GE2025 CCM yapitisha Wagombea 208 wa Udiwani Dodoma kwa Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 CCM yapitisha Wagombea 208 wa Udiwani Dodoma kwa Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Jumla ya wagombea 208 kati ya 209 wa nafasi ya udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma waliopata ushindi kwenye kura za maoni, wamepitishwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao.

Hata hivyo, mgombea mmoja wa Kata ya Ihumwa jijini Dodoma, ameondolewa kwenye orodha hiyo na nafasi yake kupewa aliyeshika nafasi ya pili, kutokana na sababu za kimaadili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Agosti 13, 2025, Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi wa chama hicho, Jawadu Mohammed amesema uamuzi huo umechukuliwa ili kuendana na matakwa ya wanachama na kanuni za chama.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Mkoa wa Dodoma una jumla ya kata 209 na wagombea wote walioongoza kwenye kura za maoni wamepitishwa na Halmashauri Kuu ya mkoa, isipokuwa Kata ya Ihumwa. Huyu jina lake halijarudi na nafasi yake amepewa aliyeshika nafasi ya pili kwa sababu za kimaadili, kikanuni na kutokana na maoni ya watu wengi kuwa hapaswi kukiwakilisha chama kugombea nafasi hiyo,” amesema Jawadu.
 
Back
Top Bottom