CCM yamgwaya Mkono! Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM yarudisha jina lake... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamgwaya Mkono! Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM yarudisha jina lake...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  25 September 2012

  For ref: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/323454-nimrod-mkono-aitisha-ccm.html

  KAMATI ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imerudisha jina la Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kwenye Jumuiya ya Wazazi.

  Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya jina la mbunge huyo kutupwa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo na kusema hadharani kwamba akiachwa moja kwa moja, patachimbika.

  "Hapatatosha (CCM)," alisema Mkono alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoswa kwake katika mchujo wa awamu hiyo ya awali.

  Katika matokeo ya mchujo huo wa awali uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam Mkono alishika nafasi ya mwisho kati ya wagombea 13, huku Abdallah Bulembo, Martha Mlata na John Barongo wakipitishwa.

  Hata hivyo, Mkono ambaye ni wakili maarufu nchini, alipinga kushindwa katika kinyang'anyiro hicho akisema bado mchakato wa uchaguzi unaendelea.

  Juzi, kamati hiyo iliyoketi mjini Dodoma chini ya Rais Jakaya Kikwete inadaiwa kuondoa jina la John Barongo ambaye alikuwa amependekezwa na Baraza Kuu la Wazazi kwenye nafasi ya tatu na kuingiza majina ya Mkono pamoja na Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza.

  Awali, ilielezwa kuwa mkono alipendekezwa na Baraza la Wazazi kwenye nafasi ya mwisho na Rweikiza nafasi ya sita. Lakini inadaiwa baada ya Mkono kupiga ‘mkwara' jina lake lilipelekwa kwenye Sekretarieti likiwa la nne.

  Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa baadhi ya wagombea wamependekezwa kuondolewa kwenye kinyang'anyiro hicho, lengo likiwa ni kujenga mshikamano wa chama.

  Wengine wanaotajwa kupendekezwa kuenguliwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja na hasimu wake, Mbunge wa Kahama, James Lembeli.

  Chanzo hicho kimesema Lembeli amependekezwa kuachwa na kamati hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa kupunguza idadi ya wabunge waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.

  Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amekuwa akirejea kuwa hayo ni mapendekezo siyo uamuzi wa mwisho na kwamba, kikao pekee chenye mamlaka ya kuondoa jina la mgombea ni Halmashauri Kuu ya CCM.

  Kamati hiyo iliyomaliza kazi yake jana alfajiri, ilipendekeza majina ambayo yamepelekwa Kamati Kuu (CC) iliyoketi jana mjini hapo ambayo pamoja na mambo mengine, ina jukumu la kuyabariki kabla ya kupelekwa katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kupigiwa kura.

  Mabadiliko makubwa yaja CCM


  Akifungua mkutano wa Kamati Kuu (CC) jana, Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alisema kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili kimechukua muda mrefu kwa sababu kilipitia kila jina la mgombea na mapendekezo yaliyotolewa na vikao husika na kwamba, watu watarajie mabadiliko makubwa.

  Rais Kikwete alisema Kamati ya Usalama na Maadili imelazimika kupangua mapendekezo mengi ambayo yalipelekwa na vikao vya kamati za siasa za wilaya na mikoa.

  Aliwaambia wajumbe wa Kamati Kuu kuwa kazi waliyofanya Kamati ya Maadili ilikuwa kubwa ya kupitia jina moja baada ya jingine na kujiridhisha kuhusu alama ambazo wagombea walipewa katika ngazi za chini.

  Alisema kamati hiyo imebadilisha alama hizo kwa wagombea wengi na kutoa alama nyingine kulingana na umakini wao mbele ya fomu na kwamba, kikubwa kilichokuwa kikitakiwa ni jinsi ya kuwatendea haki wote.

  Mwenyekiti huyo wa CCM alisema wagombea wengi wa safari hii ni wasomi na watu waliobobea katika taaluma mbalimbali.

  "Waliogombea nafasi za CCM pekee ni 2,853 na kwa nafasi za jumuiya ni 2,104 idadi inayoonyesha watu wanakikimbilia chama chetu. Kwa idadi kama hiyo unatakiwa kuwa makini zaidi katika kupitia majina yao na kujiridhisha kwa dhati kwa nini kapendekezwa huyu na huyu kaachwa?"

  Takukuru yautupia jicho uchaguzi CCM


  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru), Dk Edward Hoseah amesema taasisi yake inafuatilia kwa karibu uchaguzi huo ili kubaini watu wanaotumia rushwa.

  Dk Hoseah alisema hayo jana wakati alikijibu hoja mbalimbali za washiriki wa kongamano la kujadili utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kupambana na rushwa nchini na mapendekezo yanayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu (2012 – 2016).

  "Tatizo ni kwamba wagombea wengi wa nafasi ya uongozi wamekuwa wakijiandaa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi na kwa bahati mbaya hata wananchi ambao ni wapiga kura ni kama wanajiandaa kupokea rushwa kila uchaguzi unapokaribia, hili ni tatizo kubwa," alisema Dk Hosseah na kuongeza:

  "Tunaendelea kufuatilia lakini ni kazi kubwa kwelikweli kwa mfano, sasa tunafuatilia uchaguzi wa ndani wa CCM na tunafanya hivi ili kuhakikisha kwamba hatupati viongozi wanaotokana na rushwa, maana tukiwa na viongozi wa aina hii hatuwezi kushinda vita hivi."

  Hata hivyo, alisema rushwa ni tatizo linalovigusa vyama vyote na kwamba lengo la taasisi yake ni kuwachukulia hatua wote wanaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

  Tuhuma za watendaji Tanesco

  Dk Hoseah alisema taasisi yake, imekamilisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi ya watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kuzifikisha taarifa za uchunguzi huo kwenye mamlaka zinazohusika.

  "Kazi ya kuchunguza tuhuma dhidi ya watendaji wa Tanesco nimemaliza na tayari nimeshazikabidhi kwa mamlaka zinazohusika. Mimi siwezi kutoa nilichokiona katika taarifa ile kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru Kifungu cha 37 ambacho kinanitaka nikimaliza kazi niwasilishe ripoti kwa mamlaka zinazohusika na si kutoa kilichopo ndani," alisema Dk Hoseah.

  Sheria ya Takukuru Kifungu cha 57, inaitaka taasisi hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake, kuwasilisha jalada husika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), ambayo ina mamlaka ya kuruhusu tuhuma husika kufikishwa mahakamani au la.

  Suala la DPP kuwa kikwazo cha mashtaka hayo jana pia liliibuka katika mkutano huo wa wadau ambao walionyesha shaka ya kufanikiwa kwa vita dhidi ya rushwa katika mazingira ambayo yanathibitisha kuwapo kwa vita ya maneno kati ya Ofisi za Takukuru na DPP.

  Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha kuwapo kwa mvutano baina ya ofisi hizo akisema ana wajibu wa kuujulisha umma hatua zinazofikiwa katika uchunguzi wa tuhuma mbalimbali na baada ya hapo kazi hubaki kwa DPP kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

  Alisema taasisi yake imefanikiwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha za umma akitoa mfano wa hatua zilizochukuliwa kati ya Januari na Julai mwaka huu na kuiwezesha Serikali kuokoa Sh7 bilioni ambazo zilikuwa zipotee kupitia mishahara hewa.

  Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang'oro Dar; Midraj Ibrahim na Habel Chidawali, Dodoma.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwasababu ya kujua SIRI za VIONGOZI wa CCM kujulikana na Baadhi ya Wabunge na Haswa Mwanasheria

  Mkono CCM inaendeshwa BILA Demokrasia... Ni UBABE, KUJUANA kwahiyo it is a CULT
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,896
  Trophy Points: 280
  DPP ni kibaraka wa rais,hakuna kesi itakayofunguliwa yenye kuhusu mafisadi kabla hajamwuliza rais maoni yake endapo kuna watu wake watakuwa wameguswa,ama hata yeye mwenyewe.Mfumo huu haufai hata kidogo,na hakuna haki itakayotendeka,hapo ni kiduku tu.

  JK ndo aliyemteua DPP na hakuna kesi inayofunguliwa bila idhini ya DPP.
   
 4. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Mkono ni mbabe kwa ccm, Nape au Kikwete mnabisha?? Ondoeni jina lake mkione cha moto, madudu yenu yote nje!!
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Cheza na Mkono wewe? Aliwaambia CCM patachimbika. Naona imebidi wakuu wanywee.
   
 6. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  madhara ya mkono kuondoka yangekuwa makubwa kwa ccm!
   
 7. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Aisee!wameona hapatatosha wakarudisha jina lake!
  Kwa mantiki hii mnyonge ataendelea kuwa mnyonge daima!
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hao ndio ccm bana! Mnyonge anyongwe na mbabe abebwe!
   
 9. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kumbe kujua maovu ya viongozi ni mtaji mkubwa ndani ya CCM.
   
 10. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata huyo Nimrod sio muungwana, kama anayajua maovi tunayofanyiwa watanzania iweje ayafiche kwa ujira wa cheo?
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Si kuondoka Mkuu, wanaogopa asije akamwaga ugali iwapo wangemmwagia ka-kitoweo chake.
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kama kuna kansa kuu nje ya ulingo wa siasa ndani ya nchi hii ni huyu Hosea na mwenzake Felesi( sina hakika kama hilo ndilo jina lake sahihi huyu DPP)! Hata anachokifanya Hossea hapo ni upuuzi mtupu wa kuendeleza vita vyake vya maneno na DPP ili kuonesha ndie chanzo cha kukwama kesi za rushwa ni huyu DPP! In short, wote DPP na Hossea ni kansa sugu.
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Kiduku, bongofleva, mchiriku alhasiri kila mtu aonekane anafanya kazi.
  Nani atamnyooshea kidole mkuu wa majeshi mstaafu kama ikitokea!

  Huu upuuzi wa kufanya kazi na magazeti ni wa kusikitisha sana. Kinachoudhi sana anayefanya hivyo ni PhD holder!
  Hosea bado hatujakusahau na taarifa ya Richmond sasa unakuja na single nyingine. Hakuna lolote unalofanya likaonekana zaidi ya kucheza na vyombo vya habari. Ukikaa kimya unatusaidia kuliko kuendelea kututia hasira.
   
 14. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,367
  Likes Received: 8,382
  Trophy Points: 280
  Keshasema ccm haifi lazima wanakiweka hapo waendelee kuwepo wakitoka wamekufa
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mbona jina lake limeishawahi kukwatwa kwenye Jumuiya ya Wazazi.
   
 16. b

  bagwell Senior Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo TAKUKURU inakwenda kufanya nini kwenye uchaguzi, mbona wao ndio wanaolula Rushwa wakubwa....
   
 17. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  mbona wameshindwa kulikata sasa hivi baada ya kupiga mkwara,..labda kipindi hicho hakupiga biti
   
 18. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaa, ni ngumu sana kwa CCM kuvuana gambaz! Hizo ni ndoto!
   
 19. m

  malaka JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Du yaani CCM ndio inazidi kujichimbia kaburi. Kumbe ukijua siri zao lazima uwaendeshe!! Safi sana Mkono.
   
 20. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Nimrodi alikuwa na uwezo wa kuifuta CCM kwenye medani za siasa endapo jina lake lingekatwa Nimrod ni machine nyingine angevua ile kofia yake kama ya mganga wa kienyeji wangekoma
   
Loading...