Kwa barua hii nakuomba uwe tayari kupokea maagizo yatakayokuwa yakitolewa kutoka ngazi mbalimbali, pia uzingatie ratiba ya jimbo ulilopangiwa. Pia nakuomba ufike ofisi ya CCM Wilaya Septemba mosi, mwaka huu kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni jimbo la Nzega, aidha jimbo la Bukene itakuwa Septemba 4, mwkaa huu.
Katibu mkuu wa ccm, yusuf makamba, alipotakiwa kutoa ufafanuzi na gazeti hili, alisema yeye anatambua wazi bashe bado ni mwanachama wao halali, hivyo viongozi wa mkoa wa tabora wana haki ya kumtumia pale panapohitajika.
"kama katibu wa mkoa wa tabora amemteua, ana haki ya kufanya hivyo, anatambua mchango wake ndani ya chama… hata kama kuna makada 20, kumbuka ndugu yangu hata kanisani utasikia kuna askofu, padri, mchungaji, shemasi, katekista na wazee wa kanisa… hivyo hata ccm tunao wa aina hii,
… kama hilo suala limefikiwa basi ni jema, nadhani wamegundua namna mchango wake unavyotambulika ndani ya chama," alisema makamba..
HYPOCRITES!!!!!ogwalumapesa said:katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) yusuph makamba ,amesema kama aliyeenguliwa kugombea ubunge jimbo la nzega na chama hicho hussein bashe,ni raia halali wa tanzania basi anayestahili kubebeshwa lawama ni wasaidizi wa jk na si chama hicho
akizungumza na nipashe jijini dar es salaam jana,makamba alisema chama chake kilipata vielelezo kwamba bashe si raia kutoka kwa wasaidizi wa rais hivyo ccm haistahili lawama
'' wasaidizi wa rais ndiyo walituambia sisi kuwa bashe si raia sasa kama wizara ya mambo inasema ni raia basi ituambie ,lakini leo tunaendelea kuamini tulichoambiwa na wasaidizi wa rais''
source nipashe
Nitamshangaa sana Bashe akikubali hili na hilo litajidhihirisha wazi kwamba either Bashe huna nia dhati ya kuwatumikia wananzega au ni una agenda nyengine isiyokuwa ya utumishi kwa wananzega inakuyokusukuma ugombanie ubunge. ...Sasa kama unataka unaamini katika unafiki then kubaliana nao but kwa expense ya kuyasahau matakwa ya wananzega!!!
Maji yamewafika shingoni sasa wanahaha huku na kule. Siku chache tu walitaka kumtema huyu nje ya Tanzania leo wanampigia magoti! Bila hata ya Kikwete kumuomba samahani hadharani.
Pamoja na kujikoroga kwa CCM, na hila za kumweka Mr WAMA bungeni, nina hoja moja inayomhusu Bashe. Huyu bwana amezaliwa hapa na wazazi wahamiaji ambao si watanzania. Amekulia na kusomea hapa Tanzania hadi eimu ya chuo kikuu. Amekuwa kiongozi wa vijana na CCM kwa muda mrefu. Mwaka 2008 kwakujua kuwa anataka kugombea ubunge akaenda mahakamani kuukana uraia wa somalia, uraia ambao ameutumia kinyume cha sheria kwa kusoma kama Mtanzania na kupata nyadhifa kama mtanzania.
Ninadhani wapo watu walimshauri kuhusu jambo hili na hatari inayomkabili. Kwavyovyote vila Hussein Bashe si Mwadilifu kwasababu amevunja sheria za nchi kwa miaka zaidi ya 25 na sasa anataka aende kwenye jengo akatunge sheria zile zile asizoziheshimu. Kwamamtiki hii sidhani kuwa bashe ana mapenzi na nchi hii, vinginevyo angeukana usomali pale tu alipokuwa na fahamu za uraia wake pengine hata kabla ya kujiunga na chuo kikuu na sio miezi 24 kabla ya uchaguzi.
Tutawezaje kujua kuwa kabla ya september 2008 huyu bwana alikuwa ni mwananchama wa Alshaabab, kwa maana kuwa hakuwa Mtanzania bali Msomali aliyeishi kwa mazoea tu. Narejea tena pamoja na mizengwe aliyowekewa lakini UADILIFU wa Bashe unatia mashaka sana na mbio zake mjengoni pengine si za kuwakilisha wana nzega bali kundi jingine kwa mgongo wa Nzega
Kingine nillichozungumza ni swala zima la kufungwa kwa vyuo vikuu nchini....nilisema naamini kinachopigiwa kelele sio SERA YA UCHANGIAJI YENYEWE bali ni UTEKELEZAJI WA SERA, hivyo sioni sababu ya serikali kutumia ubabe kufunga vyuo badala yake wakae chini na wadau kujadili namna bora ya kutekeleza sera hii. Najua kuwa iko katikati ya mwaka wa fedha wa serikali lakini muhimu kukubali kuwa yapo matatizo katika utekelezaji wa sera hii, ili njia bora itafutwe kisha tuwe na utekelezaji bora zaidi mwaka ujao wa fedha. Maghembe aache ubabe si jambo la buisara kila mara kufunga vyuo hivi maana tunaanzisha utamaduni mbovu wa kutojadiliana kumaliza matatizo yetu hili sio jema.....
Kaka naona umefafanua vyema, kwanza nikupongeze kwa kuingia jamvini na kuchangia hoja hii, ninakuomba ujibu na thread nyingine zinazokuhusu humu jamvini, nimepata huzuni sana kuona thread kuwa wachagga waliopo CCM wanajipendekeza, hawa kaka zetu Cyril Chami, Aggrey Mwanri, Beno Malisa na wengine wengi akiwemo dada yangu wa Kilimanjaro mama Nsilo Swai wanaotumikia CCM ina maana wanajipendekeza?? naomba ujibu hoja zinazokuhusu humu jamvini... Ahsante ni hayo tu mkuuKingine nillichozungumza ni swala zima la kufungwa kwa vyuo vikuu nchini....nilisema naamini kinachopigiwa kelele sio SERA YA UCHANGIAJI YENYEWE bali ni UTEKELEZAJI WA SERA, hivyo sioni sababu ya serikali kutumia ubabe kufunga vyuo badala yake wakae chini na wadau kujadili namna bora ya kutekeleza sera hii. Najua kuwa iko katikati ya mwaka wa fedha wa serikali lakini muhimu kukubali kuwa yapo matatizo katika utekelezaji wa sera hii, ili njia bora itafutwe kisha tuwe na utekelezaji bora zaidi mwaka ujao wa fedha. Maghembe aache ubabe si jambo la buisara kila mara kufunga vyuo hivi maana tunaanzisha utamaduni mbovu wa kutojadiliana kumaliza matatizo yetu hili sio jema.....
Nape tunashukuru kwa kutua jamvini na kutoa ufafanunuzi kuhusiano na jambo hilo na tungelifurahi zaidi kama ungelikua unajitokeza mara kwa mara kutokana na nafasi yako katika chama kuzitolea maelezo baadhi ya hoja.Hii itatusaidia kuepuka majungu,kuna maswala mengi na kero nyingi hivi sasa ambazo ni kubwa kwa wananchi ukimya wa CCM unazaa habari nyingi amabazo ni vigumu kuelewa upi uzushi na upi ukweli.Ombi langu kwako habari namba moja na ambayo kila Mtanzania anaisubiri kwa hamu ni hatima ya kujivua "magamba"Ili kuepuka majungu tufahamishe kwa kifupi swala hili limefika wapi?Maana kuna minon'gono barua zimeandikwa hazikuandikwa,wamekabidhiwa hawakukabidhiwa nk.Ebu tupe kwa ufupiNaiheshimu sana forum hii kwani inasaidia kutoa mambo ambyo wakati mwingine hayasemwi na vyombo vingine.Nawashukuru kwa kunikaribisha, napokea kwa heshima kubwa karibu yenu wakubwa, naahidi ushirikiano mkubwa kwa kadri ya uwezo wangu wote.
SASA MAMBO MUHIMU TULIYOONGEA KATIKA KIPINDI CHA MLANGO WA DHARURA NI;
1). Niliunga mkono uteuzi wa wagombea kutoka Zanzibar kugombea Uenyekiti UVCCM. Baadhi ya sababu ni kuwa haya ni maamuzi ya kikao halali cha chama NEC, kwa kuzingatia kuwa hakuna uteuzi ambao usingekuwa na mapungufu, hata huu ninaouunga mkono una mapungufu yake mengi tu, lakini ukilinganisha na uteuzi mwingine kwa MTAZAMO WANGU huu ulikuwa nafuu kuliko mingine. Lakini nilikumbusha kuwa mwaka 2003 niligombea mimi uenyekiti uvccm na kulikuwa na wagombea toka znz ambao hawakurudishwa hivyo sioni sababu ya bara kulalamika leo.
2).Utendaji wa Makamba, nilichosema ni kuwa si dhambi kujadili utendaji wa Makamba kama katibu mkuu wa CCM, tena hata wanachama wa kawaida wana nwajibu wa kujadili hali ya chama chao, KWANI NAAMINI HICHI NI CHAMA CHA WANA CHAMA NA SI VIONGOZI. N a nikaongeza kuwa kikao chenye mamlaka ya kumwajibisha Katibu mkuu wa ccm ni NEC huu ndio utaratibu, hivyo hata baada ya kujadili mwisho lazima malalamiko yaletwe NEC ndo wanaweza kumwajibisha Katibu Mkuu.
3). Nikasema KUGOMBEA URAIS 2010 SI DHAMBI ni huru kwa mwana chama yeyote kwa mujibu wa katiba ya CCM ambayo ndio sheria mama, kwani hata ilani ya uchaguzi inatengenezwa mpya, hivyo sitashangaa kuona watu wanachukua fomu kuomba uteuzi, ndio demokrasia.
4). Nikasema pia si kweli kwamba wanaokosa wanakumbatiwa, inawezekana kwa upande mmoja lakini sio katioka kesi zote, nikatoa mfano wa waliowajibishwa kwa makosa ya Richmond, nikasema hawa walisaliti chama kwani tuliwatuma kutekeleza ilani ya chama wao wakaenda kutekeleza yao.
5.) Nikajibu swala la kufukuzwa uana chama uvccm, nikasema MWENYE AKILI NAJUA NANI MKWELI NANI MWONGO kwani UJENZI MPAKA SASA UNAENDELEA BILA MKATABA, MAPUNGUFU NILIYOYAELEZA NDIYO YALIYOUNDIWA TUME KUREKEBISHWA, SASA MWONGO NA MKWELI IKO WAZI, lakini najua mtu mzima kukiri kosa ni ngumu...maji marefu hapa kwa mzee wangu....
HAKIKA HATUKUMTAJA KABISA HUSSEIN BASHE KATIKA MAZUNGUMZO YOTE, SI MIMI, WALA OMARY KIMBAO AU JERRY SILAA NA HATA MTANGAZAJI KIBONDE, NIMESIKITISHWA NA TAARIFA HIZI KUZIKUTA HUKU, GAZETI LA TANZANIA DAIMA WALICHAPA PIA LAKINI KIMAKOSA, SIKUKANUSHA KULE COZ INGEATHIRI UCHAGUZI KWA UPANDE MMOJA NA HASA MGOMBEA MMOJA.
Namwomba ndugu yangu asituharibie heshima ya forum hii, naamini nimeeleza kwa kifupi yaliyotokea.
Nnauye Jr