Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,312
Zoezi la Uandikishaji wapiga kura au ubooreshaji wa daftari la wapiga kura limegeuzwa kuwa mkakati wa ushindi wa mezani kwa chama tawala. Nikiwa wilaya ya Manyoni ktk mji mdogo wa Mitundu nimeyashuhudia haya. Kwanza Uandikishaji ulianza kimya kimya Bila taarifa yoyote ya msingi kwa umma. Shukrani kwa gari la matangazo la CHADEMA lililokuja jumamosi jioni na kuzunguka likihamasisha watu kujiandikisha. Pili ni Tatizo la mashine, siku ya jumamosi Uandikishaji ulianza kwa mashine moja tu na ya pili ilianza kazi saa 11 jioni, saa 1kabla ya kusitisha Uandikishaji. Tatu ni utaratibu unaotumika, mtu akifika kituoni anajiandikisha na kusubiri kuitwa jina. Yule anaeita majina amekuwa akiita majina kwa mlengo wa kiitikadi zaidi na si nani kawahi. Nne ni mkakati ulioandaliwa kuwaandikisha Muda wa usiku wapenzi, mashabiki na wanachama wa Chama tawala. Kituo hiki kitaandikisha watu kwa siku 7 na mji mdogo wa Mitundu una watu zaidi ya elfu nane wenye sifa za kuandikishwa. Sijui ni kwa muujiza upi wataweza kuandikisha watu wote hawa kwa mashine 2 tu zilizopo hadi sasa. Binafsi naona huu ni mkakati wa ushindi wa mezani kwa CCM. UKAWA mna wajibu wa kulitupia jicho suala hili na kulitafutia ufumbuzi wenye tija.