CCM yanawa mikono kwa mashambulizi ya Sophia Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yanawa mikono kwa mashambulizi ya Sophia Simba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  CCM yanawa mikono kwa mashambulizi ya Sophia Simba[​IMG]Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, chama chake hakihusiki na mgogoro unaomhusu kada wake Sophia Simba.*Hakihusiki na mgogoro wake na Anne Kilango

  Na Joyce Mmasi

  CCM imeamua kutoingilia mgogoro baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Sofia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango, kwa maelezo kuwa unawahusu wao wenyewe na kwamba; hakuna miongoni mwao aliyelalamika kupitia taratibu za chama.

  Msimamo huo umetolewa siku chache baada ya ugomvi mkubwa kuibuka katia ya kada hao wa CCM, baada ya Simba kumtuhumu Anna Kilango mambo mbalimbali katika kikao cha Kamati ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kilichofanyika mjini hivi karibuni.

  Simba alidai ndani ya kikao hicho kwa harusi ya John Malecela na Kilango ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

  Simba anadaiwa kusema katika kikao hicho cha kuwa Kilango siyo msafi na kwamba kelele anazopiga kuhusu ufisadi zinatokana na kukosa kuwa mke wa rais.

  Hata hivyo, Kilango hivi karibuni alisema amedhamiria kufikisha mahakamani Waziri Simba kwa madai ya kudhalilishwa.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliambia Mwananchi Jumapili wiki hii kuwa ugomvi wa wanawake hao, ambao pia ni wanachama wa Jumuia ya Wanawake (UWT), haukihusu chama hicho.

  Makamba alisema hayo baada ya kulizwa msimamo wa CCM baada Kilango kutishia kwenda mahakamani kumshtaki Mwenyekiti wa Simba kwa tuhuma za kumkashifu.

  Makamba alisema yuko tayari kuzungumzia jambo lolote linalohusu chama kwa ujumla, lakini si ugomvi wa wanawake hao kwa sababu hataa yeye hajui wanachogombea.

  “Umesikia mama, niulize mambo yanayonihusu mimi na CCM; sitaki kuzungumza mambo ya watu…. Ule ni ugomvi wa Sofia na Mama Kilango. Yale ni mambo ya watu sio ya Chama. Elewa hivyo kuwa siwezi kuzungumzia mambo ya watu kwa kuwa hayana faida kwa chama chetu,” alisema Makamba.

  Simba ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Taifa, hivi karibuni aliripotiwa kuingia kwenye mzozo na Katibu wake, Husna Mwilima akimtuhumiwa kuendesha kampeni za kutaka kumng'oa katika wadhifa wake.

  Hata hivyo, Simba ameripotiwa akisema kwamba mzozo ulipo katika jumuia hiyo unatokana na watu kutaka kuzuia hoja ya kuwa na ukomo katika ubunge wa viti maalum na uongozi wa jumuia hiyo.

  Alisema kwamba, hatalegeza uzi katika kusimamia jambo hili ili kuondoa usultani katika ubunge wa viti maalum kuwa wapo waliofanya uwakilishi huo wa wananchi kuwa ni wa kudumu.
  Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati alisema suala la ugomvi baina ya wanachama hao halijawasilishwa ndani ya chama, hivyo hawezi kuuzungumzia kwakuwa hana ushahidi juu ya jambo hilo.

  “Hilo jambo halijaletwa rasmi kwenye chama, hivyo hatujui endapo ni maneno ya magazeti au yana ukweli kiasi gani. Wacha tuyasubiri kama yapo wakiyaleta kwenye chama ndipo tutakuwa na lakusema," alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  Alisema pamoja na kwamba Kilango na Simba ni wanachama wake, lakini hawawezi kuzungumzia au kutolea maelezo mambo yanayowahusu bila kufikishwa ofisini kwake.

  Alielezea suala la ugomvi huo kuwa ni sawa na maneno yanayovumishwa tu barabarani ambayo wakati mwingine ukiyachunguza utabaini kuwa hayana ukweli. Wakati viongozi hao wa chama wakinawa mikono kuhusu ugomvi wa makada wao wa CCM, hali ndani ya chama hicho haijatulia kutokana na mgawanyiko mkubwa kuzidi kuongezeka.
   
 2. l

  libaba PM Senior Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hiki chama , kinaymbishwa na hawa kina Simba kwa sababu Mwenyekiti wa Chama si mkali. ni muungwana.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  unajua sababu za kumchagua....wala si mambo ya ukali...mengine search kwenye google....
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  duuh.kiongozi mbona na gogle sipati results...hebu ni PM nijuze why alichaguliwa kuwa minista.hhaaaa
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kama chama kime nawa mkono it means that the opinions of Sophia Simba are not that of the party. If they are serious about what they are saying then they should stop Sophia Simba from airing her opinions using party platforms. They can't allow her to keep saying things during party meetings etc and still say they want nothing to do with her.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Jamani Sophia anatumwa.....sio kama anakuja tu anakurupuka tu....ndio maana ni untouchable...ile nafasi ni zawadi kwa fitna alizowafanyia wabaya na wapinzan wa JK na mtandao...ndani ya chama na serikali ....yeye kazi yk kujibu mapigo kwa yeyote kumchafua na kumsemea mbovu ndani ya vikao....hajakaa bure pale uliza ile ndio silaha ya mkulu no 1
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Makamba na wenzie lazima wakae kimya kwa hiyo mashine
  we Mama Kilango na kelele zake zote kaufyata, Waziri mkuu na Makamu mwenyekiti wa CCM wa zamani J Malechela kaufyata unafikiri hiyo mashine ni mchezo
   
 8. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #8
  Nov 29, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Skills4Ever,nimekupata mkuu,nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa
   
Loading...