KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
CCM bado kinajiendesha kama chama cha Kikomunisti. Msisahau uhusiano uliopo kati ya CCM na wakomunisti mahali pengi duniani. CCM wameshindwa kufanya ukomunisti Tanzania lakini hawajakosa mbinu kadhaa kutoka vyama vya kikomunisti walizozibeba ambazo wanaendelea kuzitumia.
Mojawapo ya mbinu ya kikomunisti ni hili la chama kuchukua hatamu na serikali na vyombo vyake kubaki kama mawakala wa vyama vya kikomunisti. Kwa kawaida chama cha kikomunisti huwa hakihitaji nguvu ya umma, kinahitaji waaminifu waliolishwa kiapo rasmi ndani ya chama ambao huwa ndo nguvu ya chama. Watu hao ndo huingia serikalini kufanya kazi za chama. Kwa ujumla ni vigumu sana kutenganisha chama cha Kikomunisti na serikali ndo maana unaona mwenyekiti wa chama ndiye rais. Matamko ya viongozi wa chama siku zote huwa ni amri kwa serikali.
Sasa CCM wameona midahalo inawafunua jinsi walivyo na wagombea dhaifu wanaopewa nguvu na chama dola. Wagombea hao katika mazingira ya kawaida wasingeweza kushinda. Ila nguvu ya chama dola itatumika kuwasimika madarakani utake usitake. Midahalo hii inawaweka wazi kwa watu kuwa hawana uwezo. Kwa hiyo amri ya chama ya kuwataka CCM wasishiriki midahalo ni amri kwa chombo cha umma TBC kufuta midahalo hiyo. Subirini mtaona yatakayofuata, kipindi kitaondolewa, au kubadilishwa ili kukosa mwelekeo.
Kutenganisha chama na serikali ni mojawapo ya mafanikio ya mifumo ya kidemokrasia popote duniani. Mahali ambapo hakuna demokrasia, serikali na chama hubaki kuwa kama kitu kimoja. Hali hii ndo ipo hapa Tanzania.