CCM yamgwaya Mkono! Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM yarudisha jina lake...

Kwasababu ya kujua SIRI za VIONGOZI wa CCM kujulikana na Baadhi ya Wabunge na Haswa Mwanasheria

Mkono CCM inaendeshwa BILA Demokrasia... Ni UBABE, KUJUANA kwahiyo it is a CULT

Mkono ni mmoja wa mafisadi papa wa nchi hii hivyo ana fedha nyingi aghalabu ni chafu ; lakini kwa vile mkweree ni limbukeni wa pesa kwani amezijua ukubwani hakukuwa na nafasi ya chama cha magamba kumtosa fisadi mkono!!
 
madhara ya mkono kuondoka yangekuwa makubwa kwa ccm!

Kurudishwa kwa jina la Mkono kwenye kuwania Nec ni ishara tosha kuwa hakuna fisadi papa hata mmoja ambae jina lake litatoswa!! Tutegemee Lowassa na Chenge nao kupeta huko magambani!! Hizo kelele kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa ni kelele tu hazina mashiko!!
 
DPP ni kibaraka wa rais,hakuna kesi itakayofunguliwa yenye kuhusu mafisadi kabla hajamwuliza rais maoni yake endapo kuna watu wake watakuwa wameguswa,ama hata yeye mwenyewe.Mfumo huu haufai hata kidogo,na hakuna haki itakayotendeka,hapo ni kiduku tu.

JK ndo aliyemteua DPP na hakuna kesi inayofunguliwa bila idhini ya DPP.

Ninatofautiana na wewe kidogo katika hili. Kwangu mimi tatizo siyo mfumo. DPP kuteuliwa na serikali siyo tatizo, tatizo ni kukosekana kwa transparent, accountability na independent decision making.

Mbona hata UK wana utaratibu kama unaofanyika Tanzania kumpata DPP.
 
inamaana ndani ya ccm vyeo ni kwa ubabe? Naye Mkono amekosa sifa za kiongozi jasiri kwani anaonyesha kwa kupewa cheo youko tayari kuuza hata familia yake!! Iweje ataumie silaha inayoangamiza watanzania wengi kujipatia cheo?
 
Ninatofautiana na wewe kidogo katika hili. Kwangu mimi tatizo siyo mfumo. DPP kuteuliwa na serikali siyo tatizo, tatizo ni kukosekana kwa transparent, accountability na independent decision making.

Mbona hata UK wana utaratibu kama unaofanyika Tanzania kumpata DPP.
DPP anateuliwa na rais,na hapo ndipo tatizo lilipo,kwasababu atafanya kazi kwa matakwa ya rais.Kesi ya kumgusa rais ama watu wake itafikishwa mahakamani?Unaweza kuniambia huo utaratibu wa UK kumteua DPP uko vipi?pia usipindishe kwa kusema eti ni serikali ndo inamteuwa.

DPP,kama una kesi ambayo haihusiani na kigogo wa juu wa serikali,basi kama wewe ni "mtu wake" kwa namna yeyote ie rushwa,kufahamiana etc,basi hufunguliwi kesi.Hakuna kesi inayofunguliwa bila yeye kuidhinisha.Hakuna!

Hata hizi kukurukakara sijui eti za rushwa,hakuna kesi itakayofunguliwa bila yeye kukubali.Ni huyo mtu mmoja anaamuwa,sasa hata vigezo anavyovitumia unavijuwa wewe?DPP kwenye mfumo wetu,akisema hakuna kesi huna la kufanya!wala huruhusiwi kumwuliza ni kwanini.Sasa wewe unataka kusema hamsikilizi bosi wake aliyemteuwa?Ndiyo maana nikasema ni kiduku,watu wanazungunguka hapo hapo tu,mtapiga kelele wee!lakini mwisho wa yote si TAKUKURU wala mahakama,kwasababu ikifika mahakamani ujuwe haina madhara kwa aliyemwajiri,mwisho wa yote ni DPP,na kamwe usidhani atakubali kesi inayomgusa JK na watu wake iende mahakamani.

Mfumo ukibadilishwa,hopefully na katiba mpya,basi tunaweza kupata haki.Hiyo independent decision making haitapatikana kama anateuliwa na rais,ni kama ilivyo kwa wakuu wa mikoa,wilaya nk.Na hata polisi ndo maana ni kama wanaifanyia kazi ccm.
 
jmushi1,

Kama ujuavyo sheria nyingi za nchi yetu na uendeshaji tume copy & paste kutoka kwa Mwingeleza.

DPP wa nchini UK anateuliwa na mwanasheria mkuu wa serikali, mwanasheria mkuu wa serikali anateuliwa waziri mkuu. vilevile hata UK kuna kutengo cha kupambana na rushwa. DPP hata UK ni mtu mwenye madaraka ya mwisho katika maamuzi ya kesi zote kuanzia za kuiba kuku mpaka za kuhujumu uchumi. Transparent, accountability na independent decision making ndiyo inayoongoza kazi yake.

Nimalizie kwa kusema kuwa, Tanzania rais yuko juu ya sheria kwa sababu ni head of state and head of government kwa hiyo hata kama akifanya jambo lolote kinyume cha sheria ni kazi bure kwa Polisi na DPP kutaka kujua linaloendelea kwa vile hawana nguvu ya kisheria kumtaka ajibu wakati USA katika mfumo wa rais kama huu wa Tanzania, Rais anatakiwa kisheria kujibu mbele ya mahakama kwa madudu yanadhaniwa ameyafanya (impeached) kwa sababu hayuko juu kisheria.

Nafikili tukubali kuwa, hakuna serikali humu duniani isiyokuwa na siri katika maamuzi yake. lakini uendeshaji wake usiwe wa usiri wa kiwango cha juu kama serikali zetu zinavyofanya kwa vile hakuna Transparent, accountability na independent decision making na hivyo kuwa ni kichocheo cha rushwa na kulindana.
 
mkono kwa upande wa ccm kanda ya ziwa anasaidia sana kukata jina lake nikuhalalisha upinzani na kutoa nchi kwa wapinzani hata kabla ya uchanguzi 2015. hakuna mtu aliye na nguvu, mvuto wa kisiasa ndani ya ccm kanda ya ziwa
 
Mbona jina lake limeishawahi kukwatwa kwenye Jumuiya ya Wazazi.

Inaelekea kwa vile hakuwapiga mkwara kwene hiyo position. Alinyamaza, sasa wamempeleka kwenye kona ameonyesha makucha yake mpaka Boss kagwaya..................???!!!! Hii kweli ni SISIMMMM............................!!!
 
jmushi1,

Kama ujuavyo sheria nyingi za nchi yetu na uendeshaji tume copy & paste kutoka kwa Mwingeleza.

DPP wa nchini UK anateuliwa na mwanasheria mkuu wa serikali, mwanasheria mkuu wa serikali anateuliwa waziri mkuu. vilevile hata UK kuna kutengo cha kupambana na rushwa. DPP hata UK ni mtu mwenye madaraka ya mwisho katika maamuzi ya kesi zote kuanzia za kuiba kuku mpaka za kuhujumu uchumi. Transparent, accountability na independent decision making ndiyo inayoongoza kazi yake.

Nimalizie kwa kusema kuwa, Tanzania rais yuko juu ya sheria kwa sababu ni head of state and head of government kwa hiyo hata kama akifanya jambo lolote kinyume cha sheria ni kazi bure kwa Polisi na DPP kutaka kujua linaloendelea kwa vile hawana nguvu ya kisheria kumtaka ajibu wakati USA katika mfumo wa rais kama huu wa Tanzania, Rais anatakiwa kisheria kujibu mbele ya mahakama kwa madudu yanadhaniwa ameyafanya (impeached) kwa sababu hayuko juu kisheria.

Nafikili tukubali kuwa, hakuna serikali humu duniani isiyokuwa na siri katika maamuzi yake. lakini uendeshaji wake usiwe wa usiri wa kiwango cha juu kama serikali zetu zinavyofanya kwa vile hakuna Transparent, accountability na independent decision making na hivyo kuwa ni kichocheo cha rushwa na kulindana.
Mkuu,kama ilivyo kwa DPP,ndivyo pia ilivyo kwa Hosea,yani kama issue imemgusa mtu mkubwa ama hata kama kuna connection na mkulu mwenyewe,basi usitegemee lolote,ndiyo maana hata vita dhidi ya grand corruption inakuwa shida,kwasababu wahusika ndo wenyewe wenye kutoa maamuzi nk,DPP na mkuu wa PCCB wote wanafanya kazi kwa maslahi ya rais...ebu soma hapo chini na kama una muda ipitie hiyo ripoti...
Support to Prevention and Combating of Corruption Bureau
6.2. The PCCB is the key institution in the GoT's fight against corruption, its mandate
103
being to advise and review the practices and procedures of public, parastatal
and private organisations; to facilitate the detection and prevention of corruption;
to work with international institutions, agencies or organizations in the fight
against corruption; to investigate and, subject to the directions of the Director of
Public Prosecution (DPP), prosecute corruption offences; and to educate the public
and enlist their support to fight corruption. Commissioning donors' support is aimed
at strengthening PCCB, from Sweden's support to the development of an M&E
Framework for NACSAP to Norway's financing of cars and surveillance equipment
104.
This support has been valuable but not sufficient to address the key (acknowledged)
challenges that PCCB has faced over the evaluation period.
6.3. PCCB independence, and that of other key AC institutions, is potentially compromised
by the fact that it reports directly to the President
105: For example, the
credibility of the PCCB suffered when it gave a clean bill of health to a government
deal (‘Richmond' – see Box 3.1), which was subsequently alleged to have involved
corruption. The PCCB benefits from the strong leadership of its executive director, a
positive attribute but also one that has caused concerns (amongst development
partners at least) that the Bureau and its role may become too closely associated
with just one individual, and thereby find itself politically vulnerable.
http://www.oecd.org/countries/tanzania/48912823.pdf

Sasa ebu niambie ni kesi ngapi za mafisadi zimeshafunguliwa?Wengine si aliwanyanyua hata mkono kwenye uchaguzi mkuu na akasema ni wasafi?Unataka Hosea na DPP waseme hapa mh rais,hawa ni wala rushwa na faili hili hapa wapelekwe mahakamani?Hata ile kesi ya kina Mramba ilikuwa danganya toto ili kuwa please donors,thats it,hakuna la maana.Mafisadi waliotakiwa kuwa jela sasa hivi si ndo wako poised kuchukuwa madaraka ya chama na pengine nchi?Unaweza kuniambia kwa uhakika kuwa DPP na mkuu wa PCCB hawafanyi kazi kwa maslahi ya rais?Think mkuu...Ndo maana nikasema ni kiduku,hakuna litakaloendelea hadi mfumo ubadilishwe,na hopefully katiba,kwani nani kasema kuwa mfumo flani ukifanya kazi marekani na uingereza ndo utafanya kazi bongo?Mbona hata ubepari wenyewe unatutesa?
 
Mkuu,kama ilivyo kwa DPP,ndivyo pia ilivyo kwa Hosea,yani kama issue imemgusa mtu mkubwa ama hata kama kuna connection na mkulu mwenyewe,basi usitegemee lolote,ndiyo maana hata vita dhidi ya grand corruption inakuwa shida,kwasababu wahusika ndo wenyewe wenye kutoa maamuzi nk,DPP na mkuu wa PCCB wote wanafanya kazi kwa maslahi ya rais...ebu soma hapo chini na kama una muda ipitie hiyo ripoti...
http://www.oecd.org/countries/tanzania/48912823.pdf

Sasa ebu niambie ni kesi ngapi za mafisadi zimeshafunguliwa?Wengine si aliwanyanyua hata mkono kwenye uchaguzi mkuu na akasema ni wasafi?Unataka Hosea na DPP waseme hapa mh rais,hawa ni wala rushwa na faili hili hapa wapelekwe mahakamani?Hata ile kesi ya kina Mramba ilikuwa danganya toto ili kuwa please donors,thats it,hakuna la maana.Mafisadi waliotakiwa kuwa jela sasa hivi si ndo wako poised kuchukuwa madaraka ya chama na pengine nchi?Unaweza kuniambia kwa uhakika kuwa DPP na mkuu wa PCCB hawafanyi kazi kwa maslahi ya rais?Think mkuu...Ndo maana nikasema ni kiduku,hakuna litakaloendelea hadi mfumo ubadilishwe,na hopefully katiba,kwani nani kasema kuwa mfumo flani ukifanya kazi marekani na uingereza ndo utafanya kazi bongo?Mbona hata ubepari wenyewe unatutesa?

Mkuu,
Ni kweli kama usemavyo siyo kila walifanyalo watu wa 'west' na sisi lazima tufuate.

Ni kweli kuwa Rais ana madaraka makubwa mno katika maamuzi na uendeshaji wa nchi. lakini madaraka na maamuzi haya yatakuwa ya maana kwa rais kama hatakuwa minded corrupt, inept,lazy and weak. kibaya zaidi kama ameingia madarakani kwa njia ya rushwa na udanganyifu. historia inadhihilisha kuwa, haiwezekani binadamu akatumikia mabwana wawili. wala rushwa na wasio wala rushwa. wadanganyi na wasio wadanganyi. mmojawapo lazima ataadhilika kwa kiwango kikubwa.

Mimi nafikili kama rais hatakuwa juu ya sheria, ninaamini hata utendaji wa watendaji wengine utakuwa accountable na Bunge litaweza kufanya kazi yake kisawasawa katika kuisimamia serikali.

Katika nchi zilizoendelea, theoretically and practically, Bunge lina nguvu za kiutendaji zaidi ya serikali wakati Tanzania, practically, serikali ndiyo ina nguvu za kiutendaji zaidi ya Bunge.

I wish, Tanzania ya mwaka 2015 ikawa ama na Rais kutoka CHADEMA na wabunge wengi kutoka CCM au Rais kutoka CCM na wabunge wengi kutoka CHADEMA ili nchi iwe na balance of power na uwazi wa utendaji.

Mkuu, asante kwa kunipatia hiyo link, nitaisoma usiku na nitakuja tena hapa kijiweni kesho.
 
Back
Top Bottom