CCM yapata pigo jingine ....Wagombea warejeshwa, Mabango yaanza kung'olewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yapata pigo jingine ....Wagombea warejeshwa, Mabango yaanza kung'olewa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kizimkazimkuu, Sep 11, 2010.

 1. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  CCM yapata pigo jingine Mwananchi, Saturday, 11 September 2010 09:35

  Waandishi Wetu

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepata pigo lingine baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuyatupa mapingamizi yake dhidi ya wagombea ubunge wa upinzani katika majimbo ya Bahi mkoani Dodoma na Mbozi Mashariki mkoani Mbeya.

  Hili ni pigo la pili katika kipindi cha juma moja lililopita baada ya Baraza la Ushauri wa Masuala ya Siasa kukitaka chama hicho kiondoe mabango ya mgombea wake wa urais Jakaya Kikwete yaliyopigwa Ikulu
  Kutoka Bahi habari zimeeleza kuwa NEC, imetupa pingamizi lililowekwa na mgombea wa CCM katika Jimbo hilo, Omary Badueli dhidi ya mgombea ubunge wa Chama Cha Sauti ya Umma (SAU), Melkzedek Lesaka.

  Awali Badueli aliwasilisha pingamizi hilo kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Bahi kwamba Lesaka hakutimiza idadi ya wadhamini waliotakiwa kwa mujibu wa sheria na alienguliwa.

  Lakini mgombea huyo wa SAU hakuridhika badala yake aliamua kukata rufaa NEC kupinga kuondolewa kwake kwenye kinyang'anyiro hicho cha ubunge.

  Hukumu hiyo ya NEC iliyotolewa kwa barua ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo Mwananchi imefanikiwa kuiona, imeeleza kuwa kikao kilichofanyika Agosti 31, mwaka huu kupitia rufaa hiyo, imetengua pingamizi hilo la CCM.

  "Tume imekubali rufaa yako (Lesaka). Imeona kuwa ulitimiza idadi ya wadhamini waliotakiwa kwa mujibu wa sheria. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekurudisha katika orodha ya wagombea na hivyo wewe ni mgombea halali ilieleza sehemu ya barua hiyo.

  Wakati hayo yakiendelea jimboni Bahi, Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, jana imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea ubunge wa CCM, Godrey Zambi dhidi ya Mgombea wa Chadema, Allan Mwampamba.

  Zambi alimwekea pingamizi mgombea huyo wa Chadema kwa Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Mbozi akidai kuwa mgombea huyo wa Chadema hana sifa kwa kuwa amedanganya kwamba ni mwalimu, lakini pingamizi hilo lilitupwa.

  Baadaye Zambi alikata rufaa NEC kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbozi Mashariki akitaka imwengue mpinzani wake huyo kwa kosa la kusema wongo.

  Jana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Chillewa alilieleza gazeti hili kuwa NEC imemrejesha mgombea wa Chadema kuendelea na kampeni baada ya kumwona hana tatizo la kisheria.


  Kutokana na uamuzi wa NEC kutupilia mbali pingamizi la mgombea wa CCM limesababisha umati wa wanachama wa Chadema kusherekea rufaa hiyo ya ushindi kwa mgombea wake na kusababisha siasa kuwa ngumu katika jimbo hilo.


  Akizungumza na gazeti hili jana mgombea huyo wa Chadema alisema kurudishwa kwake kwenye kinyang`anyiro hicho
  , ni dalili za ushindi kwenye uchaguzi huo.

  Alisema kama Mtanzania, ameamua kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kuwatumikia wananchi na dhamira yake kubwa ni kufikia malengo yake hayo.

  Wakati huo huo, siku chache baada ya Baraza la Ushauri la Masuala ya Siasa kukitaka CCM kiondoe mabango ya picha za mgombea wake wa urais Jakaya Kikwete ambazo zimepigwa akiwa Ikulu, suala la mambango hayo linaonekana kuzidi kukikoroga chama hicho.

  Wakati, NEC ikikutana siku mbili mfululizo sasa jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo na kuwaita wawakilishi wa CCM na kuwahoji, ,mkoani Kagera moja ya bango kubwa lililokuwa limewekwa mjini Bukoba, limeondolewa.

  Hata hivyo viongozi wa chama hicho wilayani hapa wameshindwa kutoa ufafanuzi kutolewa kwa bango hilo.


  Bango lililoondolewa ni miongoni mwa mabango matatu yanayomwonyesha mgombea huyo akiwa katika matukio tofauti. Mabango hayo yaliwekwa eneo la Rwamishenye katika njia panda inayoelekea wilaya za Muleba na Missenyi.

  Bango hilo, liliondolewa siku ya Jumatatu saa 4:30 asubuhi na vijana wawili ambao hawakufahamika kwa majina na badala yake kuwekwa bango la kampuni moja ya simu za mkononi.

  Habari hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, James Magai, Keneth Golima, Mbozi na Phinias Bashaya, Bukoba
   
 2. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ccm lazima wachanganyikiwe mwaka huu
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  hayo mabango yamegeuka uchafu mjini...ukizingatia yamewekwa kwa gharama za ikulu.....kila mtu anajuwa kuwa ikulu kupitia kwa salva rweyemamu ndio imelipa kampuni iliyochapisha mabango hayo ....dola milioni 2.....ni kinyume cha sheria za uchaguzi........
  Kutumia jengo la ikulu ...kwenye mabango ni kinyume....kutumia picha ya rais akiwa na marais wa nchi nyingine....ni uvunjifu wa taratibu za kidiplomasia...maana hatuna hakika kama viongozi ambao rais ametumia picha zao kwenye kampeni mfano lile bango lililopo pale Julius nyerere airport...ameweka picha zake akiwa na bush,obama,pope,kiongozi wa mabohora,agakham...etc.......naweza kuita ni ulimbukeni wa kupitiliza......na sijui washauri wa sheria hasa sheria za kimataifa na diplomasia .....wameachaje hadi kikwete akakubali .....picha za aina hiyo zitumike...na sidhani watawajibu nini pale mabalozi husika wakihitaji maelezo juu ya picha za viongozi wao kutumika kwenye siasa zetu za ndani......

  nadhani kutokana na kampeni ya kikwete kuwa na mapesa mengi ...sasa imejeuka kufuru....
   
 4. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikulu ya sasa si Takatifiu; ni Chafu inahitaji kusafishwa
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Sep 11, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC.


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imelitupa pingamizi la mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), jimbo la Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, dhidi ya mwenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mtela Mwampamba.
  Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Levisson Chillewa, alisema amepokea majibu ya rufaa ya Zambi kutoka Nec, ikielezea kutupwa kwa pingamizi hilo.
  Alisema kwa hali hiyo, anamtambua Mwampamba kuwa ni mgombea halali wa ubunge wa jimbo hilo kupitia Chadema.
  Zambi katika rufaa yake alidai kuwa mgombea huyo wa Chadema ni mwalimu mwajiriwa, hivyo hakustahili kuwania nafasi hiyo.
  Barua ya Nec yenye kumbukumbu namba EA.7/141/02/38 aliyoandikiwa Zambi na nakala kutumwa kwa Mwampamba Nachillewa ilieleza kuwa, kutokana na uamuzi huo (Mwampamba) ataendelea kuwania kiti hicho.
  Naye Mwampamba alithibitisha kupokea uamuzi wa Nec na kusema hivi sasa anaendelea na kampeni katika kata kadhaa za jimbo hilo.
  Awali Chillewa alilitupa pingamizi hilo Agosti 21, mwaka huu lililowekwa na Zambi ambaye hakuridhika, hivyo kukata rufaa Nec.


  Source: NIPASHE.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaaa Katibu makamba upooooo....nadhani kuongoza chama ni kelel au sawa na kucheza kiduku...jumba bovu linakuangukia mwaka huu
   
 7. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Kama kweli kuna bango uwanja wa ndege akiwa na papa liondolewe mara moja.mpuuzi huyu hana robo ya nusu ya kuwa karibu na papa
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Na bado, nimemsikia Kinana asubuhi akiague na Baregu nika jua kwanini ccm waliwazuia wagombea wao kuhudhuria midahalo. Ni nguvu tu na kutetea sera zisizotekelezeka!
   
 9. coby

  coby JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pimbi huyu, mwaka huu lazima afulie, tumempigia kelele sana amtoe Makamba lakini haelewi, kisa Makamba ndio anampeleka kwa waganga wake....ushirikina mpaka Ikulu,ngoja aendelee, kama atamaliza miaka 5..
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  CCM ni chama cha Kidemokrasia, na ni moja ya sera yetu kukuza Demokrasia na ndio maana hio hali tumeiruhusu

  lkn nnahofia(bahati nzuri haitokei) nyny kukamata nchi mtaua demokrasia

  sisi tumeweka uwanja mzuri wa ushindani, ila pale mnapokuwa nyinyi mmepoteza basi mnakimbilia kusema mmeonewa


  ila taratibu mutaelewa rules of game
   
 11. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #11
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Je wale watoto (Jakaya Kikwete anapenda watoto), na wasichana wa team ya Twiga (Michezo ni Ajira) wanaonekana kwenye mabango ya sisi emu walishirikishwa kabla ya kutumia picha zao au ni ubabe? Je wakiamua kuishtaki serikali kwa kutumia picha zao kwenye siasa itakuwaje? Naomba wanasheria humu ndani watusaidie.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  So far nimeona mabango kama mawili maeneo ya iringa along the highway.
  Unaweza kuta ni fedha za serikali zimetumika ie my PAYEE wakati sio wote wanaokatwa PAYEE ni wanachama wa CCM
  Apo kuna level playing field kweli?
   
 13. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli wewe ni muumini! hata iwe vipi huwezi kusubiri ukawaza, ukapata mawazo tofauti. Faith blinds walisema maskini!
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  nyny si mmelalamika kwa tume, na tume imewaandikia barua CCM subirini action, ss ni watu wa fair play
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ....kuna picha moja nimeona anamgawia mtoto wa shule peremende.......nikasema chama cha madaktari wa meno..ambacho binti yake pia ni mmoja wa madaktari wa meno kiko wapi????....maana siku zote madaktari wa meno wapo mstari wa mbele kuwataka wazazi waache kutumia pipi kama zawadi kwa watoto wake na badala watumie zawadi nyingine mfano matunda....pipi zinaharibu meno...

  ......pia ijulikane wazi kuwa kutumia picha ya mtu yeyote bila ridhaa ni makosa ..hasa unapoitumia kutangaza biashara...au kwenye mabango....so natoa tu hadhari...kuwa walioandaa haaya mabango wamelipwa mabilioni...na kila mwezi bango kubwa wanaendelea kulipwa milioni hadi 6 kwa kila bango kama kodi ya pango.....kwahiyo watanzania wote wengi wasioelewa ambao picha zao zimetumika wanastahili malipo...kama ulivyo utaratibu......angalau minimum 1 milioni kwa kila ambaye sura yake imetumika kwa uwazi.....na kuna kiasi cha pesa ambayo anastahili hadi picha itakapoacha kutumika......na ni lazima wawe na mkataba.....sasa kama wametumia picha za watu bila kuwasainisha mikataba ...wajiandae kwa kesi za madai...kwani ni haki wakalipwa....makampuni yote yanayotumia picha za watu huwalipa pesa..na mkataba juu...

  WITO WA WALALAHOI WOTE AMBAO PICHA ZA WATOTO WAO .....WAZEE WAO ZIMETUMIKA WAENDE KUDAI HAKI YAO ....KADIRI YA MKATABA...si vema kuwadhulumu maskini....KINANA ni vema kama amewalipa pesa watu ambao picha zao zimetumika kwenye mabango ,,,,akajitokeza na kutoa ushahidi!!
   
 16. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nafikiri muda umefika CCm inabidi ikae chini na kujiuliza nini hasa tatizo, badala ya kukalia ubishi na kujiona kuwa wapo sawa, otherwise mipasuko hii midogo midogo italeta balaa zaidi na zaidi katika Taifa letu.
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  shame ..fair play kwa kuzui uhuru wa habari kwa baadhi ya wagombea....?? fair play kwa kutumia pesa za ikulu kununua fulana na mabango?? fair play kwa kukataa kulipia kodi vifaa vya kampeni???....fair play kwa kutumia magari ya serikali na resources.............fair play kwa mke wa rahisi kutumia pesa za hisani anazopewa kwa ajili ya masikini pale WAMA kama zake kwa ajili ya kampeni ....?? fair play gani tunaongelea ..
   
 18. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Doh nimemsikia Kinana alivyokuwa anachemsha. Anawalaani Chadema eti kwa kudai wanaweza kutoa elimu bure ambapo anaona haiwezekani. Anashindwa kujua kuna matumizi mengi serikalini ambayo yangeweza kuepukika na hivyo kuelekezwa kwenye elimu.

  Ila Baregu hakumkawiza, ameibua ile CCM kuwanyima wagombea wake kushiriki mdahalo, tena kwa ufasaha sana akisisitiza haja ya kuwa wabunge wa CCM wamekuwa wakitoroka bungeni wengine wakisinzia. Eti Kinana, anadai watu kwenye remote areas wanahitaji kujua watasaidiwa hivi, eti midahalo sio muhimu, CCM hawana nafasi kwa maana wana kazi kubwa ya kufanya kuliko CCM, hawana muda wa kupoteza.
   
 19. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  SAMAHANI NAOMBA NIKUULIZE SWALI,
  Hivi ni kwanini amna bango ambalo linaonyesha picha ya Dakitari Kikwete na Mshahuri wake wa kiufundi Sheikhe Yahaya?
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  njaa na kujipendekeza na kujkomba vitakuuwa kaka!
   
Loading...