CCM yaliteka jiji la Arusha - Jan 26, 2014

CCM yaliteka jiji la Arusha - Jan 26, 2014

Not in use

Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
6
Reaction score
2
Mkutano mkubwa wa na wa kihistoria wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani wa CHAMA CHA MAPINDUZI kata ya Sombetini utafanyika leo soko la Mbauda.

Kipenzi cha watu, homa ya CHADEMA Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri wa fedha atafungua kampeni hizi pamoja na viongozi wengine wa mkoa.

Mama yetu Mh.Chatanda atatema cheche. Baada ya hapo tutafanya maandamano mji mzima .Rasmi tumekuja kuizika CHADEMA Arusha.

Kaa mkao wa kula nakuletea live yatakayojiri.

-------------------------------

Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Mh;Mwigulu Nchemba ameshawasili Jijini Arusha Mchana huu akitokea Kiteto na Babati kwaajili ya Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani zinazoendelea nchi nzima,Chaguzi hizi ni ndogo kwaajili ya kujaza nafasi za Madiwani waliojiuzulu na wengine kufariki.
149339_654757834586291_9032614_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu CCM Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Mgombea wa Udiwani Kata ya Sombetini WIlaya ya Arusha ndugu David,Hapa akiwa kwenye maandamano kutokea Ofisi za chama hapa Sombetini kuelekea Viwanja vya Mkutano,Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.

1530466_654757727919635_810483619_n.jpg
Mh:mwigulu Nchemba akipata mapokezi mazito kutoka kwa maelfu ya wananchi waliomiminika Viwanja hivi vya Soko la Mbauda kwaajili ya Mkutano wa hadhara wa kampeni za Udiwani.
1546468_654757681252973_623286997_n.jpg

Mapokezi yanaendelea hapa Soko la Mbauda kwaajili ya kuanza mkutano wa hadhara.

1743598_654757497919658_124467756_n.jpg

Sehemu ya Mamia ya Wananchi wakiwa tayari kusikiliza Mkutano huu wa hadhara kwaajili ya Kampeni za Udiwani kata ya Sombetini jijini Arusha.

1551756_654757531252988_1962922630_n.jpg

Wananchi wanaendela kumiminika kwenye viwanja hivi vya soko la Mbauda kwenye Mkutano wa Hadhara wa CCM kumnadi mgombea wa CCM kwenye Kinyang'anyiro cha Udiwani.


 
kwa heading hiyo ni wazi utakuwa wa kihistoria!
 
Bado vikao vya hapa na pale vya kufanya logistics vinaendelea.Na muda muafaka ukifika ntawajuza rasmi.Baadhi ya makada wetu nimeongea nao hapa wanaonyesha furaha sana.Pongezi kubwa kwa kamati ya maandalizi
 
safi sana, tumechoka na hawa wanaozunguka na chopa, na tukiwapa nchi je, mboye alijidai kukataa shangingi kumbe alikua anataka helicopter , ccm haina mbadala chama cha wananchi wanyonge, ccm mali yetu, tutailinda KWA nguvu zetu zote,

 
Leo madereva wa arusha kaeni mkao wa kula maana magari yenu ccm wata yakodisha kuwa beba wanachama wao na wasio wanachama,ila wanajisumbua kwakua watapata hasara bure
 
Hatuendi piga pombe leo?
Ingekuwa mtu mwingine bora ila mwigu hapana namuogopa kama CCM?
 
Poleni ccm mbona nasikia mmepigana usiku au ndio mnataka kumwonyesha anayekuja kuhutubia kuwa mnayaenzi aliyoyaanzisha?
 
weee hivi ama kweli ccm ni janga la kitaifa kutoka chama tawala kusimamia serikali chakavu ya ccm hadi kwenye mandamano? Kama ndivyo poleni niwashauli jiuneni na chadema kwakuwa mmeshagundua mandamano ni sio vulugu wala fujo
 
Hivi wewe mleta mada unaishi wapi?kama huijui arusha bora unyamaze.unamwita gaidi kipenzi cha watu na hilo limama'
 
hahahahha du! leo hii?
wekeni viti vya kutosha na ubwabwa nitakuja bila kukosa
cc. Arusha one
 
Last edited by a moderator:
Mkutano mkubwa wa na wa kihistoria wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani wa CHAMA CHA MAPINDUZI kata ya Sombetini utafanyika leo soko la Mbauda.Kipenzi cha watu,homa ya CHADEMA Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri wa fedha atafungua kampeni hizi pamoja na viongozi wengine wa mkoa.Mama yetu Mh.Chatanda atatema cheche.Baada ya hapo tutafanya maandamano mji mzima .Rasmi tumekuja kuizika CHADEMA Arusha.Kaa mkao wa kula nakuletea live yatakayojiri.
kwanza jifunze nyakati wakati unaandika unaandika ccm yaiteka badala ya ccm kuiteka tuna wasiwasi na elimu yako au ndo dv 5
 
Hapa hatuna shughuli.kazi ilikuwa 4-0.hapa kama unampeleka mlevi nyumbani
 
Mkutano mkubwa wa na wa kihistoria wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani wa CHAMA CHA MAPINDUZI kata ya Sombetini utafanyika leo soko la Mbauda.Kipenzi cha watu,homa ya CHADEMA Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri wa fedha atafungua kampeni hizi pamoja na viongozi wengine wa mkoa.Mama yetu Mh.Chatanda atatema cheche.Baada ya hapo tutafanya maandamano mji mzima .Rasmi tumekuja kuizika CHADEMA Arusha.Kaa mkao wa kula nakuletea live yatakayojiri.

And for sure this is Not in use anymore in arusha for the time being!
 
Last edited by a moderator:
Dah! Ulitaka kuvuta hisia za watu eee? Nadhan heading ingekuwa, ccm kuiteka Arusha leo?
 
Vipi Mwigulu atakuja tena na ile! mtu yake ya maonesho..!?
 
Back
Top Bottom