CCM yamgwaya Mkono! Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM yarudisha jina lake...

Hivi hizi jumuiya za chama zina nini? Kwanini huyu tycoon Milionea wa kutupa Mkono analia na kutapatapa ili apewa kazi ngumu ya kuongoza jumuiya ya wazazi?
 
MH. KIKWETE NA MH. MUKAMA

C/O MH. NAPE,


Hivi katika karne hii mwanachama yeyoyote anaweza ku threaten chama kikubwa kama CCM na watu eti wakahaha kuwa akiwekwa pembeni wengine waendeleze uongozi basi chama kitatikisika au kufa?

Kama baba wa Taifa, J.K. yerere mwasisi wa chama alifika mahala akang'atuka na chama hakikutikisika na sasa hata katangulia mbele ya haki lakini chama kipo na kinaendelea kuwepo sembuse Mkono????????? kweli?????? Eti ana siri? Hivi nani mwenye siri nyingi za chama kati ya Mkono na aliyekuwa Chief campaigner wa rais wetu; aliyewahi kuwa Waziri n.k lakini anafika mahali anasema imetosha wengine waendelee!

Basi, fuateni sauti za watani wenu wa jadi wanaomshangilia Mkono, kuwa huyu jamaa ni kiboko kwamba ana MVUTO na kweli chama kitaendelea sana.

Kidumu chama cha mapinduzi

Ni mimi,

mwanachama nisiye na fedha nyingi wala siri za chama.
 
Back
Top Bottom