Ccm yapiga mkwara wabunge waropokaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm yapiga mkwara wabunge waropokaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babukijana, Aug 20, 2009.

 1. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  MAAMUZI yaliyopitishwa wiki hii na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuwadhibiti wanachama, hususani Wabunge wake ambao wamekuwa msitari wa mbele katika kukipaka matope chama hicho, yanahitaji kupongezwa kwa nguvu zote na wanachama wengine wote walio na nia ya kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuiongoza nchi yetu. Wabunge na wanachama hao wamekuwa msitari wa mbele katika kuendeleza makelele ya wapinzani kuhusiana na vitendo vya ufisadi vya watu wachache walio ndani ya chama hicho, bila kujua kwamba chama kina mikakati gani ya kupambana na watu hao ambao wamekwenda kinyume na maadili yake!

  Wamesahau kabisa kwamba cha kuandamwa hapa ni watu wenyewe binafsi na si sera au mfumo wa CCM ambao unajulikana kabisa katika kupiga vita uovu wowote ndani ya chama na katika jamii ambayo inaongozwa na serikali yake.

  Kwa kifupi, wanachama hao wamekuwa wakinyea kwenye mkeka ambao wanaulalia na ambao wataendelea kuulalia!

  Katika mazingira ya sasa ambayo ni ya ushindani wa kisiasa, ni bora wanachama wa CCM wakatambua mfumo uliopo unaotumiwa katika kukosoana miongoni mwa wanachama wake. Na watambue kwamba katika mfumo wa vyama vingi, siasa imekuwa sawa na soko huria. Soko huria kwa maana kwamba vyama vina sera zake na namna ya kuendesha si mapambano yake tu bali na namna ya kujihami.

  Hivyo, Wabunge wa CCM na wanachama wengine ambao wamekuwa wakiiyumbisha serikali yao kwa makusudi au bila kujua, wafahamu wamekuwa wakifanya hivyo kwa faida ya vyama vya upinzani na kwa hasara ya CCM!

  Tabia ya kusema hadharani kauli zenye kukivunjia hadhi chama chao – badala ya vikao husika vyenye lengo la kukosoana na kuwekana sawa – ni ukiukaji wa kanuni zinazoongoza nidhamu ya chama, hulka ambayo ikiachwa kuendelea, itakiangamiza chama.

  Ikumbukwe kwamba CCM ndicho kilichowafikisha mahali walipo watu ambao wanakishambulia kutoka ndani yake. Na pia lazima wafahamu kwamba hakuna chama au kikundi chochote ambacho wanachama wake hawana dhambi au madhambi yoyote!

  Pia ni muhimu kufahamu kwamba chama ni kama familia moja ambayo ina kiongozi wake na mfumo maalum wa kutatua matatizo yake.

  Ni tabia mbaya ndugu wa familia moja kusaidia kufichua siri au matatizo ya ndani ya familia, hata kama watu wa nje tayari wanayaelewa. Kufanya hivyo, ni kuidhalilisha zaidi familia, na anayefanya hivyo lazima afahamu anajidhalilisha na yeye pia kwani ni lazima atakuwa ameshiriki kwa namna fulani katika kuibuka kwa matatizo ya familia hiyo.

  Na dawa ya kumaliza matatizo ya ndani ya familia, ni kwa familia yenyewe kukaa na kuyajadili na kuyapatia mwafaka badala ya kuwasaidia watu wa nje kuyafahamu zaidi, kwani maadui zao wanaweza kuyatumia kuifarakanisha zaidi familia hiyo.

  Kwa kweli, kitendo cha kuwaunga mkono wapinzani katika kukipiga vita Chama Cha Mapinduzi ni usaliti wa wazi wa kutoa siri za matatizo ya familia kwa watu wa nje.

  Kitu muhimu kwa kila mwanachama wa CCM ni kufahamu kwamba kutoa siri yoyote ya ndani na kuipeleka mitaani ni jambo la madhara makubwa kwani likikosa ufumbuzi kwa kuzidiwa na fedheha matokeo yake ni kufarakanika kwa familia.

  Jambo la kuzingatia ni kwamba kama kweli wanachama wa CCM wanaamini kwamba kuyatoa matatizo ya ndani na kuyapeleka mitaani ndiyo ufumbuzi wa matatizo hayo, ni bora wakajiunga na vyama vya upinzani ambavyo vimeyashikilia bango matatizo binafsi ya baadhi ya wanachama wa CCM.

  Na ni vyema wakafanya hivyo mapema!

  ******************
   
 2. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Babukijana,
  Nakubaliana na wewe kwamba kawaida matatizo ya kifamilia ni bora yakajadiliwa ndani ya familia. Lakini ukiona mambo ya familia yanaanza kujadiliwa hadharani ujue kuna mushikeli. Mara nyingi utakuta familia imeshindwa kutatua matatizo hayo na wanafamilia wanakimbilia nje!

  Utaratibu wa CCM kujadili mambo yao faragha alikuwepo tangu zamani. Nini kimetokea mpaka wana CCM wakaamua "kuasi" na kuanza kuweka mambo hadharani hususani katika Bunge? Lazima kuna tatizo. Tumesikia mara nyingi kwa mfano wabunge wa CCM wakilalamika kwamba wakiitwa kwenye Caucus za chama wanabanwa na kukaripiwa na wakubwa. Kwa maana nyingine hawapewi uhuru kamili wa kuzungumza au maazimio ya caucus hayawaridhishi wabunge. Matokeo ni uasi huu tunaouona bungeni.

  Ni mawazo yangu kwamba Tume ya NEC inayoongozwa na Rais Mstaafu Hassan Mwinyi lengo lake kuu ni kujariibu kuboreshsa demokrasia ndani ya CCM hasa katika caucases za wabunge wa CCM. Suluhisho sio fukuza fukuza au kuwambia wana CCM kujitoa kwenye chama hiyo itakuwa ni kuchimbia kaburi kwa CCM pole pole. Suluhisho ni kwa chama tawala kukubali kwamba hakiendi na wakati na kukubali kwamba kuna matatizo ndani ya chama na kuyakabili kwa ushujaa na uadilifi mkubwa kwa kuzingatia kwamba "Nothing is permanent except CHANGE"
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kuwadhibiti wabunga ni kuuwa demokrasia na kuvunja kanuni za Bunge la tanzania na vile vile kuvunja katiba ya muungano wa Tanzania.
   
Loading...