
Habari yako inapingana na habari iliyopo kwenye gazeti la serikali,acha uongo lete habari za kueleweka JF inaheshimika zaidi ya vyombo vyote vya habari unavovijua wewe.

tumuhesabie siku huyo uzushi wake sasa hivi ataungana na wenzie
 
Ukiendekeza woga wa kijinga huwezi pata maendeleo kamwe.

attachment.php
 
Habari,

Ninazoendelea kuvuja kutoka ndani ya kikao kilichoketi Jumatatu hii na kuhusisha marais wastaafu Mh.Mwinyi, Mh. A. Karume, rais wa Zanzibar Dr. Shein, Balozi Seif na Maalim Seif, zinasema chama cha Mapinduzi Zanzibar kimekubali kuachia madaraka.

"Kilichobaki ni kustahimili kushirikiana na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa" alisema mmoja wa wawakilishi kutoka CCM.

Habari zaidi kutoka CCM Lumumba zinasema "hatuwezi kuendelea kupigania kitu ambacho kimeshatutoka. Haya tuache tusonge mbele, kwani dunia nzima inatushangaa."

Kumbe gazeti la Mawio, , , , hili gazeti inabidi uwenalo makini sana siku hizi lina habari za udaku. Changanyeni na zakwenu pia mtafute ulinganifu kutoka vyanzo vingine vya habari.
 
Zanzibar hawaendi kokote, watu wanaota, mtakuja kuona kitakachotokea. Uchaguzi utafanyika baada ya miezi mitatu full stop. People should grow up Tanzania haikuota kama uyoga.
 
Wacha utani we. Umeshasahau ya Bi Asha Bakari kwenay BMK? "Hatuitoi, hatuitoi, hatuitoiiii. Ilipatikana kwa bunduki na hatuwezi kuitoa kwa karatasi" Hiyo ndo sera ya CCM!!
Hawezi kukubali kuufyata ..
Huyu bibi Ana maneno makali
 
Kumbe gazeti la Mawio, , , , hili gazeti inabidi uwenalo makini sana siku hizi lina habari za udaku. Changanyeni na zakwenu pia mtafute ulinganifu kutoka vyanzo vingine vya habari.
Kwa hiyo unanishauri nika balance story na gazeti la Uhuru?
 
kuna tetesi kwamba zanzibar tangu mfumo wa vyama vingi uanze ccm haijawahi kushinda uchaguzi kamwe....
 
Back
Top Bottom