CCM yakatakaza wagombea wake kuonekana TBC1, Tido Mhando ataarifiwa

Hii ni dharau kwa watanzania, tatizo la CCM kung'ang'ania vizee kuongoza chama, wakati dunia inakwenda na wakati sisi tumejikita na mambo ya ujima. Kudharau debate kwenye TV na kusifu mikutano ni sawa na kusema hata nikipanda punda nitafika safari bila kujali muda, type ya viongozi kama hawa ndio wanaoirudisha nyuma nchi yetu, ningekuwa na uwezo wa kumkaribia Makamba ningemzaba kibao.
 
Tungekuwa na wananchi wenye uelewa mzuri na wanaojua mambo huo ndo ulikuwa mwisho wa CCM. Naona kama kaburi lao limeishakuwa tayari nawapa up 15 years watakuwa wamezikwa kabisa.

Mkuu lyangalo, 15 years?!!! Kwani umewapa vidonge vya kurefusha maisha?
 
Kama baba anakula bangi basi hata wanaye wanahatihati ya kumuiga
Baba kagoma mdahalo na nyie watoto mnajifanya mna akili kuliko yeye?

Sitashangaa kuona TBC wakisitisha hicho kipindi kwa tatizo la kiufundi au funds au hata kukiendesha hovyo hovyo kipoteze maana
 
Inaelekea hiki chama bado kina wadharau wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi ambao hawawezi kuhudhuria kampeni za chama hicho kwani kwa muda wa kampeni wanakuwa vibaruani mwao. Zaidi ya hayo inaelekea kuwa hiki chama kimekuwa na zile kampeni za kijima hivi hawaoni nchi zilizoendelea wanavyofanya kampeni kupitia televisheni??? Au wanaogopa kivuli chao? Ninavyofahamu mimi televisheni inatazamwa na watu wengi kuliko hizo kampeni za jangwani au sehemu nyingine yeyote. Sasa huyu Makamba anavyosema kuwa midahalo haifai kwani haina watu wengi anajua ni watu wangapi huangalia televisheni kwa wakati mmoja? Na kama si televisheni tungeweza kumfahamu ama kumsikia Rais Obama na sera zake??? Na hii inanileta kwenye kioja kingine cha CCM na serikali yake ambayo bado haijaridhia raia wake wanaoishi nje ya nchi kupiga kura huko waliko. Je hawa wasubiri Kikwete au Pinda atembelee nchi hizo ndipo wajue sera na mipango ya serikali yao??? Yaani tunashindwa na nchi kama Msumbiji??? Ni wakati sasa watanzania waamke na kujua mbivu na mbichi ni zipi.
 
Kweli kabisa ndugu yangu Msanii, "like father, like son"

CCM ni waoga na ndio maana wanaogopa midahalo. Hakuna jipya wanaloweza kuwaeleza wananchi kwakuwa tangu uhuru hakuna lolote la kujivunia lililofanywa na CCM. Ndio maana wagombea wao, badala ya kujinadi kwa mafanikio ya utendaji katika mikutano yao, wanahangaika kutoa ahadi nyingine mpya ambazo watu wote pamoja na wao wenyewe wanajua hawataweza kuzitekeleza.

Makamba naye ubongo wake umetindia, anasahau kwamba ule mdahalo ukirushwa kwenye TV unasambaa katika sehemu kubwa ya jimbo au nchi kuliko mkutano mmoja wa kawe ama Ubungo ama Vunjo. Pia kama kweli wanajiamini, basi wawashinde wapinzani kwenye midahalo na si porojo na umbea wa mitaani. Na hili pia amelifanya Kikwete alipozira kura za wafanyakazi, na wapinzani kutumia kususa huko kama mtaji ndipo akaamua kulamba matapishi yake kwa kutoa hongo kinyumenyume. Ni wapinzani na vyombo vya habari ndio vilivyo istua CCM kuwa, wale wafanyakazi ambao wao wanadhani wako Laki tatu unusu tu, kumbe nyuma yao kila mmoja ana watu kama watano hadi wanane wanao msapoti mfanyakazi huyu. CCM iko dhoofuli hali

ama kwa hakika, CCM ikishinda mwaka huu, itashinda kwa sababu ya UMBUMBUMBU wa wa Tanzania, na si vinginevyo.
 
Nina wasi wasi ata na uwezo wa Makamba kufanya maamuzi ya chama.
It is a common sense kuwa katika uchaguzi wananchi ndio wateja sasa iweje unawakimbia alafu bado unataka kura ZAO.
Seriously speaking nitajitolea kugharimia KOZI FUPI ya customer care.
Kibri inakuja pale akijua fika KUWA asilimia kubwa ya watz ni watu wa kuburuzwa tatizo hasomi ata alama za NYAKATI.
Kuogopa mdaharo ni sawa na kuogopa kura au kumwogopa mteja wako mwenyewe wakti ndie anakufanya uende ******
 
CCM wanakiburi kisicho kifani kwa vipi wanaweza kupinga matakwa ya umma,kuna watu wangapi wanaokosa muda wa kwenda kwenye kampeni,ambao wangenufaika kwa kuwapembuwa wagombea kwa kupitia kipindi cha television cha TBC1,hivi CCM ni na ni katika nchi hii ambao wanadhani wanaweza kupindisha kila jambo la kijamii kwa ajili ya kuwanufaisha wao ili wajipatie kura kwa njia za mkato wanaandikisha namba za kadi za wapigia kurra karibu kila wilaya ili waweze kujaza karatasi zingine za kupigia kura,wanawasomesha wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo waweze kupindisha sheria ili wawapendelee wagombea wa CCM,Jambo hili ni hatari sana kwa mustakabali wa usalama wa nchii,watu wakichoka wtakuja kunyanq'anya nchi hii nchi bila utaratibu mzuri, hakuna atakayepona kati yetu hatutaweza kurudisha amani tuliyonayo,nchi zingine zote zilizoingia kwenye machafuko zilianza baada ya vyama tawala kupindisha kila sheria na utaratibu uliopo ili kujinufaisha kwa manufaa yao na kunq'anq'ania kukaa madarakani hata pale walikuwa hawatakiwi kabisa na wananchi ,tunataka viongozi sio watawala ebu wakome watuachie nchi yetu iliyo salama ,
CCM madebe shinda,hamuna kitu mukichwa zaidi ya maji matupu OVYYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.
 
Makamba awaweka pabaya wagombea CCM
Thursday, 09 September 2010 07:23


Yusuph Makamba
Waandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewazuia wagombea wake wa ubunge kushiriki katika mdahalo unaoendeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuhusisha wagombea wa vyama vyote katika kila jimbo.

Kipindi hicho kinarushwa kila Jumanne kupitia Kituo cha Televisheni cha TBC1 kwa lengo la kuwasikiliza wagombea wakijinadi pamoja na kunadi sera za vyama vyao.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa wagombea wa CCM wamezuiwa kushiriki mdahalo huo kwa barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,Yusuf Makamba kwenda kwa makatibu wa chama wa wilaya na mikoa yote nchini.

"Ninawaandikia kuwajulisha kwamba, wagombea wetu wasishiriki katika aina hiyo ya mdahalo, mpaka hapo mtakapoelezwa vinginevyo.” imesema sehemu ya barua hiyo ambayo nakala yake imepelekwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC.

Hata hivyo tayari wagombea kadhaa wa ubunge wa CCM wameshiriki kipindi hicho kilichoanza kurushwa hewani mbili zilizopita kwa kuwakutanisha wagombea ubunge wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.

Baadhi ya wagombea ubunge wa CCM waliokwisha shiriki mdahalo huo ni pamoja na Hawa Ngh’umbi wa Jimbo la Ubungo na Chrispin Meela anayegombea ubunge katika jimbo la Vunjo.
"Kipindi hicho kimerushwa hewani kwa mara ya kwanza katika Jimbo la Ubungo Dar es Salaam na mgombea wa CCM alishiriki, sijui kwa maelekezo ya nani. Sina tatizo na kipindi. Nina tatizo na ushiriki wetu," ainasema sehemu ya barua hiyo ya Katibu Mkuu.

Katika kipindi hicho wagombea ubunge wa vyama mbalimbali huulizwa maswali na wasikilizaji na watazamaji wanahudhuria katika mdahalo huo.

Kipindi hicho kiliporushwa kwa mara ya kwanza katika Jimbo la Ubungo, mgombea wa CCM (Hawa Ngh’umbi )alipata wakati mgumu kujibu maswali ya watazamaji wa kipindi hicho na kuishia kupandwa na jazba nakutishia kumshitaki, mtu aliyemuliza swali gumu.

Katika barua yake hiyo ya Agosti 31, mwaka huu, Makamba licha ya kukitilia mashaka kipindi hicho na alihoji mgombea wao wa Ubungo alishiriki kwenye mdhahalo huo kwa maelekezo ya nani.
Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kwamba agizo hilo la Makamba limeanza kutekelezwa, juzi mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo la Arusha Mjini, Batilda Buriania hakushiriki kipindi hicho.

Hata hivyo, Batilda alisema hakuhudhuria mdahalo wa Arusha kutokana na chama chake kutopewa taarifa na yeye ni mgombea wa CCM sio mgombea binafsi.


“Nimekuwa nikitumiwa ujumbe wa simu kuwa nimeingia mitini katika mdahalo…mimi siwezi kuingia mitini nimedhuria midahalo mikubwa tena ya kimataifa ndani na nje ya nchi siwezi kukimbia hivi sasa,”alisema Dk Batilda.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CCM/OND/SG/194/9 ya Agosti 31 ambayo Mwananchi imefanikiwa kuiona, Makamba aliwaambia makatibu hao wa CCM kuwa wagombea wote wa chama hich wasishiriki kipindi hicho hadi CCM itakapotafakari kwa kina manufaa itakayopata kwa kushiriki kwao
Alisisitiza kuwa CCM ina utaratibu wake wa kujinadi na kunadi sera zake kwa wananchi ambao anaamini kuwa bado unakidhi haja.

“Tuna utaratibu mzuri wa kijinadi na kunadi sera zetu kwa wananchi; utaratibu wa mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani. Utaratibu huo bado unakidhi haja. Tunaendelea nao,” alisema Makamba.

Akizungumza na gazeti hili jana, Makamba alisisitiza akisema: "Hatutaki. Tumekataa ndio. Sisi yetu ni mikutamo ya hadhara. Tutaeleza huko malengo, ilani yetu na sera zetu kwa wananchi. Hatuoni sababu ya kukaa katika chumba kidogo na kuwapa nafasi ya ushiriki watu wachache."

Aliendelea: "Hatuoni sababu ya kwenda kwenye huo mjadala kwa kuwa mikutano yetu ya hadhara inajitosheleza."
Alipotakiwa kueleza kama chama kitawachukulia hatua wagombea wake waliokwishashiriki kipindi hicho, Makamba alijibu: "Hakuna adhabu watakayochukuliwa kwa sababu chama kilikuwa hakijatoa maagizo."

Taarifa zilizopatikana baadaye jana zilieleza kwamba, agizo hilo la Makamba pia limepokelewa katika jimboni Karatu ambako mgombea ubunge wa CCM aliamua kujitoa kwenye mdahalo huo juzi.

Mdahalo wa wagombea wa jimbo hilo, ulipangwa kufanyika juzi katika ukumbi wa maendeleo Karatu, lakini wakati wagombea wengine wakiwa wanajiandaa, taarifa zilitolewa kuwa mgombea wa CCM, Dk Wilbard Lorry hawezi kuhudhuria.

Viongozi wa vyama vya Chadema na CUF, katika wilaya hiyo, walilalamikia kuahirishwa ghafla kwa mdahalo huo wakati walikuwa wamesitisha kampeni vijijini na kurudi Karatu.

Katibu wa CUF Wilaya ya Karatu, Stivin Siay alisema chama chao kilikuwa kimemwandaa mgombea wake kwa mdahalo huo.

“Tunashangaa kujiondoa kwa CCM katika mdahalo huu kumesababisha mdahalo kuahirishwa…,” alisema Siay.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe alisema walipata taarifa za kuahirishwa mdahalo huo dakika za mwisho kwa maelezo kuwa mgombea wa CCM hatahudhuria.

Alisema taarifa hizo kwanza zilipatikana ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, ambao ndio awali walitoa taarifa za kuwepo maombi ya TBC kuandaa mdahalo huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Karatu, Clemence Berege akizungumzia kuahirishwa kwa mdahalo huo alisema kwamba, ofisi yake haihusiki kwani waliotaka kuendesha mdahalo huo ni TBC.

CCM wanajitafutia kaburi
 
CCM kuogopa mdahalo ina maana hawataki kura zetu? wanategemea mabango ndiyo yatawapa kura? ninaomba vyama vingine muendelee na midaharo ili wanachi waweze kusikiliza sera zenu. Kati ya viongozi watakaoiangusha CCM ni pamoja na Makamba sijui kwa nini CCM wamemng'ang'ania. SHAME ON YOU MAKAMBA!
 
Msishangae iwapo TBC wataamua kutoendesha kipindi hicho kwa kuwa CCM hawataki kushiriki.

Keil, uwezekano huo ni mkubwa sana, i can say kwa TIDO huyu aliyepo ni 80% litatokea hilo ili asiwa aibishe mabwana wakubwa zake
 
Like father like son. Kama baba yao (JK) amekacha mdahalo we ulitegemea watoto wake wangeweza??? Wao wanataka wapewe nafasi ya kudanganya watu na wasiulizwe maswali ya ukweli. Si unajua tena kwenye mdahalo huwezi kupanga watu wa kukuuliza maswali!!!! Hahahaaaa, SISIHEMU mwaka huu mnalo. Lakini najua mtachukua ubunge kwa wizi wa kura kama ilivyo desturi yenu
 
Wanajua wanachokifanya, si uliona yaliyotokea kwa mdahalo uliopita!!!

Yaani kama na hili wananchi hawaoni basi ten!! lol!
 
Tungekuwa na wananchi wenye uelewa mzuri na wanaojua mambo huo ndo ulikuwa mwisho wa CCM. Naona kama kaburi lao limeishakuwa tayari nawapa up 15 years watakuwa wamezikwa kabisa.

Kuna haja ya kuwaeleza wananchi hili!! Maana sioni sababu ya Makamba kama ni valid!! lol!
 
... Mwenye dhambi nyingi hujificha, hata asipofuatwa na mtu!!:smile-big:

:llama:Whoever Sent Me Here Sent a Reason Home!:llama:


Mkuu hii signature yako inanikumbusha jamaa mmoja anaitwa MS.
tehe tehe tehe..................
 
Back
Top Bottom