CCM yapokea kwa mshtuko taarifa ya ajali mbaya ya Wasanii Belle 9 na Bonge la Nyau, yawatakia uponyaji wa haraka!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,012
142,046
Mwenezi wa CCM komredi Polepole amesema chama kimepokea kwa mshtuko taarifa ya ajali mbaya iliyowahusisha Wasanii Belle 9 na Bonge la nyau.

Polepole amewatakia uponyaji wa haraka na kwamba chama kinafuatilia kwa karibu tukio na chanzo cha ajali hiyo.

Source Ayo tv

Maendeleo hayana vyama!

===
Wasanii Lulu Diva, Belle 9 na Bonge la Nyau wamepata ajali ya gari alfajiri ya Septemba 07, Chalinze Pwani safarini kuelekea Dar, Lulu amethibisha na kusema “Nimeumia kichwani nimevimba ila Belle 9 kaumia zaidi amewaishwa Hosp. Bonge la Nyau kaumia ila kiasi”

1599458717678.png

PIA SOMA:
- Polepole atangaza CCM kusimamia matibabu ya Wasanii waliopata ajali
 
Bwashee jaribu kuwa na utu japo kidogo!
Bwashee Kumbuka Neno la Jana Kanisani, Somo la Kwanza

Eze. 33:7-9

Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu.

Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako

My take

Nitawaambia Ukweli law Sababu sitaki Mungu aje kuidai Damu yenu Mikononi Mwangu.
Nataka kuikoa Roho Yangu
 
Ajali mbaya za awamu hii ya CCM haziwezi kumuacha mtu salama. Watuambie hiyo ajali mbaya iliyowasalimisha wameipataje???
 
CCM ikifuatilia kwa karibu chanzo cha ajali, itabadilisha nini?
 
"Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau, tunafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wanapata huduma ya matibabu haraka na tunamwomba Mungu awape wepesi na kupona haraka”-Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM CCM Humphrey Polepole ameandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya kuripotiwa kuwa wasanii watatu wamepata ajali hii leo wakitokea mkoani Iringa.

Habari Star TV Tanzania

Kutumia Ajali za Watu kama tiketi yako ya 'Kujiimarisha' zaidi 'Kisiasa' inaweza ikawa ni sehemu Kuu ya Kuonyesha 'Udhaifu' wako wa Kifikra kuliko ambavyo pengine umetegemea. Je, kwa mfano Watu wakisema kuwa hiyo Ajali 'imetengenezwa' nanyi 'Kiuchawi' ili mjipatie 'Political Mileage' katika Kipindi hiki cha Kampeni mtawalaumu?

Sasa kwakuwa mmeonyesha Upendo kwa hawa 'Wasanii' nawaombeni ili niamini mna Upendo kwa Watanzania hebu 'Kalipieni' upesi sana 'Bills' za 'Wagonjwa wote wasio na Uwezo wa 'Kulipia' katika Hospitali zetu Kubwa nchini Tanzania. Mkimaliza hapo lipieni pia na 'Bills' za walioshindwa 'Kulipia' Maiti zao Hospitalini nchi nzima.

Najua na nina Uhakika 'Nitachukiwa' sana tu ila mtanisamehe katika Maisha yangu 'Msamiati' wa 'Unafiki' na 'Kujipendekeza' haupo. Tuvumiliane tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom